Wenye hela benki kuweni makini na akaunti zenu

Manager kisa kiko wapi isije ikawa ni marketing war!!?
Is not marketing war. Mtoa taarifa ni mtu wa kawaida sana. Anasimamia akaunti ya taasisi.

Nimejua kwa sababu naidai taasisi hiyo. Muda walioahidi kunipa hela yangu ulipofika nilipoona kimya, nikwashtua ndo wakanipa kisa hicho na kwamba imeshindikana hadi kesho yake.

Iko hivi: alikwenda benki kutoa hela kwenye akaunti ya taasisi hiyo. Katika process za kuchukua hela hiyo, lazima uanze kwa kuchukua benki statement. Hapakuwa na shida kwani benki statement ilionesha fedha ipo.

Kuingia kwenye mfumo wa serikali wa malipo, fedha iko kidogo kuliko bank statement. Ikalazimu kumwona msimamizi yaani idara ya fedha ngazi ya halmashauri.

Akasema taasisi hiyo ilishafanya malipo kwa mtu fulani siku chache zilizopita.

Kwa bahati mbaya malipo hayo yalifanywa kwa chek ambayo siyo ya taasisi hiyo wala hakuna document yoyote iliyoandaliwa na taasisi hiyo kuidhinisha malipo.

Jiulize, benk statement inaonesha hela zipo, lakini fedha kwenye akaunti iko pungifu. Nani anaweza kufanya hilo kama si wao?

Nimewashauri wapeleke malalamiko polisi ili niwatafutie msaada wa kisheria ikiwa ni pamoja na kudai fidia kwa usumbufu kwani wameenda mara mbili kufuata hela wakawa wakiambiwa amount ya chek ni kubwa kuliko kiasi halisi kwenye akaunti.

Si vita ya kibiashara, ni tukio la kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Upuuzi huu umekuwa mwingi sasa tena hasa kwa NMB
 
Bank ni majizi kwa matukio yaliyonikuta
Nilikuwa naweka kila wakati kama 10m au zaidi kwa mzunguko ya biashara

Sasa mnajua mteja anakuja kahesabu hela zake, na mimi nahesabu ninapopokea
Baadae nazihesabu tena ili ziende Bank hapo tumeisha hesabu mara 4

Unafika bank unampa teller anahesabu kwenye machine halafu anasema kuna 10,000 hakuna

Hapo unasema labda kweli unatoa mfukoni unampa
Ilijirudia kwa wafanyakazi kama watatu
Siku hiyo tumehesabu wawili hela zote kufika eti ten hamna
Nilipiga kelele na kuwaita wote waizi
Waliona aibu sana mpaka GM akaja kuniomba yaishe
Ila hawakuchukuliwa hatua zozote naona wote lao moja

Siku nyingine mmoja wao eti ananipa 10,000 akasema imezidi nikamwambia Chambo hiyo eti [emoji1] [emoji1787]
 
Hueleweki. Bank statement ni taarifa za akaunt katika karatasi au softcopy. Unavyoelezea ni as if akunti ni box fulani lenye pesa wakati ni taarifa tu. Embu eleza vzr hapo unaposema bank statement fedha zipo ila kwenye akaunt hazipo.
 
Hueleweki. Bank statement ni taarifa za akaunt katika karatasi au softcopy. Unavyoelezea ni as if akunti ni box fulani lenye pesa wakati ni taarifa tu. Embu eleza vzr hapo unaposema bank statement fedha zipo ila kwenye akaunt hazipo.
Benk statement inatumika kama reference kuingia kwenye FFARS.

Unaandaa malipo kulingana na kilichomo katika benk statement. Unapitisha chek kwa mamlaka husika. Unapoenda benk kuchukua, wanaangalia wanakwambia hela iliyoko kwenye akaunti ni kidogo kuliko unachohitaji kuchukua.

Yametokea hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hujaweka kisa
 
[emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…