Kuwepo kwa masikini na matajiri ndio kuna ifanya Dunia kua hivi ilivyo,ndio maana Mungu anasisitiza kua unapobarikiwa kipato usisahau kuwasaidia masikini coz alijua masikini watakuwepo,hatuwezi kua wote matajiri au wote masikini,
Kuutokomeza umasikini ni mwenye nacho kumsaidia asiye nacho kama Mungu alivyo sisitiza,ukiwa na uwezo na ukakutana na masikini,toa hicho kidogo ulichonacho umsaidie nae apate mahitaji japo kidogo,kila mtu akiwa na moyo wa kusaidia basi tutapunguza sana hili tatizo la kua na watu ambao hawamudu hata kununua chakula,
Utajiri ni mtihani na umasikini ni mtihani pia,maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya juu sana,Binadamu wote ni ndugu na hii Dunia tunapita tu,ukibarikiwa usisahau kuwasaidia wenye uhitaji,maisha ni fumbo.