Wenye tatizo la usikuvu hafifu kama langu tukutane hapa kupeana faraja

Wenye tatizo la usikuvu hafifu kama langu tukutane hapa kupeana faraja

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2020
Posts
9,016
Reaction score
24,650
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 30 kwa sasa naishi iringa mjini, nimeondoka dar february baada ya kula sana msoto nikaamua ngoja niende sehemu ambayo hakuna anaenijua nipate utulivu wa akili, hapa iringa nimepewa hifadhi ya kulala tu na ndugu.

Twende kwenye main topic sasa, nina tatizo la kushindwa kusikia vizuri, nishazunguka kwenye hospitali nyingi sana tangu mwaka 2007 ambapo nilianza kuhisi tatizo. Mara ya mwisho nilsaidiwa pesa na jirani yetu wakati nipo Dar nikaenda hospitali ya CCBRT miaka kama minne hivi imepita baada ya vipimo waliniambia ngoma ya masikio haina tatizo, tatizo ni mishipa na hata nikifanya operation haitasaidia chochote.

Nikapewa dawa za kumeza asubuhi, mchana na jioni kwa miezi mitafu nikimaliza dozi nirudi hospital baada ya kumaliza dozi na kurudi hapakua na maendeleo yoyote, nikaambiwa suluhisho pekee ni kuvaa earing device ambazo ni gharama na zina risk kuongeza tatizo na kupelekea kuwa kiziwi kabisa basi nikaachana na mpango wa earing device na mambo ya kuwenda hospital maana nishaibgia gharama nyingi bila mafanikio, nikakubaliana na hali yangu, ndio mtihani wangu huo hapa duniani

Shule ya msingi nilimaliza nikiwa sawa kabisa nikafaulu kwa daraja A na kupangiwa kwenda Azania secondary. Wakati nikiwa form 1 mama angu alifariki nikawa yatima rasmi (maana baba alifariki nikiwa na mwaka mmoja tu hata kumbukumbu ya sura yake sina nimeoneshwa picha zake tu). Kwa kweli ugumu wa maisha niiyoishi kutokea kifo cha mama mimi mwenyewe ndo nayajua naomba nisiandike maana nitaitaji kujaza kitabu kizima.

Kuanzia kifo cha nikawa nasomeshwa kwa msaada wa baadhi ya ndugu na majirani, nilipofika around form 3 hivi ndo nikaanza kuhisi utofauti kwenye suala la kusikia napata shida kumsikia mtu akiongea kwa sauti ya chini, mtu mwenye kigugumizi, mtu akiongea akiwa mbali na kuongea na mtu kwa simu ndo simwelewi kabisa.

Kwa kweli shule ilikua chungu nikaanza utoro hata kujumuika na wanafunzi wenzangu ilikua shida darasani nikashuka sana form 4 sikufanya vzr. Nikasoma certificate, diploma na bachelor degree, ila najilaumu sana kupoteza huo muda kusoma chuo.

Ningeweza kurudisha muda nyuma ningesoma masomo ambayo yanaendana na hali yangu mfano uandishi maana nipo passionate sana na kuandika au ubunifu wa mavazi. Maana watu wananisifia sana najua kuchagua nguo nzuri kuna wengine huwa wananipa hela nikawanunulie au niwasindikize dukani kuwasaidia kuchagua au ningesomea ufundi.

Ila nikasoma masomo ya biashara ingawa ufaulu wangu wa chuo ni mzuri ila ni vigumu kupata ajira au kujiajiri. Maana mambo ya selling, marketing, uhasibu, customer care na ku-organize shughuli zote za biashara kwa kiasi kikubwa yanahitaji kuonana na watu kuwasiliana nao, presentation, seminars n.k.

Kwenye kutafuta kazi ni kisanga embu fikiria ugumu wa kupata ajira sasa ongeza na tatizo la kusikia vizuri ni balaa na nusu. Fursa nyingi sana zinanipita ni mwaka wa 6 sasa tangu nimalize chuo sijawahi kupata ajira yoyote, napigiwa simu za kuitwa kwenye interview siwezi kuongea na kuelewana na mtu kwenye simu, nikijaribu kujibu ujumbe kwa kuweka wazi nina changamoto ya kusikia waajiri wanaona nafanya ujanja janja tu wananijibu tu "asante" na mchakato unakua umeishia hapo.

Mbaya zaidi sina connection kwenye familia na ndugu wa karibu hakuna ambae anashikilia kitengo kizuri au mfanyabiashara mkubwa kidogo kusema anaweza akaniingiza kwenye mishe zake, nimepambana sana kutafuta mtu wa kunisaidia nimewafata watu mpaka sebureni kwao kuwaomba na kuwaambia nipo tayari kufanya kazi bure kama akihitaji kujiridhisha na uwezo wangu lakini nimeambulia patupu. Ni kama miaka 6 ya kusoma chuo kuanzia certicate nimepoteza muda na kuingia gharama tu, kwa sasa bado nipo mtaani sina mbele wala nyuma ingawa ufaulu wangu nilioupata chuo ni mzuri tu.

Ushauri wangu kwa wenye tatizo kama langu usikate tamaa, potezea dhiaka unazofanyiwa na watu, jikubali, pale unapokutana na mtu ambae haujuani nae jieleze kwamba una changamoto ya kusikia usione noma, chagua marafiki wachache ambao wanaelewa hali yako na pia jishughulishe au somea mambo ambayo yanaendana na changamoto inayokukabili yaani hauonani sana na watu na kufanya mazungumzo nao mfano uhandishi, ufundi, ubunifu n.k.

Lifestyle yangu kwa kiasi kikubwa ni ya upweke, sio mtu wa kuchangamana na watu kampani yangu kubwa ni kwenye vibanda umiza nikienda kuangalia mpira (story za ucheshi, majigambo na utani wa kishabiki vibandani angalao nasahau kwa muda matatizo yangu) hakuna kipindi chochote cha kwenye tv ninachokifatilia maana sisikii vizuri wanachoongea, nikiangalia tv ni mpira na movie zenye english subtitle tu, kuwasiliana na watu kwenye simu ni kwa sms tu, dharau, dhiaka, kupuuzwa, kuonekana mtu mwenye malingo kwa kutoitikia salamu au nikiongeleshwa alafu sijasikia ni changamoto ambazo nakutana nazo sana kwa ambao hawanijui na baadhi wananijua ila wanataka kunifanyia bullying tu mbele za watu.

Tusikate tamaa ndugu zangu kikubwa wote tupo hai
 

Attachments

  • 1662714369310.gif
    1662714369310.gif
    42 bytes · Views: 34
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 30 kwa sasa naishi iringa mjini, nimeondoka dar february baada ya kula sana msoto nikaamua ngoja niende sehemu ambayo hakuna anaenijua nipate utulivu wa akili, hapa iringa nimepewa hifadhi ya kulala tu na ndugu. Twende kwenye main topic sasa, nina tatizo la kushindwa kusikia vizuri, nishazunguka kwenye hospitali nyingi sana
Pole sana, nitafute inbox...
 
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 30 kwa sasa naishi iringa mjini, nimeondoka dar february baada ya kula sana msoto nikaamua ngoja niende sehemu ambayo hakuna anaenijua nipate utulivu wa akili, hapa iringa nimepewa hifadhi ya kulala tu na ndugu.
Pole sana mkuu

Ulipoenda kwa specialist wa ENT

Hawajakuambia suluhuhisho la tatizo lako,ufanye nini ili uweze kusikia

Ova
 
Pole sana mkuu
Ulipoenda kwa specialist wa ENT
Hawajakuambia suluhuhisho la tatizo lako,ufanye nini ili uweze kusikia

Ova
Ah yah,earing divice ni gharama sana
Sana,maana kuna mzee wangu mmja boss wangu pia aliendaga South africa aliwekwaga kwa $5000
Ila usikate tamaa ushauri wangu uzidi kuwasiliana na wadau wa ENT Labda inaweza tokea msaada wa kimatibabu
Kwa watu wenye matatizo kama wewe

Ova
 
Mimi ni kijana wa kiume umri miaka 30 kwa sasa naishi iringa mjini, nimeondoka dar february baada ya kula sana msoto nikaamua ngoja niende sehemu ambayo hakuna anaenijua nipate utulivu wa akili, hapa iringa nimepewa hifadhi ya kulala tu na ndugu.
Tupo pamoja mkuu, mimi ni kama wewe tu. Muhimu tusikate tamaa
 
Pole sana mkuu
Ulipoenda kwa specialist wa ENT
Hawajakuambia suluhuhisho la tatizo lako,ufanye nini ili uweze kusikia

Ova
Aliniambia hakuna tiba suluhisho ni kutumia earing device ambazo ni gharama na pia kuna risk ya kupelekea kuwa kiziwi kabisa
 
Back
Top Bottom