Wenye uzoefu na biashara ya mkataba kwa bodaboda na bajaji naomba mnielimishe

Sasa na waendesha mabus wangekuwa wanafanya hivi sijui ingekuaje baada ya muda chombo inakuwa ya kwake 😄 hili suala halijawahi kuniingia akili kabisa
 
Mwamba umezoea mabiashara makubwa au siyo..!! imejini una boda boda 20..!!

Anyway, ni njia ya kutunza fedha.
Kuhusu kuibiwa, hakunaga risk free business.
Kuna watu wanawalipa mahouse girlTshs 50,000/- kwa mwezi pamoja na kuwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala.

UMESHAWAHI KUPIGA HESABU ZA KUMILIKI TAXI? BINAFSI HUKO NAKUONA NDO MICHOSO HASWA
 
Hahahahaha,maokoto hayo mkuu,elf 3 daily unaidharau tena yenye uhakika?

Ok wengine tunasaidia vijana na pia watoto wasisumbue hela ya shule na chips
 
Bodaboda 20 😄 aisee lazima kichwa kipate moto
 
Hahahahaha,maokoto hayo mkuu,elf 3 daily unaidharau tena yenye uhakika?

Ok wengine tunasaidia vijana na pia watoto wasisumbue hela ya shule na chips

Kuingiza Elfu 3 kwa siku sio mbaya..

Ila ninachopinga ni kuingiza elfu 3 kwa siku kwa kutumia mtaji milioni 3 kasoro. Plus Risk kubwa.. na hapo hapo mwisho wa mwaka mali inakuwa sio yako tena

Ingekuwa non risk business kama Nyumba ya kupangisha.. hata ukiingiza 1000 kwa siku sio mbaya.. maana nyumba inabaki yako milele na ni non risk
 
Nilinunua kinglion mwaka 2019 December 2350000 nikapeana kwa mkataba wa miezi 12 huwezi amini kufikia mwezi wa tatu kijana alizingua sio kidogo. nikapiga hesabu nikaona mi ndo naingia cha kike nikampora pikpiki nikauza kwa 1.7..hii biashara sio rahisi kiivo
 
Viongozi wawe na mapenzi kwa raia wao..Tunaomba atokee kiongozi mwenye imani Afute hii biashara ya bodaboda na bajaji..ni janga la taifa..zipigwe marufuku kwenye miji mikui na iwe marufuku kuagiza pikipiki au bajaji na Toyo madhara ni makubwa kushinda faida zake..ni Kinyaa kwenye miji yetu fujo inayoletwa na aina hii ya transport. Pawed na statistics kwa siku ni ajali ngapi za pikipiki na bajaji ukijumlisha na kuwakwaruzia watu magariyao na kukimbia. Wanach tunawaomba wenye Mamlaka pikipiki zipigwe marufuku.
 
Wewe ni mwamba...wengine wanamiliki biashara kwa ego tu ya kumiliki biashara...ila in long run wanakuwa upande wa loss....at least anunue Bajaj Kama anauwezo na kipande kwa siku ni 20000..
 

nani amekuambia nyumba haina risk?

Likipita tetemeko?kama je ulijenga kimakosa mradi wa serkali unapita na hawalipi fidia?ikiwaka moto na huna bima?
 
Kwa hesabu zangu na uzoefu wangu hadi sasa bora hesabu japo madereva n wasumbufu kinoma hawakosagi sababu ya kutokukupa hesabu,unaweza pata fedha mara 3/4 kwa wiki hizo siku zngne n janjajanja labda upate dereva mwenye anajielewa…Oil uwe unabadili mwenyew hawa wahuni oil inakaa had mwezi

Kimsingi mkataba kama haijakaa vizur(haina maslah mapana kwa boss)kwan baada ya miez 12 chombo sio yako,na pikipiki mpya ukikomaa na derava vzr ndan ya mwaka unakua umerudsha fedha yako kwa hesabu ya 7000/8000 na pikipiki mpya inaweza kuishi had miaka 5 ikitunzwa vizur ko utakua na miaka 4 ya kuokota hata kama ikiwa 100 kwa mwez sio mbaya inakua n passive income

Swala la risk hilo lipo wazi kama n ajali/kuibiwa itaibiwa tu hata iwe n ya mkataba…kikubwa unapoingia kwenye game yeyote uandae moyo wako lolote zaid sana dua mambo yawe nafuu



Binafsi nafanya za hesabu,Japo kusema ukwel hakuna pesa rahisi madereva n pasua kichwa kama unahasira za haraka unaweza tandika makofi
 
Mku Mkuu, mbona faida ni ndogo Sana.

Yaani 3650,000-2,600,000 = 1,050,000 ndo faida Tena ya mwaka mzima?

Mbona ni Kama Biashara kichaa? Maana mwaka wote huo Kuna kuumwa na matatizo ya hapa na pale. Kwa hela hiyo ukiumwa Tu mara moja si inaishia kujiuguza.

Me nadhani faida itaonekana Kama Una Bodaboda kuanzia 10 hivi sio mbaya.
 
Umeongea mambo mazito,naomba ufafanuzi zaidi!Umeongea kitu hiki "bora hesabu" sijakuelewa!!Mimi bado mgeni kabisa kwenye hili suala!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…