Hili nalo pia ni tatizo katika familia nyingi,
Unakuta mtu mmoja kafanikiwa kwenye maisha katika familia yao,na anaona ufahari sana pale ndugu wanapokuja kumlilia shida nae huwasaidia,na anatamani maisha yawe hivyo hivyo,yaani anatamani miaka yote wenzake wawe chini yake tu ili waendelee kumlilia shida,hujiona ni kama mfalme fulani hivi,sasa mtu kama huyu akianguka ghafla kiuchumi,familia/Ukoo wote wanapata tabu,
Unapobarikiwa,jaribu kuwainua na wengine hasa watu wako wa karibu,ili kama mmoja wenu ataanguka kiuchumi basi wawepo na wengine ambao watamuinua na mwenzao tena,hili linafanyika sana kwa baadhi ya jamii za Waarabu na Wahindi,
Kitu muhimu ndani ya Koo ni lazima kuwe na upendo,kuheshimiana,kuaminiana....na hizi good discipline and attitude haziji ghafla au kimiujiza,hujengwa katika malezi tangu utotoni.