Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Wenzangu mnaombaje mpaka maombi yenu yanajibiwa?

Utapeli ndio unaanza hivi hivi.

Una mwaminisha mtu kwamba ana mikosi, mizimu na mibalaa, Ili uanze kumhubiria habari uchwara za uponyaji kutaka hela zake na mali zake kama sadaka.

Mleta mada Bunchari kaa rada, Acha kupokea ushauri wa namna hii wa kwenda kwa manabii uchwara mwishowe uje upigwe hela zako.

Kaa chini, jitathmini na utambue kwamba..👇

You are your own provider and you are your own solutions in your life.
😄😄😄 ni ushauri tu. Akiamua afanye atafanya asipotaka asifanye pia.
 
Na mojawapo ya umaskini mbaya wa Akili ni huu wakusubiri na kumuomba huyo Mungu akusaidie shida zako,

ilhali kiuhalisia ni wewe mwenyewe ndio unaumiza kichwa, namna gani utoke kwenye hizo shida.

Halafu bado unakaa kuamini kauli uchwara za Mungu hakawii wala hachelewi.

We unapenda kulalamika Sana upo too negative
 
usiombe bila kutoa sadaka kwa nature...sasa chukua asali pure lita moja....tafuta mti mkubwa kaimwage hiyo asali yote kisha rudi nyumbani kafanye maombi kama unavyoombaga...harafu uje ulete mrejesho...!
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Usijali utajibiwa endelea kuomba, kuwa na uvumilivu wakati unasubiria huku ukikifanyia kazi kwa kuchukuwa hatua kile unachokiomba hakika amini nakuambia utajibiwa.

Neno la Mungu ni kweli na amina
 
Katika mambo ambayo.huwa naona watu wanakosea ni kukaa na kuomba kisha wakategemea walichoomba watakipata exactly kama kilivyo.

Je, umeshawahi jiuliza huenda hiko ulichonacho huenda ndiyo fungu lako ulilopangiwa?

Pamoja na kuomba, mimi nimelelewa ktk falsafa ya kuridhika na kuishi kulingana na kile nikipatacho. Yani tumekuzwa ktk falsafa ya ku-maximize kile tukijaliwacho. Hivyo, hata nipate kidogo vipi huwa nina imani na Mungu wangu kwamba hiko ndicho alichonipangia.

Then, kesho mapambano yanaendelea. Hii imenisaidia kuepukana na uncesessary stresses na kutolose focus na maisha.

Pia inakusaidia kutokuwa na tamaa.
 
Vitu vya kumuomba Mungu.

1.Uzima
2.Afya
3.Baraka.

Ukishakua na hivi. Kua mtu wa kufanya kazi na shukrani tu kwa Mungu wako. The rest unatakiwa ufanye kazi uvipate.

1.Ukitaka mchumba, socialize na watu utapata copy yako.
2.Ukitaka kazi, Ongea na watu watakupa connection
3.Ukutaka gari, Fanya biashara au tafuta kazi usave, utanunua.

Nje ya hapo, utasubiri sana majibu ya maombi na hutapata
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Hicho unachokiomba au kikiombea unakifanyia kazi? Unaomba hela wakati huko ndani umelala? Pambania hicho unachokiombea na acha mambo ya kutoa hela kizembe eti sadaka utafanywa kama "kiboko wa wachawi". Timing ya maombi ni muhimu! Wengi ukinga maji wakati mvua imeishakata! Mfano unaombea siku yako ya kesho asubuhi saa 12 wakati wachawi wanaloga saa 9 usiku!!! Utatoboa kweli? Siku hizi wachawi wanaloga hata mchana kweupe ni kwa vile huna macho ya rohoni!
Isaya 62: 6-12: Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA, msiwe na kimya;
 
Habari ndugu zangu

Naomba kuelekezwa namna ya kuomba maombi yangu yakajibiwa,kama kusali nasali sana,kufunga nafunga sana,kutoa sadaka natoa ila maisha yangu yameandamwa na magonjwa ya ajabu,kutofanikiwa na kukosa kazi

Sasa wapi ninakosea au mimi sijui kuomba ndugu zangu,kwani ninyi mnafanyaje?

Asanteni
Endelea kuomba..Mungu atakujibu wakati atakao, ila hata asipojibu utakavyo ataendelea kubaki Mungu tu
 
Je umeokoka kweli kweli,maana bila kuokoka hauna uhusiano na Mungu lakini pia mshirikishe roho mtakatifu maana yeye ndie anaejua kutuombea jinsi ipasavyo.
 
Sasa unawezaje kusoma b kama p?

Umeshawahi kupimwa na wataalam kama una dyslexia?
Mkuu,
Sina tatizo Kama Hilo nilikua natembea jua la dar es salaam na heka heka za kariakoo sikua kwenye utulivu kabisa.
Wakati mwingine sito rudia kusoma na kuandika kwa haraka haraka Kama ivyoo.
 
Je umeokoka kweli kweli,maana bila kuokoka hauna uhusiano na Mungu lakini pia mshirikishe roho mtakatifu maana yeye ndie anaejua kutuombea jinsi ipasavyo.
SIKU IZI WENGI NI WALOKOLE MAMBOLEO (NEO_WALOKOLE)
😊
 
Back
Top Bottom