MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Jinsi ya kuutokomeza umaskini ni kuhakikisha wanafamilia wameenda shule na kupata elimu ya kutosha. Watu wakiwa na elimu wanaweza pambana angalau wakaweza kujimudu hata kama sio kuwa matajiri. Mzazi ahakikishe kwa namna yoyote ile mtoto apende shule. Binafsi nimesoma shule za serikali mwanzo mwisho. Mzee wangu alikuwa ananijaza sana matumaini.. yaani alikuwa ananijaza upepo nikienda shule hata bila pocket money najiona niko sawa na kuamini baba atatuma. Ile spirit niliyojazwa na mzee wangu ikanifanya niwashike wadogo mkono kwenye ishu za shule. Kwa sasa familia nzima imefika chuo kikuu na angalau kila mtu anajishughulisha.
Mbinu yangu ya elimu inaweza isifanye kazi pia kama wanafamilia hawana nidhamu. Familia iliyokosa maadili hata wawe na akili za darasani wanaweza bado wakaendelea kuwa maskini. Wanafamilia wanatakiwa kuheshimiana na kuishi kama timu. Sio mmoja ajione bora zaidi.