Wenzetu mliotumia pesa za kujikimu (BOOM) la chuo mkatoboa mmefanyaje huenda wadogo zenu wakasaidika

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Kwangu mimi niliweza ku-save lakini sio kiasi kikubwa sana hadi namaliza chuo ni kama naanza upya

Sasa nimekutana na mdada katika story mbili tatu ananiambia pesa ya Boom ndio iliyomfikisha hapo, kiukweli na biashara anayofanya na zile pesa za kila baada ya miezi miwili ni mbingu na ardhi, sikuweza kumdadisi sana ataona namuonea wivu au kijicho

Kwenu wenzetu mliotoboa na pesa za BOOM mlifanyaje wakuu
 
Hivi mpaka umri huo bado unaamini mwanamke hawezi kupata pesa kwa njia tofauti tofauti zaidi ya hiyo. Kwanza mwanamke anaonewa huruma sehemu nyingi na kwenye mambo mengi, simu yake moja tu anaweza kuokota laki ila wewe mwanaume simu 10 unaweza usiokote hata 10. hivyo acha kushindana na wanawake. Hata kumpigia mahesabu.
 
Kabisa mtu anatembea na Mgodi mda wowote anapata Madini.
 
Tusiwape pressure wadogo zetu bn, mimi nlikuwa napata hiyo hela ilikua haitoshi nkawa nasaidiwa tena kutoka home. Yaani 560,000/=, 524,000/=, 540,000/= saiv wamefika 600,000/= hiyo hela utumie kupata msosi, nauli, bando, matumizi binafsi, laptop, nguo & Mahitaji ya geto/hostel kwa miezi miwili na ibaki ufanyie biashara?
 
Ukiweza kutumia Boom la chuo kufanya biashara au uwekezaji wowote ule, basi wewe utafanya vizuri sana kwenye eneo la biashara hapo baadaye.

Mimi enzi zangu kila nilipopata hilo boom (2500 prr day) niliwekeza zaidi kwenye kupanda daladala za Mwenge, Tandika na Kariakoo kwenda kununua simu, feni, tv, deki, sub woofer, nguo za mitumba, nk.

Baada ya hapo nilikuwa nakomunika mpaka basi.
 
Hivi mpaka umri huo bado unaamini mwanamke hawezi kupata pesa kwa njia tofauti tofauti zaidi ya hiyo. Kwanza mwanamke anaonewa huruma sehemu nyingi na kwenye mambo mengi, simu yake moja tu anaweza kuokota laki ila wewe mwanaume simu 10 unaweza usiokote hata 10. hivyo acha kushindana na wanawake. Hata kumpigia mahesabu.
Nami niliwaza hivyo pia lkn tukiiweka ki-positive vp haiwezekan?
 
Kwangu mimi niliweza ku-save lakini sio kiasi kikubwa sana hadi namaliza chuo ni kama naanza upya

Sasa nimekutana na mdada katika story mbili tatu ananiambia pesa ya Boom ndio iliyomfikisha hapo, kiukweli na biashara anayofanya na zile pesa za kila baada ya miezi miwili ni mbingu na ardhi, sikuweza kumdadisi sana ataona namuonea wivu au kijicho

Kwenu wenzetu mliotoboa na pesa za BOOM mlifanyaje wakuu
Nimekutana na wengine kwa hiyo boom wanasaidia kusomesha na wadogo zao huko vijijini. Ila wapo ambao kwa matumizi yao boom haitoshi kabisa. Its all about priorities na mipangilio.
 
Tusiwape pressure wadogo zetu bn, mimi nlikuwa napata hiyo hela ilikua haitoshi nkawa nasaidiwa tena kutoka home. Yaani 560,000/=, 524,000/=, 540,000/= saiv wamefika 600,000/= hiyo hela utumie kupata msosi, nauli, bando, matumizi binafsi, laptop, nguo & Mahitaji ya geto/hostel kwa miezi miwili na ibaki ufanyie biashara?
Sasa hapo si ni wastani wa laki 3 kwa mwezi mkuu kama wanapata laki 6 kila baada ya miezi miwili..ni mshahara kabisa huo kabla kima cha chini hakijapandishwa mpaka laki 5 ile mwaka jana.
 
Nimekutana na wengine kwa hiyo boom wanasaidia kusomesha na wadogo zao huko vijijini. Ila wapo ambao kwa matumizi yao boom haitoshi kabisa. Its all about priorities na mipangilio.
Hili ndio tatizo la wengi kutoweza kusave hata buku maana mzazi akishasikia unapewa hela za matumizi yeye kwake ni sawa unalipwa kwahiyo majukumu kama yote
 
Ukiweza kutumia Boom la chuo kufanya biashara au uwekezaji wowote ule, basi wewe utafanya vizuri sana kwenye eneo la biashara hapo baadaye.

Mimi enzi zangu kila nilipopata hilo boom (2500 prr day) niliwekeza zaidi kwenye kupanda daladala za Mwenge, Tandika na Kariakoo kwenda kununua simu, feni, tv, deki, sub woofer, nguo za mitumba, nk.

Baada ya hapo nilikuwa nakomunika mpaka basi.
Nahisi huyu mdada nae kafanya kama wewe
 
Kwangu mimi niliweza ku-save lakini sio kiasi kikubwa sana hadi namaliza chuo ni kama naanza upya

Sasa nimekutana na mdada katika story mbili tatu ananiambia pesa ya Boom ndio iliyomfikisha hapo, kiukweli na biashara anayofanya na zile pesa za kila baada ya miezi miwili ni mbingu na ardhi, sikuweza kumdadisi sana ataona namuonea wivu au kijicho

Kwenu wenzetu mliotoboa na pesa za BOOM mlifanyaje wakuu
Kwanza usome chuo ambacho kipo karibu na home, kama mkoani uwe unakaa kwa mtu bila kulipa kodi,

Pili boom lako lisihusike na kulipa ada, yaani uwe full funded na heslb

Tatu, usiendekeze kula cafe, uwe na ratiba ngumu ya msosi, na msosi wa usiku ni lazima uwe unakula home.

Usiwe na majukumu kama kumzalisha mtoto wa mtu, kiufupi punguza mapenzi chuoni, hata kama unamchumba, asiwe sehemu ya kukuumiza sana kukutobia.

Commitment muhimu, inahitaji, uvumulivu, ujasiri na maamuzi magumu.

Acha kukopesha, acha kusafiri mara kwa mara, sahau kupenda technolojia, kama simu za bei, laptop, n.k

Kama kuna biashara umeielewa fanya, ila sio zile za kuuza peni, dagaa na karanga chuo utajisumbua. Me nilikuwa type writer wa assignment za watu kwa siku hukosi 10k na kuendelea.

Piga msuri usidisco ili uendelee kumake pesa zikija.

Hivi ndivyo nilivyofanya na kujikuta namaliza chuo na mtaji japo sio nyingi ila inatosha kuanza maisha.
 
Hili ndio tatizo la wengi kutoweza kusave hata buku maana mzazi akishasikia unapewa hela za matumizi yeye kwake ni sawa unalipwa kwahiyo majukumu kama yote
Wanafunzi wengine wanatoka familia duni sana lakini wana akili ya kujitambua. Nilikutana na Binti hapo UDSM miaka hiyo 1990s, katika boom anakwenda kununua nguo za mitumba ili kuuza kwa wanafunzi wenzie ili kusomesha wadogo zake waliopo kijijini.
Nahisi huyu mdada nae kafanya kama wewe
Ni akili za kutambua majukumu na wajibu kwa wanafamilia.
 
Back
Top Bottom