Wenye uzoefu naombeni ushauri, kuhusu baba kaoa kule na mama kaolewa huko

Wenye uzoefu naombeni ushauri, kuhusu baba kaoa kule na mama kaolewa huko

Record Man

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2023
Posts
525
Reaction score
876
Wakuu Habari za weekend.
Hivi unakuta Baba na mama walizaa ila kila mmoja akaenda na ndoa yake.

Sasa kijana anataka kuoa, na yeye hajaishi kwa Mama yake wala kwa Baba yake. Kaishi na shangazi yake.
Sasa anajiuliza kuhusu situation itakuwaje kuhusu mama yake kuudhulia kwenye shughuli kama kupeleka mali. Na kwenda kumtambulisha mchumba kwa mama yake kwani, kwa mama yake hajawahi kwenda walikuwa wanakutana tuu mara chache sana.
Ishu kwa mzee atasema ataenda tuu japo hana mazoea na mke wa mzee wake.

Ishu ndo hio anawasiwasi kuwa kwa mama yake anaweza kuto kwenda yani hapa, wasiwasi anaona anaweza kuuzulia tuu labda siku ya harusi na sio shughuli zingine kama kumtambulisha mchumba, kwenda kwenye kisherehe cha kupeleka mahali, na send-off.

Wakuu mnamsaidiaje huyu.
 
Hao waalikwe tu kama machizi wengine tulomaliza nao 4m4, kuitikia au kuvunga ni juu yao.

Mzazi ni zaidi ya kutupia bao au kulea mimba,
Msiwalazimishe wazazi walioamua kuwakataa.
 
Yaan ingekuwa n mm shangazi yangu ningempa kipaumbele asilimia 100 ktk Kila ktu Cha hyo ndoa ..hao wazazi wangejua umuhmu wako wangekulea Kwa vile hawakujua umuhmu wako wakajiangalia tamaa zao za miili kuliko ww ,bac shangazi ndio baba ndio mama ishi hapo panatoshaa..
 
Si lazima amtambulishe mchumba nyumbani kwa mama yake wala baba yake. Awaite waje kwa shangazi wawepo wote watatu baba, mama na shangazi afanye utambulisho. Kwenye kila hatua kama mahari na harusi nyumbani kwao ni kwa shangazi. Sio anakurupuka kwenda kwingine ambapo hajui.
 
Back
Top Bottom