Currently nina mikataba ya aina hii na watu kadhaa. Bodaboda nilizonazo ni boxer. Hesabu kila siku ni Tshs. 10,000/- kwa mwaka mzima (siku 365, sawa na Tshs 3,650,000/-, boda hiyo niliinunua Tshs. 2,600,000/-). Sasa toka hapo mtakubaliana kwamba mpeane hesabu kila baada ya wiki (70,000), au kila baada ya siku 10 (100,000/-). Usiweke siku zaidi ya 10 maana na wao kutunza fedha ni changamoto.
Ila mnasainishana serikali ya mtaa. Binafsi huko serikali ya mtaa, nalipa 20,000/- kila mkataba ninaoingia na mtu.
NB. Ukitaka sample ya mkataba wa bodaboda njoo inbox, nitakupa ukiwa kwenye word format.