Kwa ufupi kabisa,
Wenje anaposema Kamati Tendaji ya Kanda ya Kati ilimwondoa Lissu kwenye Uenyekiti wa Kanda ni kinyume na Katiba ya CHADEMA kwani mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Kanda ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ni Kamati Kuu au Baraza kuu sio Kamati Tendaji ya Kanda.
Haya hapa maneno ya Wenje,
"Lissu amewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kati, alihudumu kwa mwaka mmoja, Kamati Tendaji ya Kanda ikamfukuza, hakufanya chochote kwenye Kanda, sasa anataka uenyekiti wa Chama Taifa. Ninawaambia leo Lissu akiwa Mwenyekiti wetu wa Chama Taifa ndani ya mwaka mmoja wanachama wenyewe wa Chadem ndio wataandamana kwenda kumfukuza."