Wakati wabongo wanaanza kuingiza magari used kwa wingi, jamaa yangu mmoja alinunua benzi lake, ki-mwonekano lilikuwa ni zuri kweli kweli. Baada ya mwezi akaliweka kwenye mawe na halikufufuka tena. Hoja yako inaangukia kwa watu kama hao. i.e. watu wasio na uwezo wa kumiliki gari lakini wanajikakamua kununua ili kuonyesha makapuku ''cha moto'', kuwaringia. Kwa kifupi ni ulimbukeni. Ukisikia mtu analia ''hii gari inakunywa mafuta mno'' (kama aliambiwa gari inakunywa maji) au ni ndoa ya kikatoliki, haliuziki etc jua amenunua kitu asichomudu gharama zake. BTW kumiliki gari ni gharama za uendeshaji, kununua ni step ndogo sana. Ile helkopta ya Musukuma ''mbunge'' bado ipo?