Pre GE2025 Wenje akiri kufahamiana na Abdul (Mtoto wa Rais) na ana mawasiliano naye

Pre GE2025 Wenje akiri kufahamiana na Abdul (Mtoto wa Rais) na ana mawasiliano naye

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
View attachment 3180908
Baada ya Miezi zaidi ya mitano Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu kutuhuma hadharani kwamba kuna hela za Mama Abdul na Abdul zilipelekwa kuvuruga uchaguzi wa Chadema.

Lissu pia akaenda mbali zaidi na kuanza kutaja watu na miongoni mwao ni Mtu anaetajwa alikuwa ndiye Dalali wa kuunganisha hizo hela ni Mhe Wenje ambae ni Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria na mjumbe wa kamati kuu na ndiye alimpeleka Abdul nyumbani kwa Lissu kwa kusudio la Kumuhonga

Mhe Wenje kwa miezi yote hiyo hajawahi kutamka wala kuelezea tuhuma hizo dhidi yake usipokuwa leo amekubali ombi la team ya Habari online Star Tv kusema haswa kipi ni Mbivu na kipi n mbichi

Tumefanya nae Mahojiano Maalumu kupitia Habari Star TV

Tumetaka kujua Abdul ni nani kwake Wenje

Tumetaka kujua ilikuwaje mpaka Lissu,Abdul na yeye wakakutana nyumbani kwa Lissu

Katika interview wenje amekiri wazi anamfamu Abdul kuwa ni mtoto wa Rais na anamawasiliano nae je swali walienda nyumbani na hela za kuhonnga?

Tukutane baadae mzigo utakuwa hewani
Niko hewani tayari, team ya MBOWE imejaa vilaza, walafi na wala rushwa... Kick them off now
 
You may thought that,.....!
Lugha ngumu hii, kwanini usiandike lugha unayoijua badala ya kukera na pumba hizi?
Incriminations of democracy 🤣😀😀 hata sielewi alikuwa anataka kusemaje!!! kwani si heri angeandika kilugha cha kwao ingekuwa poa tu kama hawezi kuandika kiswahili kuliko kupelekea aibu ndogondogo kwenye ukoo wao 🤔
 
Abdul aliongozana na wenje ,

Chadema Kuna utapeli
Wenje,mbowe,Lema,msigwa ni malaya wa kisiasa. Lisu amekosa chama sahihi, wengi wa wajumbe wa mkutano mkuu wananunulika, wengine hata Tzs 50,
You may thought that,.....!
Lugha ngumu hii, kwanini usiandike lugha unayoijua badala ya kukera na pumba hizi?
KINGEREZA CHA MMKWA
 
You may thought chadema under Freeman Mbowe, fought for incriminations of democracy in Tanzania!
#Hillo ni genge lenye maudhui ya kujinufaisha na familia zao, chadema ile ya ahadi, italetwa na Lissu!
Hicho 'kidhungu' bwana nenda kafanye mazoezi zaidi. Tumia hii lugha yetu nzuri tu inatosha kueleza vizuri tu unayo taka kutufahamisha juu yake.
Si mara ya kwanza, nimekusoma mara kadhaa ukiboronga tu kwenye lugha hiyo.

"You may think chadema under Freemani Mbowe fought for 'incriminations' (promotion?) of democracy in Tanzania"... Sasa sijui ulitaka kusema nini hapa, maanake hata sentensi yenyewe ime baki ikielea tu hewani!
 
Wenje kanisikitisha sana!
Tofauti kidogo na Msigwa, yeye nilidhani anayo nafuu kidogo kwenye upuuzi wa namna hii!

Najuwa huko ndani ya CHADEMA watu wa aina hii wamo wengi tu, ndiyo maana waTanzania wengi kusita kukiamini chama hiki hadi sasa.
Lakini, ni wazi ukiwa huko juu kabisa, huku chini ndipo panaoza kabisa.

Kwa hiyo hawa ndio "wajumbe wa Kamati Kuu" ambao ndio wanatakiwa kuamua maswala muhimu ya chama?
Walitaka Tundu Lissu awe anawasilisha habari huko zimaliziwe huko huko ndani! Huo ndio ujuha wenyewe.
 
Tudokezee kidogo ndugu mwandishi.

Maana Yericko Nyenyere anadai eti Abdul alienda kwa Lisu kuchukua nyaraka ili alipwe fedha zake. Really??? Abdul ni nani serikalini?

Huyu Yericko Nyenyere anatuchezea akili watanzania
Yericko naye amefanikiwa kuchekecha kwa mwenyekiti hatimaye kufaulu kujipatia kagorofa kake Game of fews bright men makonki master
 
Back
Top Bottom