DOKEZO Wenye Hospitali binafsi wakataa kuwahudumia wateja wa NHIF kutokana na vifurushi vipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huu ni uonevu mkubwa sana hasa kwa watumishi wa umma ambao hawana uchaguzi wa kuchagua kutumia bima binafsi au bima ya serikali. Mfanyakazi anachangia kila mwezikwa kukatwa mshahara wake,badala ya kuboreshewa mafao ya matibabu unakuta mfuko unafanya mambo ya kisiasa kwa kutumia michango ya wanachama.

Unakuta eti mkurugenzi wa bima anatoa mashuka au vitu vya miundo mbinu za hospitali
ambazo kimsingi hazitakiwi kugharimiwa na michango ya wanachama,michango inatakiwa
itumike kuboresha vitita vya huduma kwa mchangiaji,
Matumizi hayo huwa nayaona ni kama hongo kwa viongozi ili hao wakurugenzi waendelee kupewa nafasi za kiuongozi
.Jambo hili linawatesa wachangiaji wa mifuko hii.

Endapo hospitali binafsi zitafunga huduma kwa wachangiaji,italeta tatizo kubwa sana
kwetu watumiaji wa huduma. Nashauri taasisi za serikali nazo zianze kununua huduma
kutoka kampuni binafsi za bima ili kuepusha watumishi kuwa wahanga wa mivutano kati ya NHIF na hospitali za binafsi,
 
Impossible mission
Nakubaliana na wewe,hospitali nyingi za serikali zipo tangu uhuru lakini huduma siyo nzuri,
Kwa magonjwa kama kansa,kama umeandikiwa mionzi nenda kalinganishe huduma kati ya ocean road
na besta ile hospitali ya wachina kinondoni. utagundua hata lugha za watoa huduma zinatofautiana kabla hatujazungumzia mitambo.
 
Upo sahihi mkuu Agakhan hawapokei NHIF nikasema sirudii tena kukata hiyo bimaHapana Agakhan hawapokei NHIF ninayo timiza nililipia 1m point something nilienda kwa ajili ya meno walinikatalia hawapokei nikaenda Hindu Mandal
Labda kama wameanza siku hizi. Mama angu alitibiwa mwaka jana aghakhan na yeye ana bima ya nhif ya mtumishi. Gharama yake ya matibabu ilikua karibu laki 9.
Kitu kingine nhif watu wa bima za vifurushi wanakua kama wana nyanyapaliwa. Chunguza utakuja kuniambia
 
Labda ulienda zile polyclinic za aga khan ila aga khan yenyewe hawapokei nhif miaka mingi sana
 
sio private hospitals ni zipo chini ya CSSC, APHTA sio CSSC. Pia CSSC wametoa tamko kukubaliana na kitita usichanganye habari. Pia hilo tamko APHTA wamelikataa.
Hawana uwezo huo.Usisahau hata KCMC,BUGANDO NA MBEYA ni Private ..
 
Mbona kuna hospitali nyingi tu za binafsi hasa za Wahindi huwa hazipokei wagonjwa wenye Bima za afya za NHiF tangu zamani?
Nahisi Wahindi walishaweka wizara husika mfukoni mwao
Hospitali ya wahindi iliyokuwa inaleta shida na NHIF ni Aga Khan pekee ila mwaka juzi walikubali ila kwa bima zenye supplementary packages. Kumbuka NHIF ni sehemu ya wizara ya afya na hakuna hospitali inatoa huduma pasipo ruhusa ya wizara ya afya. Acha kukariri.
 
Labda ulienda zile polyclinic za aga khan ila aga khan yenyewe hawapokei nhif miaka mingi sana
Kwanza naomba uelewe, bima unaotumia ni ya kifurushi hivyo hata ungetoka nyumbani moja kwa moja kwenda Bugando, Muhimbili au Ekenywa ungekataliwa. Kufika huko ni kupitia mfumo wa rufaa tu. Ukishapewa rufaa ndio unaweza toka kwenye hospitali ya rufaa kwneda za kanda au taifa. Pili, Aga Khan wanapokea kadi za bima ya afya ya NHIF ila kwa wanachama wanaotumia packages za ziada na si za standard au vifurushi.
 
Serikali imehujumu watoto wa nchi hii, imefuta BIMA toto. Mamilioni ya watoto wanapata tabu.

Rudisha Bima toto NHIF
Mamilioni wapi wakati wanachama wa Toto Afya hawakufika hata 300,000 Tanzania nzima
 
Serikali walishakaa mezani na bado hawajafanya kama maridhiano.yalivyotaka
 
sio private hospitals ni zipo chini ya CSSC, APHTA sio CSSC. Pia CSSC wametoa tamko kukubaliana na kitita usichanganye habari. Pia hilo tamko APHTA wamelikataa.
Hiyo barua wamekubaliana na Tarehe 27 barua ilitoka wakatoa tamko la pamoja ..
Ila baada ya Serikali kuwakalia kooni CSSC na BAKWATA wametema Ndoano tumebaki APHTA peke yetu..
Ila mwanzo tulikubaliana wote..
Soma hiyo barua..
Na weww hujiulizi kwanini hawakutoa Tamko Tarehe 27 na 28 watoe leo..

Na kama unakumbuka hata chama cha madaktari MAT nao waliwahi kupinga hicho kitita kwa barua na kemeo ila unashangaa kwanini leo nao wamesema wanakubaliana halafu nyuma walipimga kwa barua?
Wewe haikupi Red flag hiyo?
Siasa ni Mchezo mchafu snaa
 
You guys are too greedy

Naomba serikali ikaze kamba hasa kwenye kodi ya mapato, exemptions na bei zenu hadi tukae sawa
 
Nimetibiwa Aghakhani sana na nina NHIF mkuu
This mgomo itasaidia sana hospitali za umma kupata chance ya kushowcase improvements zote hasa wards service na general admissions

Kwanza hospitals kama aga khan waishakua haters wa NHIF

I predict this to be a huge blow kwa private hospitals and a boom for public and NHIF

Private we’re harvesting huge money for little services
 
Sasa mkuu waendelee kutoa huduma,hebu cheki mtu anatumia sh 100 kutoa huduma analipwa 40 baada ya miezi atakua na biashara tena?.
 
Unafahamu kwa Dar es Salaam asilimia 79 ya vituo vya kutolea huduma za afya ni vya binafsi? Kama watoa huduma wa vituo wakiitikia wito wa huu mgomo kikamilifu madhara yake yatakuwa makubwa sana

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
You guys are too greedy

Naomba serikali ikaze kamba hasa kwenye kodi ya mapato, exemptions na bei zenu hadi tukae sawa
Sasa mgomo umeibuka Sio tu wa NHIF Bali hakuna Mgonjwa atakayepokelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…