Mimi naona Biashara ya mkataba ni kichaa
Biashara pasua kichwa hiyo ni sawa na kujaza maji kwenye tenga.
Ipo hivi pikipiki aina ya boxer inauzwa mil 2.8, hesabu ya siku unaletewa elfu 10 na mkataba kwa kawaida ni miezi 13..ukiwa unaletewa kila siku elfu 10 kwa mwezi utakuwa umeingiza laki 3,laki 3*13=3900000
3900000-2800000=1100000
Faida kwa mwaka mzima unapata mil 1.1
1100000÷13=84615...
Unatoa mil 2.8 mfukoni halafu kwa mwezi faida unaingiza elfu 84615 kama sio utahaira ni nini? Na hapo ukiigawanya kwa siku ni kama unaingiza 2800.
Sasa kwa mtaji milioni 3 kasoro sio sahihi kuingiza 3000 kwa siku. Huku mama muuza mihogo anaingiza zaidi ya hiyo kwa mtaji chini ya elfu 30.
Na hapo hapo mwisho wa mwaka piki piki inakuwa sio yako.. mtaji wote umekwisha
NB: Hapo bado haujapewa taarifa ya kuibiwa pikipiki, service ikiwa kubwa ni juu ya boss