CHangamoto aliyokuwa nayo msigwa wkt huu ni kubwa sn, pote kwa sasa haaminiki isipokuwa nafuu yake kidogo ni kurudi alipotoka. Kwa nn?
Kwasababu adui mkubwa wa ccm kwa sasa ni mwenyekiti wa chadema ambaye msigwa ni rafiki yake na anamkubali na pia alimpigia chapuo ashinde uenyekiti sasa u can imagine how msigwa yupo kwenye bad spot.
Ccm hawakutaka hata kidogo lisu awe mwenyekiti wa chadema fikiria mtu waliyejaribu kumuua kwa kumpiga risasi nyingi mwilini, kumnyima matibabu na kumletea kila aina ya shida duniani leo yupo hai na ameshinda uchaguzi ktk mazingira magumu kama yale unafikiri viongozi wa ccm watataka kuona miongoni mwa makada wao wana urafiki wa karibu na lisu?
Kimsingi tangu lisu alipochaguliwa kuwa mwenekiti wa chadema na msigwa alishatengwa ccm, atawekewa ma shushu, simu yake itawekewa vinasa sauti na hata aminiwa tena hata afanyeje ndani ya ccm, hatakuwa na raha tena ndani ya ccm na akiendelea kuwa huko stress, na hata kupelekea stroke vitamkuta huko.
Ni wkt sahihi kwa msigwa kutakari kwa sasa ni nini cha kufanya wkt huu. Anazo option tatu achague moja
Kwanza anaweza kustaafu siasa akajiweka pembeni na masuala yote ya siasa, atafute mfumo mwingine wa maisha wa kumuingizia kipato.
Pili arudi alipotoka atubu kwamba alikosea ni jazba tu na moja mbili tatu kwakuwa bado lisu ni rafiki yake atapokelewa japo kaheshima fulani alichokuwa nacho kabla ya kuhama kitashuka,
Tatu abaki huko huko na ya mkute mabaya kwakuwa mchumia janga hula na wakwao