Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Inaonekana humu wengi wazee wetu hawapo nasi duniani. Kwa heshima zao R.I.P our lovely ones. Baba angu alikua anaogopewa mtaa mzima japo hakua na shida na mtu hata marafiki walikua hawaji kwetu. Sema baba alipanda hewani halafu black wa ukweli jicho jekundu kwa sbb ya kilaji. So watu walijjua mtiti wake hatari kumbe walaa hata fimbo hajawahi kutuchapa. Ila sitasahau nilifeli hesabu nikiwa drs la tatu alinipa kofi moja niliona nyota nyota na kukaa chini bila kutoa sauti yoyote alijua kanimaliza akaondoka kimya kimya akarudi night akiwa njwiiii. Mie shavu limevimba mpk vidole vyake vimetokea toka siku ile nilikua kipenzi chake.
 
Kumbe we we wa kishua..mlikuwa na simu ya mezani wakatio huo,sisi kwetu tulikuwa na radio moja ya mkulima.
 
Pamoja na kujifanya umezimia bado akakumalizia na buti ha ha ha
 
dingi yangu alikuwa mkoloni sana, kipindi nakua nimechezea sana mikanda ila nashukuru ilinitoa ujinga na kunipa ujasiri kiasi kwamba mpaka leo sitetereki, dah r.i.p Dady
 
Leo ni miaka 57 imepita dingi kafariki kaniacha Nina miaka saba tu sasa shuruba na mateso niliyoyapata kwa walezi wangu siwezi kusimulia huwa nalia nikikumbuka binadamu wabaya sana ni wazuri tukiwa tumelala kwenye makaburi tu
Duuh walikutesaa sanaa mzee mpaka useme kauli nzito hivyo..!?? umeshindwaa hata kusamehee
 
Mi mshua wangu hakua mkatili kiivyo sema ile akikukamata bora ukimbie tu pia anaweza kukuungia sasa mwanae mim dish liliyumba kitambo nikawa namkimbiza mitaa yenye watu wengi kwa heshima aliyokua nayo basi alikua anavunga tu Mimi kichapo nmechezea kutoka kwa mama daaah ilifika stage najiuliza huyu n mama angu kweli daaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…