Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Duh wazee wa zamani kiboko... Mimi kwa bahat mbaya wazaz wangu walifariki ningali mdog mnoo RIP MAMA na BABA. Ila nimelelewa na mama yangu mdg jamani alikua anachapa kosa dogo tuh anakuchapa had majilan wanamuachanisha lkn wapi.

Nakumbuka Christmas ya 2007 cku iyo aliandaa maandaz sasa alipanga yatumike wiki nzima kama mjuavyo ckukuu chakula kinapikwa watu wanakula na kufurahiaa nakadhalika watu wote waliondoka nyumban nikabaki mimi pekeangu, akaja mama mmoja na mmewe wakaniomba chakula nikawapa wakala wakat wanataka kuondoka nikawachotea maandaz kdg kwenye mfuko wakaondoka. Jion mamdg alivolud aliona maandaz yamepungua akaniuliza nan kagawa maandaz nikajib n mimi mamdg alinichapa nusu kuniua
Sitasahau aisee kile kipondo kwa bahati mbaya bado hajabahatika kupata mtt labda ni vile hajui uchungu wa mwana maana dah stakaa nimsahau mamdg wangu.
Una jina zuri,,
Natamani kuja DM.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Siku moja mimi na dogo tulirudi saa mbili na nusu hivi na hiyo ilikuwa 1999, akatuuliza kama tumeswali swala ya ishaa, tukamwambia ndio. akatuuliza kaswalisha nani na amesoma sura gani?? kudaadeki akatubana. aiseee tulikula kichapo mpaka leo sikisahau, alitufunga kamba za katani na kututandika nyaya za umeme ajabu, kipindi hicho tunaishi Pemba kwenye nyumba za serikali na ni ghorofani sasa, kutoka mbio tulishindwa halafu alivyokuwa mkaksi, alimfungia bi mother mlango kwa nje kwanza ili asije kuamua ugovi. Siisahau iile siku, but we a re who we are because of him otherwise tungekuwa ganja mtu sasa hiv. Akili yangu kipindi kile ilikuwa inaniambia dingi anatuchukia but now I understand he was/is the best dad ever in this world. Thank you papaaa
Hahahahaa
 
Mmenikumbusha Bi. Mkubwa Mama Karim, aieee ukifanya kosa bora uende ukalale polisi.

Bibi mkubwa alikuwa ananipiga kinoma sio kwamba alinionea, hapana kuna makosa nilikuwa natafanya huku nikujua kabisa hili ni kosa.

Mzee wangu alikuwa hana noma, ili Mama Karim akikiwasha ndio balaa hata akina Donnie Yen, Jet Lee sijui akina John Cena wakasome.

Bi mkubwa alikuwa anapiga sio mchezo, yaani mpaka leo nimekuwa mtoto mwema.

R.I.P Mama
 
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji16][emoji16][emoji23][emoji2][emoji1][emoji1][emoji1][emoji3][emoji16]
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
[emoji16][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji28][emoji28][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
amefariki mwaka jana akiwa na miaka 79.. ila mpaka uzee wake hadi wajukuu walikuwa wanamuogopa.. anacheza nao ila akiamua anawatia viboko..

kuna mjukuu aliua kuku wa nyama... mama anafuga kuku sasa kuna siku wanawapa kuku dawa kuna mjukuu akaenda kumkamata kuku wa nyama bahati mbaya akamnyonga mzee alikuwepo jirani akaenda mtia fimbo mjukuu hadi mama yake mke wa kaka akataka kulia... bro akamwabia kama unataka kulia kalilie chumbani maana mzee akikuona unalia hapa anaweza anzisha ugomvi mzito na usikanyage tena hapa
[emoji16][emoji16][emoji2][emoji2][emoji2][emoji16]
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
Kama nakuona ulivyoaibika mbele ya mchumba..🤣
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
[emoji23][emoji23][emoji23] wazaramo waliipata fresh
 
Huyu jamaa hua nafikiria atakua sio mzazi wangu kweki maana He treat me like an orphan, regarding bado nipo kwenye age ya kutegemea msaada wake asilimia 80
Pole, na ndio maana umekuwa introvert, kifupi wewe si INTROVERT ila ni malezi yamefanya uwe hivyo. You need a serious psychological treatment!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] na ila nahisi madingi wengi miaka hiyo walikuwa wakali sio wa siku hizi mtoto anakusalimia kwenye whatsapp asubuh

Mimi viboko nilipata vya kutosha enzi hizo na ugomvi mkubwa ulikuwa kati yangu na sister make huyo kila siku tulikuwa tunazenguana na akirudi mzee ata kama mimi sina makosa nachezea za kufa mtu ....ukishika anafuta anaanza upya au ukinyanyuka anakwambia nenda na usirudiii [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]pole tu, ila nawe ulikua cha utundu
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Yaani mimi natamani hata leo nikutane na mzazi anafanya ujinga wa namna hii kwa mtoto, halafu watu watashangaa nitakavyonunua kesi hiyo, huyo mzazi atachoka na hatarudia tena. Upumbavu wa hali ya juu sana huu
AAAAH WAPI!! HUNA UWEZO HUO MMAKUWA WEWE.! MMAKUWA WEWE!!
 
Hongera yako! Sisi anazeeka ndo anazidi kuwa moto hatari! Yaani apite binti karibu yake kavaa vya ajabu au asimpe salamu! Atajutia kupita pale,huwa nammisi tu nikiwa mbali lakini usijiroge ukapiga cm kumsalimia badla ya salama yataanza mausia hayo na huko mwishoni ni kufokewa mpaka vocha inaisha!
Mkuu mzee wako ni kama wangu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] eti baada ya salamu yataanza mausia yatakayosababisha kufokewa mpaka vocha iishe[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
alikugeuza ndama .....
[emoji2][emoji1][emoji1][emoji28][emoji28][emoji28]yaani hivi nashangaa sana siye mdingi hakuaga hvyo hata robo kiukweli sijui ingekuaje na utundu wote wa kwenda mabwawa saba kucheza,kukimbilia midundikoo na kwenda umbali mrefu kucheza rede!!!
 
Back
Top Bottom