Jua kwamba matatizo mengi ya kifamilia ni ya kijenetic mengine ni ya kimazingira na mengine ni ya kimalezi na mengine ni ya kiroho. Yote haya yaweza kutengeneza mzunguko usio na mwisho (vicious cycle) ambapo ni ngumu kutoka.
Chunguza vizuri kujua nini chanzo cha kushindwa kwa familia au ukoo wenu, halafu chukua hatua stahiki.
Naunga mkono hoja hii.
KIJENETIC inamaana kuna baadhi ya tabia ni za kurithi. Ni vema mtu akajitambua na kujitathmini, kuna watu wamerithi tabia za uvivu kutoka kwa babu na Bibi zao huko kizazi cha nyuma.
Lazima mtu mzima ufike mahali ujitathmini na ukigundua kuna tabia umerithi Fanya kila namna kuachana nayo.
KIMAZINGIRA inamaana watu wanaokuzunguka na vitu vinavyokuzunguka. Baadhi ya watu toka wanazaliwa na kukulia kwenye jamii ya watu ambao ni walevi na hawathamini elimu.....Kijana huyu akishakuwa pia anarithi tabia za wale aliowakuta na mwendelezo unaendelea hivyo.
Katika hili cha kufanya ni kuhama mazingira. Wapo wengi waliofanikiwa kimaisha kwasababu sehemu alipopangiwa kwenda kusoma alijikuta amebadilisha mazingira na kuiga utamaduni wa kistaarabu unaochochea kufanikiwa zaidi.
Lakini wapo waliokulia mazingira mazuri sanaa ila wakashindwa kujitambua wakaishia kuwa walevi na watumiaji wa madawa ya kulevya na kuharibikiwa maisha pia.
MALEZI ( UPBRINGING) hii inamaana kipindi ambacho Mtoto hajui jema na baya ....anakuwa chindi ya uangalizi wa walezi/ wazazi. Baadhi ya wazazi wanashindwa kabisa kusimamia MALEZI ya watoto wao. Mtoto inafikia kipindi anaamua kufanya analotaka maana hakuna anayemfatilia kuhakikisha anakwenda katika njiabiliyonyooka.
Kwenye hili pia wapo waliolelewa na wazazi wazembe kabisa au wakaoshe walezi kabisa lakini wakakuwa na kufanikiwa maishani. Point inabaki palepale KUJITAMBUA.
KIROHO hapa ndio mzizi wa matatizo ulipo. Sisi tunaoamini mambo ya Rohoni tunafahamu ya kwamba zipo nguvu za giza ( mizimu, majini na uchawi) vinavyoweza kurudisha nyuma maisha ya mtu au jamii Fulani.
Nguvu hizi za giza huwaandama hasa watu wenye nyota ya mafanikio makubwa mbeleni.
Lakini baadhi ya watu huwapata kwasababu ya tabia ya kuendekeza mabaya kama umalaya, kukosa Imani dhabiti etc.
Kwa anayejitambua lazima atatafuta ufumbuzi wa KIROHO .
Kwa wanaoamini katika nguvu ya Maombi na Maombezi nawashurikisha Maombezi haya ambayo yatakuwa ufunguo wa WA vifungo vya KIROHO