Wenye maabara za binadamu wanauza na dawa wakati leseni yao haiwaruhusu. Ni hatari kwa afya za watu

Wenye maabara za binadamu wanauza na dawa wakati leseni yao haiwaruhusu. Ni hatari kwa afya za watu

Mifumo yetu ya Afya mingi iko hoi. Ukienda India huwezi nunua dawa kama huna cheti chenye muhuri na sahihi ya daktari.

Njoo 'Bigwa' sasa kila mtu ni Prescriber halafu tunalalamika kuhusu 'Usugu wa dawa' (AMR).

Ilibidi kuwe na 'Ongoing supervision' kuhusu hivyo vituo na maduka ya dawa, angalau tutapona kidogo.
 
Shida si hizo maabara Shida ni sisi watanzania na umasikini uliopitiliza.
Mtu anakwambia hospitali gharama nenda pharmacy pima nunua dawa kwa Hela iliyopo kwa wakati huo.
Na hii kitu imeshaota mizizi mtu mpaka azidiwe ndio aone mlango wa hospital.
Serikali inabidi ipige kampeni watu waelewe umuhimu wa kuonana na daktari.
 
Umasikini Wa kushika na mikono miwili ni shida sana
 
Back
Top Bottom