Wenye tatizo la usikuvu hafifu kama langu tukutane hapa kupeana faraja

Mimi nilikuwa na tatizo la kutosikia, na niliwah kupita hapa kweny ID nyingine kuomba msaada.
Nilizunguka hospitali zote bila kufanikiwa, jibu la madaktari ilikuwa hawaoni tatzo.

Kwa neema ya Mungu nili bahati kuja kuishi Marekani.
nikaenda hospitali kuona kama naweza kupona.

daktari wakuu aliniunganisha na watu waonahusiana na masikio.

Daktari wa sikio alinichukua vipimo na baada ya vipomo alisema ndani ya sikio kuna shimo ndo zinafanya husikie. na akaniambia sikio la kwanza nina 80% ya kupona na nyingine 70%. alinipa siku ya kufanya upasuaji sikio la kwanza. nilienda hospitali na alifanya yake. ukweli sikio lilirudi katika hali ya kusikia.

Nikapewa tarehe ya kurudia sikio la pili, now miaka miwili sijarudi kwa daktar. nimeridhika na hili moja linasikia vizuri maana sijawah kuitwa kiziwi kama zamani.

Daktari aliwahi kuniuliza, hao madaktari wa africa walikuwa wanakuambie?. nikamjibu walisema hawaoni tatizo. ila nikamwambia naisi ni ukosefu wa vifaa kama hvi ninavyoviona hapa.

Kutosikia sio kitu kizuri, kinapunguza hata hujasiri
 
pole sana Mweneyzi Mungu akuwekee wepesi ....umejaribu dawa za asili pia??
 
Nami nafanya ivyo namwambia kabisa mtu nina shida ya kusikia kuanzia mwanzo wa maongezi ingawa siwezi kufanya ivyo kama matangazo kwa kila mtu mwingine naishia kumsikiliza tu basi natabasamu, kutikisa kichwa au kuonesha tu sapoti yoyote ingawa sometimes nakuwa sijamwelewa alichosema especially kama tupo sehemu yenye makelele
 
Hyo ni tinittus mkuu usihangaike mama angu mdogo anayo since mdogo mpaka sana ana miaka 40 na kitu kashazoea kwa vile mwanamke ila nae kuongea pia kapoteza uwezo sio kwamba hajui ila anamua tu kuwa kama bubu ila anashikia sometime anaishi kawaida tu ...usijipe shida mpaka watu hwaoni wanaishi huenda one day unaweza kurudi.

Ili tatizo Linaweza kutokea katika hali flani za kushtua ubongo pia,..Linaweza sbabishwa na hata homa kali haswa malaria ,hata vile vidonge vya quinine pia zinahusika kingine saikolojia mawazo sana kichwani kupelekea kuathiri ubongo.

Ila achana na hawa watu coz asilimia ya watu wengi weny tatizo hilo ni vichwa la unabisha fuatilia yaani darasani wako vizuri so Kuna myth kwamba wanarogwa achana nazo .
 
Safi sana
 
Naomba mawasiliano au jina la iyo clinic mkuu.. who knows labda siku moja nami nitapata msaada niweze kufika uko
 
Unaongea mambo mengi yanayonigusa moja kwa moja, mimi pia primary nilikua vizuri class nishawahi kupiga interview pale feza nikaperfom vizuri ila bi mkubwa akakataa kusoma pale maana braza angu niliefanya nae interview yeye alifeli wakamkataa na bi mkubwa anataka wote tusome shule moja nakumbuka yule mwalimu mkuu enzi izo alikua mzungu mtu wa ujerumani akampa bi mkubwa mpaka ofa ya punguzo la ada nisome pale feza ya mikocheni ila bi mkubwa akachomoa msimamo wake tusome shule moja na bro., primary nimesoma miaka mitano tu maana madarasa mengine nilikua nalukishwa sababu ya uwezo mkubwa class, nakumbuka mtihani wa taifa s.t.d 7 somo hesabu nilipata 49/50 siku naenda kutembelea shule niliyomaliza std 7 mwalimu mkuu akawa ananitania kama ananichapa kwanini niliiacha iyo moja iliyobaki. kuhusu story za kulogwa nishawahi kuambiwa uenda watu wamenichezea kualibu future yangu ila ni vile siamini kabisa hayo mambo ya ulozi
 
Pole sana,kutana na ma specialists wa ENT,ungekua Dodoma,ungeenda pale Benjamin Mkapa,ukutane Dr.Mkinga au Bukano,wakufanyie intensive examination ya masikio,you never know,unaweza ukapona.
Pole Sana,once again.
 
Pole sana kaka,
Hiyo shida inanisumbua pia,
Najikuta confidence inapungua saana, na upweke kwa wingi, lakini nashukuru Mungu amenipa akili sana, performance yangu ni nzuri. Ila masikio bado ni changamoto kwangu nimeenda kwa wataalam MNH, wameniambia hakuna dawa, wakasema ninunue hearing devices,
Sijazinunua napambana na hali yangu.
Usife moyo haupo peke yako.
 
Pole kijana na mimi nina tatizo kama lako ila mimi sikio langu moja halisikii vizuri

Nilianza primary kutosikia vizuri ila nilikomaa na kitabu nikafaulu shule ya serikali nakufaulu mtihani wa seminari
Nikapiga kitabu nikaenda A level shule nzuri ya serikali nikaenda chuo

Nikaingia mtaani nikaa miaka mitatu natafuta ajira naomba ajira hata siitwi kwenye interview private wala utumishi

Baadaye nikazidisha maombi sana nakuombewa nakaomba ajira tena utumishi nikaitwa ya kwanza NHC Duke dar nikafanya written nikadunda


Nikaitwa ingine tena ya pili ya utumishi nikafanya nikafaulu sasa hivi nipo Dodoma wizarani hapa napiga kazi naishi watu vizuri tu wala hawanibagui

Jaribu utumishi Mkuu Ajira unaweza kupata
Hakikisha unakuwa mtu wamaombi sana sana Mkuu

Kikubwa usikate tamaa hata majaribu yawe makubwa

Mwenyezi Mungu akubariki sana sana Mkuu
 
Hii ni kweli kaka,
Akili ipo active sana,
Nashukuru Mungu nilifanikiwa kupata shule ya vipaji maalum. Ijapokuwa nipo na hili tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…