Mkuu hiyo siyo ishu ya kijinga ,ikitokea na inatokeaga huyo mtu anaruhusiwa kuondoka na anapewa msaada.
Watu wanaongeaga ishu za kijinga we acha tu mfano mtu anamuadithia mwenzake jinsi jana alivyofanya uzinzi wengine wanaongea non issues kuna jamaa nilimtimua juzi kapigiwa simu akaongea zaidi ya dk 2 pamoja na kwamba nilikuwa karibu naye nasikia kila walichokuwa wanaongea ila sikuweza kuelewa kabisa .
Na nilivyo mtata nikamwambia anieleweshe kwenye hiyo simu aliyopigiwa walikuwa wanaongea nini akaamua kuacha kazi na kuongea .
Akaishia kunijibu mambo yetu tu bosi yaani kwa kifupi hata yeye alishindwa kueleza walikuwa wanaongea nini.
Ndugu, nakwambia kuna watu wengi wapo hivyo mwengine anaweza kukujibu kabisa bundle langu linakaribia kwisha ndio nalitumia kupigapiga nilimalizie. Embu just imagine mtu anaamua kusitisha kazi inayompatia fedha hadi amenunua bundle ,eti ili apige simu randomly tu (yeyote atakayekuwa hewani na kupokea simu anaanzishiwa tu story) ili atumie tu bundle lake liishe kwa kuongea tu vitu visivyoeleweka.
Ukijiona unapiga simu ili mradi tu umalizie bundle please jirekebishe hayo ni matumizi mabovu ya simu