Kwakweli sijui hili wazo la kulipa kodi ya nyumba iwe ya makazi, office ama biashara kwa muda wa kuanzia miezi 6 hadi mwaka ulitoka wapi, kwa makubaliano yapi kitaifa na kwa mujibu wa sheria zipi?
Sisi wajasiriamali wenye mitaji midogo ya kudunduliza mnataka tuishie kuwa ombaomba kwa kushindwa kujikwamua?. Sisi wapangaji wenu wenye kipato kidogo tunaumia sana kwakweli. Hebu tufikirieni jamani. Sawa nyumba ni zenu na ujenzi wa nyumba tunajua ni gharama. Ila mtufikirie na sisi wamiliki wa nyumba wa miaka ijayo. Maisha kusaidiana. Siyo poa hivyo mnavyotufanyia.
Yaani unakuta unaambiwa ulipe kodi ya mwaka let's say 250,000 x 12 = 3,000,000. Sasa kweli hii kodi kwa sisi wajasiriamali wadogo tutaweza vipi kulipa? Najua mtasema mnaogopa usumbufu, ila imefika wakati tubadili huu utaratibu wajameni.
Huko duniani nchi za Wenzetu walioendelea utaratibu wa kodi ni kila mwezi, na inalipika vizuri tu. Sasa sisi huu utaratibu wa mwaka unakujaje? Tubadilike.