Wenye tabia za kichawi, acheni kuwanga

Wenye tabia za kichawi, acheni kuwanga

Omba mwanangu ushuhudie

Mimi niliwahi kumuona mmoja kitaani mabibo ila polisi waliwahi kumuokoa mbele ya raia.

Mwingine alikuwa ni baba mkubwa akayakanyaga Kwa ma'mkubwa alidhani mama mkubwa ni mchekea

Uchawi/ushirikina mwingine nilishuhudia Shule huko Iringa Migoli asee watoto wa day wasio lala mabwenini wa Ile shule wanaroga balah! Kisa tu kreti za soda,mbuzi na ng'ombe,

Nusu final ya chandimu tukapigwa goli tatu za chapuchapu lakini wataalamu wetu wakaleta chumvi na tangawizi tukategua tego tukashinda mechi kibabe

Final nyingine ya gozi wachezaji wakagoma kulala mabwenini Ili kujihadhari, wakajifanya wanabundi lakini madogo wakajua kabisa tumewakimbia wao (maana asubuhi walitupiga vijembe na mipasho ya hapa na pale) kesho yake kabla ya mechi wachezaji wakakubaliana wajipake mafuta ya nguruwe mmoja akogoma akesema yeye muislamu,dah! chuma ikipitia kulekule kwake tukafa kimoja Cha uchungu.

Kwenye handball na basketball atakufua dafu kabisaa tuliambulia volleyball tu ambayo walishutukizwa hivyo hawakufanya maudhaufha yao.

Nyingine nahisi kabisa ilikuwa kwenye Lukuvi Cup asee uchawi/ushirikina upo na mimi kunajambo lilinikuta pale migoli,yani pale ni pamoto
Mkuu hapo kwenye soda na nyama walikuwa wana roga ili msile?
Kwanini watu wa mikoani wachawi sana, Yani mtoto akilelewa mkoani ladhima ajue uchawi, tofauti na mtoto aliyezaliwa mjini mfano Dar.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mashemeji Zangu nyie ni watu waajabu tumewaacha angalau mumfariji Mama wa rafiki yangu ambae ni mkwe wangu,,na nyie mkasepa alafu Unakuja kutangaza mitandaoni,,Rose unashida gani lakini??umeshindwa kabisa kutustiri Kwa hili??Umetufedhehesha mnoo Mimi na rafiki yako!!
 
MAMA MCHAWI
****************

Habari za leo wapendwa....

Nina kisa kimoja kimetokea juzi tarehe 11,๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข

Iko hivi kuna rafiki yangu mmoja alipata mchumba,baada ya kuridhiana wakaanza maisha,kijana alienda kumtambulisha binti kwao ila binti hakuwahi kumtambulisha kijana kwao,basi wameishi kwa pamoja muda wa mwaka mmoja na miezi2 baadae binti ambaye ni rafiki yangu akaamua kwenda kumtambulisha mchumbaake kwao.

Basi shoga zangu,akatuandaa sisi marafiki tumsindikize na kijana nae akaandaa marafiki zake watakaomsindikiza..kwao binti.... Basi bana si tukajiandaa vizuri siku ya tarehe10 ndo tulienda kwao rafiki yangu. Namshukuru Mungu tulikaribishwa vizuri kwa ukarimu na ucheshi sana. Tulifurahia kuwafahamu wazazi wake rafiki yangu basi taratibu nyingine zikaendelea

Usiku ulipowadia tukaingia kupumzika mahali tulipoandaliwa wageni,basi sie tukalala

Wapendwa usiku huo kumbe mama mkwe ni mchawi katoka zake kwenda kuwanga,na huo mji aloenda kuwawangia kumbe haungiliki ovyo.....mama wa watu kaganda hadi asubuhi saa12.

Sisi tumelala mara ghafla kelele huko nje zikaanza huyo mchawii umezoea leo umeshindwa mmh,
Hizo kelele za kijijin ikabidi nasi tuamke na kwenda kushuhudia.

Vile tumetoka wageni wote nje. Tulipigwa na butwaa sana baada ya kumkuta mamaake rafiki yangu ndo anayepigwa na kavaa zake kaniki na vibuyu mkononi na mijitu kashikilia mkononi๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข๐Ÿ˜ข

Jamani omba isikukute ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญmama mkwe mbele ya mkwewe amevaa kaniki,binti alilia akisema mama laiti ningejua leo hii ningekuzuia usiende kuwanga binti wa watu akazirai mkwe kaamua kuondoka, na kamuacha binti kabisa hamtaki tena..binti alivyoamka nae kaondoka nyumbani ikabidi nasi turudi zetu nyumbani.

JAMAN WAMAMA WAMAMA MNAOWANGA JAMAN ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญNaumia sana najaribu kuvaa kiatu cha yule dada kinanibana jaman Inaumiza sana

Acheni kuwanga jaman wenye tabia kama hizi.


Ilitokea Jimbo gani la Marekani? Maana hakika kama ni mipaka ya Tanzania lazima ingekuwa habari kubwa, umezidisha Tangawizi ila ladha ujaharibu sana.
 
Stori hii nimeisoma kwa umakini nakiri ni UONGO MTUPU.
 
Back
Top Bottom