Majuzi kuna daktari nimempigia simu aisee alinikoromea kama mtoto kwamba kwa nini nampigia simu?? Nikiwa na shida naye niende kumuona ana kwa ana. Ikabidi niwe mpole tuu maana wahenga wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto. Last week jirani yangu mzee wa makamo naye yalimkuta, alikuwa na shida yake akapata ushauri akamuone DC, akaenda twice lakini akawa hamkuti. Basi secretary akampatia namba ili aongee naye aweke appointment. Basi bwana ile kupiga simu tuu ilivyopokelewa alikaripiwa vibaya sana kwamba nani kampa na.yake?? Kama ana shida aende ofisini na siyo kumpigia simu hovyo hovyo!! Mzee alisononeka mpaka huruma yaani.