GE2025 Wenyeji wa Mikoa ya Kaskazini Wana Haki ya Kuongoza Majimbo Yao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Unahubiri ukabila na ukanda ndugu mleta mada. Kila mtanzania ana haki ya kuishi na kugombea ubunge mahala popote kwenye Jimbo lolote.
sawa ila awe anakubarika, angalau ameishi kitambo. jeuri hii itaisha kukiwa na haki ya wananchi kuchagua wamtakae. Nrne muhimu
 
Kweli bro Arusha yote Ina watu hawana uwezo??? Just how aisee. Yani tuweze kujenga miundombinu ya kupokea watalii vizuri tushindwe ubunge?? Duh
Arusha inamilikiwa na Wachagga!. Wachagga ndio wenye biashara zote kubwa kubwa, mahoteli, guests na maduka!. Akigombea Mmasai na Mchagga, Mchagga ndie anachaguliwa!.
P
 
Majimbo ya uchaguzi katika mikoa ya Kaskazini yanapaswa kuongozwa na watu waliowazaliwa au waliokulia katika maeneo hayo. Itakuwa ni dharau kwa wananchi wa mikoa hii iwapo watu wa nje – wasiokuwa na mizizi wala historia ya eneo – watateuliwa au kupitishwa kugombea nafasi za uongozi kwa kigezo cha kisiasa tu.

Watanzania bado wanakumbuka jinsi mikoa ya Kaskazini ilivyohujumiwa na kudhalilishwa wakati wa awamu ya tano ya uongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Hayati Rais John Magufuli. Mikoa hiyo, pamoja na kuonyesha mchango mkubwa wa kisiasa na kiuchumi, iliambiwa isubiri zamu ya mikoa mingine – hasa ya Kanda ya Ziwa – ambayo viongozi wake walionekana kupewa nafasi nyingi serikalini.

Leo hii, hali kama hiyo inataka kurudiwa kwa sura mpya. Mfano halisi ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda – ambaye anatoka nje ya mkoa huo – kuonyesha nia ya kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini. Hili linazua maswali mengi kwa wananchi wa Arusha: Je, ni kweli hakuna wenyeji wenye uwezo, maono na sifa za kuwa wabunge? Kwa nini tusione huu ni mwendelezo wa siasa za kulazimisha utawala kutoka nje ya mikoa ya Kaskazini?

Kama kweli CCM inasikia sauti ya wananchi, basi ni lazima izingatie hisia na historia ya watu wa mikoa ya Kaskazini. Tunahitaji viongozi wanaotufahamu, walioko karibu na changamoto zetu, na wanaoguswa na maisha ya kila siku ya wananchi wa maeneo haya.

Kwa muda mrefu, wananchi wa Arusha na mikoa jirani wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za haki, uhuru na maendeleo. Haitakuwa busara kuwavunjia heshima kwa kuwaletea viongozi wa "kupachikwa" wasiogusa mizizi ya jamii hizi.

Tukumbuke Historia – Tujenge Mwelekeo Mpya

Ni muhimu tujifunze kutoka kwenye makosa ya awamu zilizopita. Tukumbuke namna mikoa ya Kanda ya Kaskazini ilivyotengwa na kusahaulika katika masuala ya kitaifa, licha ya mchango wake mkubwa. Sasa ni wakati wa wananchi kusema: inatosha! Tunataka viongozi wetu watoke miongoni mwetu, watu wanaojua shida zetu na wanaoweka maslahi ya wananchi mbele.

Mungu ibariki Arusha. Mungu ambariki Tundu Lissu – kiongozi aliyesimama kidete kutetea haki bila woga. Ni wakati wetu sasa, watu wa Kaskazini, kusema kwa sauti moja: "Uongozi wa majimbo yetu ni wetu!"
Msukuma Paul Makonda lazima awatawale hapo Arusha.
 
Arusha inamilikiwa na Wachagga!. Wachagga ndio wenye biashara zote kubwa kubwa, mahoteli, guests na maduka!. Akigombea Mmasai na Mchagga, Mchagga ndie anachaguliwa!.
P
Arusha haimilikiwi na kabila lolote ni sehemu ya Jamhuri.
 
Bro kiroho safi Sasa hivi naweza kwenda Sengerema nikagombea kisa tu nimekua mkuu wa wilaya kwa miezi 10? Au nikaenda Uyole nikagombea kisa tu nimekua DAS kwa mwaka mmoja? Hebu niambie kule usukumani ni mbunge yupi ambae sio msukuma? Hajui kisukuma na amegombea? Sio ukabila, watu wa mahali fulani wanakua na changamoto zao unique ambazo ni watu wa maeneo Yale tu ndo wanazielewa. Ndo maana hakuna mtanganyika anayependa kugombea Pemba nafasi ya ubunge wa Kimuungano. Why? Kwa sababu hajui matatizo ya wapemba ni nini na nini.
Hata marekani Wana kigezo Cha ukaazi wa Mahalia kwa miaka kadhaa Ili ugombee.
1. Mh. Kiwia (mchanga) alikuwa Mbunge wa Ilemela Mwanza 2010-2015
2. Mh. Mh Wenje (mjaruo wa rolya/Kenya) alikuwa Mbunge wa Nyamagana Mwanza 2010-2015
3. Jimbo la Kwimba usukumani Mbunge wake siyo Msukuma, ni Mhindi
4. Nzega ambapo population yake ni Nyamwezi/Sukuma mbunge wake siyo katika kabila hizo
5. Rostan Aziz pale Igunga hakuwa Msukuma/Mnyamwezi
 
Kwa I mleta bandiko MRema LIVYOCHAGULIWA MBUNGE TEMEKE WANANCHI WALIKOSEA? MBONA WENYE TEMEKE HAWAKULALAMIKA.
ACHA HIZO , MAMBO TUPENDANE TU WOTE WATANZANIA
 
Watu wakieleza ukweli mnasema ukabila!

ukabila unatokea wapi wakati ni ukweli.

Awamu ya 5 ya Msukuma mwenzio ambao ulikuwa nanukabila kwa kubagua mokoa ya Kaskazini mbona ukukemea?????
We are being watched. The gvt has a secret system,a machine to spy on you in every hour of every day. I designed the machine to detect acts of terror but it ceased everthing, violence and crimes that involve ordinary people, the gvt consider these people irrelevant, we dont. Hunted by authorities, we work in secret, you will never find us, but victims or perpetuator, if your number is up, we will find you.
 
Majimbo ya uchaguzi katika mikoa ya Kaskazini yanapaswa kuongozwa na watu waliowazaliwa au waliokulia katika maeneo hayo. Itakuwa ni dharau kwa wananchi wa mikoa hii iwapo watu wa nje – wasiokuwa na mizizi wala historia ya eneo – watateuliwa au kupitishwa kugombea nafasi za uongozi kwa kigezo cha kisiasa tu.

Watanzania bado wanakumbuka jinsi mikoa ya Kaskazini ilivyohujumiwa na kudhalilishwa wakati wa awamu ya tano ya uongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Hayati Rais John Magufuli. Mikoa hiyo, pamoja na kuonyesha mchango mkubwa wa kisiasa na kiuchumi, iliambiwa isubiri zamu ya mikoa mingine – hasa ya Kanda ya Ziwa – ambayo viongozi wake walionekana kupewa nafasi nyingi serikalini.

Leo hii, hali kama hiyo inataka kurudiwa kwa sura mpya. Mfano halisi ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda – ambaye anatoka nje ya mkoa huo – kuonyesha nia ya kugombea ubunge Jimbo la Arusha Mjini. Hili linazua maswali mengi kwa wananchi wa Arusha: Je, ni kweli hakuna wenyeji wenye uwezo, maono na sifa za kuwa wabunge? Kwa nini tusione huu ni mwendelezo wa siasa za kulazimisha utawala kutoka nje ya mikoa ya Kaskazini?

Kama kweli CCM inasikia sauti ya wananchi, basi ni lazima izingatie hisia na historia ya watu wa mikoa ya Kaskazini. Tunahitaji viongozi wanaotufahamu, walioko karibu na changamoto zetu, na wanaoguswa na maisha ya kila siku ya wananchi wa maeneo haya.

Kwa muda mrefu, wananchi wa Arusha na mikoa jirani wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za haki, uhuru na maendeleo. Haitakuwa busara kuwavunjia heshima kwa kuwaletea viongozi wa "kupachikwa" wasiogusa mizizi ya jamii hizi.

Tukumbuke Historia – Tujenge Mwelekeo Mpya

Ni muhimu tujifunze kutoka kwenye makosa ya awamu zilizopita. Tukumbuke namna mikoa ya Kanda ya Kaskazini ilivyotengwa na kusahaulika katika masuala ya kitaifa, licha ya mchango wake mkubwa. Sasa ni wakati wa wananchi kusema: inatosha! Tunataka viongozi wetu watoke miongoni mwetu, watu wanaojua shida zetu na wanaoweka maslahi ya wananchi mbele.

Mungu ibariki Arusha. Mungu ambariki Tundu Lissu – kiongozi aliyesimama kidete kutetea haki bila woga. Ni wakati wetu sasa, watu wa Kaskazini, kusema kwa sauti moja: "Uongozi wa majimbo yetu ni wetu!"
Sifa za uongozi ni uraia, si ukabila.

Tanzania tushakuwa na wabunge mpaka wazungu hapo Kinondoni kina Derek Bryceson na Wahindi Morogoro kina Shamim Khan.

Kama wananchi hawamtaki mtu kwa sababu hawamjui na hawajui, wamkatae kwa sababu hawamjui na hawajui, si kwa sababu si mzawa wa eneo fulani.

Kwa sababu inawezekana mzawa akawa haelewi shida za wananchi na mgeni akaja na kuelewa shida za wananchi.
 
Bro kiroho safi Sasa hivi naweza kwenda Sengerema nikagombea kisa tu nimekua mkuu wa wilaya kwa miezi 10? Au nikaenda Uyole nikagombea kisa tu nimekua DAS kwa mwaka mmoja? Hebu niambie kule usukumani ni mbunge yupi ambae sio msukuma? Hajui kisukuma na amegombea? Sio ukabila, watu wa mahali fulani wanakua na changamoto zao unique ambazo ni watu wa maeneo Yale tu ndo wanazielewa. Ndo maana hakuna mtanganyika anayependa kugombea Pemba nafasi ya ubunge wa Kimuungano. Why? Kwa sababu hajui matatizo ya wapemba ni nini na nini.
Hata marekani Wana kigezo Cha ukaazi wa Mahalia kwa miaka kadhaa Ili ugombee.
Hujui kwamba Dr. Hussein Ally Mwinyi (Rais wa sasa Zanzibar) alikuwa Mbunge wa jimbo la Mkuranga lililoko mkoa wa Pwani Tanzania Bara?
 
Back
Top Bottom