Wenye Nyumba: “Nataka Mpangaji Asie na Mtoto Tu!” Huu ni Uchawi au Roho Mbaya tu?

Wenye Nyumba: “Nataka Mpangaji Asie na Mtoto Tu!” Huu ni Uchawi au Roho Mbaya tu?

Nina pangisha sehemu fulani, na ninakiri baadhi ya wapangaji wenye watoto sio wastaarabu kwa nyumba au wenzao.

kelele, uchafu, usumbufu wa kuingia milango ya wengine.

Mimi sibagui, as long as una timiza mkataba wako kwa wakti.
(3 wana watoto kwenye sehemu hiyo).

# watoto ni ishara ya upendo, utulivu na utu so wasibague kihivyo.
Mdogo wangu hapa kodi inakaribia kuisha, nitakuja kupanga kwako, tusumbuane sumbuane kulipana kodi kidogo
 
Kuepuka stress kama
Halafu mpangaji anaenda kutangaza kuwa una roho mbaya .

Hapo ukute uli piga rangi ya 150k ile deluxe uwii 😁😁
Kuepuka stress kama unajenga nyumba kwa ajili ya wapangaji fanya finishing ya bei nafuu. Rangi achana na silk/wash and wear palka rangi ya maji 20L 30,000 mtu akitoka hata akichafua unapaka ingine chap.
Usijenge nyumba ya kupangisha kama unavyojenga nyumba ya kuishi wewe. Wanaokaa hapo ni wapita njia tu they won't appreciate any quality. Unless ni zile apartment za Masaki au Oyserbay za $2000+ kwa mwezi.
 
Kuna matangazo kibao ya nyumba ambapo dalali anasema kabisa mwenye nyumba anataka mpangaji asie na mtoto/watoto.

Issue ni nini? Wivu au Roho mbaya?
Watoto wanachangia kuharibu Nyumbq
 
Watoto waharibifu sana nao.

Wakati nipo mdogo miaka ya 2006 nilichuna rangi ya toyota corolla ilikuwa nyeupe ya mwenye nyumba aliumia sana akafukuza wapangaji wotee.

Uzuri watoto tulikuwa wengi so hakunijua.
2006 yaani unapiga nike kwa kamasi? ***** kweli humu watoto ni wengi
 
Kuna matangazo kibao ya nyumba ambapo dalali anasema kabisa mwenye nyumba anataka mpangaji asie na mtoto/watoto.

Issue ni nini? Wivu au Roho mbaya?

Uharibifu wa watoto; Wazazi wengi hasa wa kizazi hiki hawajui kusimamia watoto, uchafu, kelele nk
Ukubwa wa nyumba inayokodishwa; sasa mtu anakodisha chumba kimoja self unataka muingie wangapi hapo?
Umekodisha vyumba viwili upo na mume na watoto wawili, na house girl, na mama mkwe, na mtoto wa ndugu nk nk kama mwenye nyumba anaishi humo hawezi kukubali...
 
Watoto waharibifu sana nao.

Wakati nipo mdogo miaka ya 2006 nilichuna rangi ya toyota corolla ilikuwa nyeupe ya mwenye nyumba aliumia sana akafukuza wapangaji wotee.

Uzuri watoto tulikuwa wengi so hakunijua.
Shrnzy kabsaa nakutafuta kumbe ni ww ?? Ww sio Alfan mtot wa mama Said??
 
Anajua fika ukiwa na familia kubwa hataweza kukuomba msosi wala hela ya kubet maana anajua fika nafsi yake itamsuta.
 
Akina juniya huwa wanakuwa watundu kesi haziishi, wanawapiga watoto wenzao, wazazi wao wanawatetea. Wakipigwa na wazazi waliochoka kupigigiwa watoto wao, nyumbani hapakaliki. Utasikia zaa wako ndio umpige wakati tayari nina mtoto.

Kuepusha yote hayo, akina juniya marufuki.
 
Acha uoga wa maisha mdogo wetu, unajenga ili iweje, hakuna elfu iliyoandikwa ya kununulia mfukobwa cement, kujenga uoga wa maisha.
Hata usipojenga, ukifa utajengewa nyumba ya milele tu.

😂🤣🤣
Bora niendelee kuzungusha raundi au sio mkuu. Kwanza ntajengaje njiani na duniani tunapita 😂
 
Gharama za kujenga huko kijijini kwao usukumani ni ndogo sana tofali anafyatua mwenyewe, mbao anapasua miti ya babu yake, kiwanja ni shamba alilopewa na babu yake mzee Budeba, fundi ni mtoto wa aunt yake na maji anachotea ziwa victoria
hapo gharama kubwa ni za kupambana na wachawi wasiopenda maendeleo.
 
Issue ni nini? Wivu au Roho mbaya?
Hawataki kesi watoto yale madude yao wanayowafunga mkunduni kupokea mavi wanayajaza kwenye matundu ya vyoo wanasababisha vyoo kujaa haraka, hii ilishatutokea mpangaji kaja na familia ya watoto watatu wote wadogo na wote wanawafunga ya mapampas magumu wakawa wanayatupa chooni choo kikajaa ndani ya muda mfupi sana kumbe kimejaa yake mapampas na hayayeyuki hata kwa petrol, hapo ni kuchomba choo kimya au kuzibua upya na kutoa mapampas yote.. hii ni gharama kubwa kwa mwenye nyumba.. hio ni moja tu ila kero zipo nyingi
 
Kwanini ume-generalize kwamba ni wivu au roho mbaya?. Mbona ni swali ambalo ungeweza kuuliza tu kistaarabu na kupewa majibu mazuri.

Mtu kajenga nyumba yake, kaweka masharti yake wewe kinachokuuma ni nini?

Mimi binafsi nina nyumba ya kupangisha mbele ina flemu za biashara. Sharti namba moja sitaki mpangaji atakaefanya biashara ya saluni ya kike. Nina sababu zangu na haki ya kuweka masharti kwenye nyumba yangu
Mkuu wanawake walikufanya nini aisee?
 
Back
Top Bottom