Wenzetu mmewezaje kuvunja 'cycle' ya umasikini wa ukoo/familia?

Wenzetu mmewezaje kuvunja 'cycle' ya umasikini wa ukoo/familia?

  • Kuna familia na Koo zipo hakuna aliyemaliza form 4 wote elimu iliwashinda.
  • Kuna familia na Koo mmoja tu kafanikiwa kufika chuo na kumaliza ila kazi hana.
  • Kuna familia na Koo ndio unakuta masikini wa kukufuru, mabinti wote wamezalia nyumbani, hakuna aliyeolewa na vijana nao wote wameleta wake zao nyumbani. Hakuna hata mwenye afadhali ya maisha.
Nyumba ukiingia tu inanuka njaa. Wewe ndio umebahatika kupata vijihela, lakini hela yenyewe haikai unaenda unajikuta unarudi pale pale; ile circle ya umasikini haivunjiki.

Wenzangu mnafanyaje mliozaliwa kwenye umasikini?

View attachment 2493306
Picha kutoka maktaba
Tatizo mnaona kwa kuangalia tako,ukitaka kuoa angalua kichwa chwa huyo mke na familia yao,
Pili usikae mkoa uliozaliwa kutoboa ngumu,sababu ya mizinga
 
Kuna kitu kinaitwa WAHULE (sijui kama ni lugha inayoweza kueleweka kwa wote), hii kitu ikitembelea ukoo wenu bila jitihada binafsi, kila anaezaliwa ataingia kwenye mfumo wa umaskini.

Yani hata upewe Mil 100 leo asubuhi, kwa namna yoyote ile baada ya mwaka au miaka utakuwa ni kapuku tena, bila kujali una elimu au huna.

Umasikini ni swala pana sana ni la kigenetic na kiroho zaidi, ukoo wowote unataoweza kuzifungua hizo patterns basi umasikini na nuksi hupita mbali.

Sio umasikini tu, mnaweza kwenda sehemu mkiwa wawili ila kabla hata hamjafanya lolote mwenzako atachangamkiwa kuliko wewe, kama vile ni mwenyeji pale, wakati kiuhalisia wote ni wageni. Vivyo hivyo kwa fursa mbalimbali.
Embu fafanua zaid hichi ulichoandika,natamani kufahamu zaid na jinsi gan ya kutoa hizo patterns
 
[emoji1787]
Hahahah nimezungumzia swala la Ridhiwani kurithi falsafa za baba yake. Hio ni genetically mtu anatoka nazo kwa mzazi.

Ila kuhusu mtonyo ni swala la miundombinu tu.
Karithi tabia za baba ake abazo zitampa uongozi kama baba ake, ni mtu wakutabasamu wakati wote huruma hizo zote karithi.
 
Mkuu hiyo ni roho mbaya siku utapopata matatizo ndo utajua umuhimu wa extended family.
Acha ujinga wewe, ndugu maskini hawana maana na hata ukipata tatizo fukara atakusaidia vipi?
Kama unajielewa na tayari umeamua kuuaga umaskini, piga chini ndugu mafukara. Ukiamua kuwasaidia wadaidie ukiwa tayari ni tajiri.
 
Tatizo sio umasikini, tatizo kuu sisi waafrika moja akichomoka wengine waliobaki huazisha vita kumpinga na kuhakikisha anafeli, husda na roho mbaya nimuendeleza wao wengine mpaka wanaenda kwa mganga wa kienyeji wakuroge.

Ukipata shida wanafurahia, omba sana Mungu usije kuzaliwa na ndugu wajinga wenye umasikini wa akili....... tatizo sio umasikini wa kipato huo ni suala la muda unaisha ukiwa na ndugu waaminifu, wenye upendo, watiifu wenye busara na heshima.
"tatizo sio umasikini wa kipato huo ni suala la muda unaisha ukiwa na ndugu waaminifu, wenye upendo, watiifu wenye busara na heshima."

[emoji115]
Hakika watu wengi hawajui kuwa hakuna umasikini mbaya kama wa akili na fikra.
 
Ishi Maisha yako wengine wapo katika Gundu mfano Mimi Jamaa yangu mmoja amekuwa na wanawake wachafu mpaka leo kapewa gundu Hana future kila kitu kwako kizito

Umasikini ndugu yake ni Uzinzi so usisaidie Mtu tofauti na wazazi tu
Hii ni kama kweli hivi. Umasikini ndugu yake ni uzinzi
 
Kuna familia kaka na dogo wote wanapiga day, tena wamefundishwa na baba yao mdogo!

Ambao hamjaoa epuka kuoa au kuolewa na familia kapuku kama yetu.

Masikini hatuna faida.
Mkuu umeongea maneno machache na kwa uchungu mno. Umefikiria nini kuiita familia yako kapuku?
 
Kunakuwa na matatizo ya kiroho yani, kwa ambao wazazi hawakuwa na mawazo na dunia kuwa kuna watu wa hovyo wanaweza kuharibu future ya familia ndio hivyo tena mnaweza kuporomoka kutoka A class family to F Class...

Laiti mzee angejua mapema kuwa dunia haiko jinsi anavyofikiri maybe familia isingeparanganyika tukarudi kwa ground!

Watoto ndio tuna suffer kwa kufidia uzembe ule.
Kitu ambacho watu wengi hatutaki kukubali ni kwamba, dunia ni uwanja wa vita na yale mengi ya giza ambayo utandawazi unatushauri tuyapuuze ndo yenye kuamua hatima ya wengi.

Kufanikiwa sio tu shule na kufika chuo kikuu, sio mentality wala mipango na wala sio kuchapa kazi saaaana kama wengi tunavyotaja kuaminishana hapa. Wapo watu wana hivyo vitu na bado hawawezi kutoboa leo wala kesho.
 
Kitu ambacho watu wengi hatutaki kukubali ni kwamba, dunia ni uwanja wa vita na yale mengi ya giza ambayo utandawazi unatushauri tuyapuuze ndo yenye kuamua hatima ya wengi.

Kufanikiwa sio tu shule na kufika chuo kikuu, sio mentality wala mipango na wala sio kuchapa kazi saaaana kama wengi tunavyotaja kuaminishana hapa. Wapo watu wana hivyo vitu na bado hawawezi kutoboa leo wala kesho.
Amini kwamba
 
Baba yangu ni wa Kwanza kwao na alifika form 6.... Akapata kazi wakati wa MWINYI

Mimi wa Kwanza kwa Baba yangu nikafika chuo....Sijapata kazi mpk sasa.


Ila MIZIMU ya ukoo imeniambia nikitaka kutoboa nisifanye kazi wala kuajiriwa wamenipa UGANGA wao watanipa UTAJIRI kupitia watu.


KOO zetu zina Siri kubwa sana
Nimeshuhudia marafiki zangu wawili waliopitia kwenye chain kama yako, mmoja alileta ujuaji wa kitandawazi kuyakataa hayo mambo mwisho wa yote alikota makopo, wengine wakadai kavuta bangi. Alichukuliwa akaenda kutubiwa kienyeji na mpaka leo ni mganga😅.

Sema huu huwa ni uonevu bwana, inakuwaje nilazimike kuwa mganga ilhali sitaki??
 
Shida kubwa ni "mentality" ndo sababu kubwa ya umasikini.

Kama hujui unachofanya hata ukipewa mtaji utazingua tu.

Ila jamii nyingi wanabebana, mmoja akifanikiwa anawabeba wenzake.
Jamii nyingi za waliofanikiwa,..Wayahudi, Wahindi, Wachaga, Wakinga, Waha..etc
 
Mkuu ungesema "poor mentality" sio "poverty mentality" that's poor English tofautisha naun and adjective....poor ni neno povert ni kitendo cha kua poor.
Mkuu endelea kutoa darasa la matumizi ya Lugha,..atakae kumind achana nae.
 
Hakuna uhusiano kati ya umasikini na Genetics or Race,umasikini unasababishwa na man made,kuanzia life style,bad discipline and attitude,kutokujali muda,kutokua na mipango,kutokujiwekea akiba,kuvamia kazi au biashara ambayo hujaifanyia research,kuiga kwa kuona fulani kafanikiwa kwa kufanya jambo fulani huku ukiwa hujui amepitia njia zipi mpaka kufika hapo alipo,kukata tamaa na mengineyo,

Life is one Big road with lots of sign,So when you riding through the ruts,don't complicate your mind,flee from hate,mischief and jealousy,put ur vision to reality.
Kweli kabisa naunga mkono
 
Jua kwamba matatizo mengi ya kifamilia ni ya kijenetic mengine ni ya kimazingira na mengine ni ya kimalezi na mengine ni ya kiroho. Yote haya yaweza kutengeneza mzunguko usio na mwisho (vicious cycle) ambapo ni ngumu kutoka.

Chunguza vizuri kujua nini chanzo cha kushindwa kwa familia au ukoo wenu, halafu chukua hatua stahiki.
Naunga mkono hoja hii.
KIJENETIC inamaana kuna baadhi ya tabia ni za kurithi. Ni vema mtu akajitambua na kujitathmini, kuna watu wamerithi tabia za uvivu kutoka kwa babu na Bibi zao huko kizazi cha nyuma.

Lazima mtu mzima ufike mahali ujitathmini na ukigundua kuna tabia umerithi Fanya kila namna kuachana nayo.

KIMAZINGIRA inamaana watu wanaokuzunguka na vitu vinavyokuzunguka. Baadhi ya watu toka wanazaliwa na kukulia kwenye jamii ya watu ambao ni walevi na hawathamini elimu.....Kijana huyu akishakuwa pia anarithi tabia za wale aliowakuta na mwendelezo unaendelea hivyo.
Katika hili cha kufanya ni kuhama mazingira. Wapo wengi waliofanikiwa kimaisha kwasababu sehemu alipopangiwa kwenda kusoma alijikuta amebadilisha mazingira na kuiga utamaduni wa kistaarabu unaochochea kufanikiwa zaidi.

Lakini wapo waliokulia mazingira mazuri sanaa ila wakashindwa kujitambua wakaishia kuwa walevi na watumiaji wa madawa ya kulevya na kuharibikiwa maisha pia.

MALEZI ( UPBRINGING) hii inamaana kipindi ambacho Mtoto hajui jema na baya ....anakuwa chindi ya uangalizi wa walezi/ wazazi. Baadhi ya wazazi wanashindwa kabisa kusimamia MALEZI ya watoto wao. Mtoto inafikia kipindi anaamua kufanya analotaka maana hakuna anayemfatilia kuhakikisha anakwenda katika njiabiliyonyooka.

Kwenye hili pia wapo waliolelewa na wazazi wazembe kabisa au wakaoshe walezi kabisa lakini wakakuwa na kufanikiwa maishani. Point inabaki palepale KUJITAMBUA.

KIROHO hapa ndio mzizi wa matatizo ulipo. Sisi tunaoamini mambo ya Rohoni tunafahamu ya kwamba zipo nguvu za giza ( mizimu, majini na uchawi) vinavyoweza kurudisha nyuma maisha ya mtu au jamii Fulani.
Nguvu hizi za giza huwaandama hasa watu wenye nyota ya mafanikio makubwa mbeleni.
Lakini baadhi ya watu huwapata kwasababu ya tabia ya kuendekeza mabaya kama umalaya, kukosa Imani dhabiti etc.
Kwa anayejitambua lazima atatafuta ufumbuzi wa KIROHO .

Kwa wanaoamini katika nguvu ya Maombi na Maombezi nawashurikisha Maombezi haya ambayo yatakuwa ufunguo wa WA vifungo vya KIROHO

 
  • Kuna familia na Koo zipo hakuna aliyemaliza form 4 wote elimu iliwashinda.
  • Kuna familia na Koo mmoja tu kafanikiwa kufika chuo na kumaliza ila kazi hana.
  • Kuna familia na Koo ndio unakuta masikini wa kukufuru, mabinti wote wamezalia nyumbani, hakuna aliyeolewa na vijana nao wote wameleta wake zao nyumbani. Hakuna hata mwenye afadhali ya maisha.
Nyumba ukiingia tu inanuka njaa. Wewe ndio umebahatika kupata vijihela, lakini hela yenyewe haikai unaenda unajikuta unarudi pale pale; ile circle ya umasikini haivunjiki.

Wenzangu mnafanyaje mliozaliwa kwenye umasikini?

View attachment 2493306
Picha kutoka maktaba
Kuivunja vicious circle of poverty ya familia au ukoo ni mtihani mgumu sana.

Labda vizazi vya tatu ndio vinaaweza walau kupata nafuu.
 
Back
Top Bottom