Umeongea machache lakini mazito. Ikikupendeza elezea kwa undani zaidi.
Matatizo ya kijenetic: jua kwamba kila trait au tabia za msingi walizonazo viumbe hai zinarithiwa kizazi hadi kizazi. Kuna familia zimerithi tatizo fulani labda ni uwezo mdogo wa kujifunza na kutenda. Kinasaba hiki chaweza kutiririka kwenye vizazi vingi vijavyo na kuufanya ukoo mzima kuonekana usio na watu wenye mafanikio.
Matatizo ya kimazingira: Mnaona jinsi mazingira tunayotoka yanavyoathiri uwezo wa mtu. Mtu wa mjini utamwona tu ha mtu wa shamba hali kadhalika. Wewe umezaliwa kwenye familia baba, mama, na kila mtu ni wajasiriamali, uwezekano wa wewe kufaulu kwenye mkondo huo ni mkubwa kuliko yule aliyezaliwa kwenye familia wanayokaa chini ya mnazi wakisubiri nazi zianguke.
Kimalezi: Kama familia au ukoo wenu hauna hulka nzuri na hawasomeshi watoto wao usitegemee wakatoka wasomi huko.
Kiroho: Hapa ni pagumu zaidi na mara nyingi hutokana na makosa ya kijenetic, kimazingira na kimalezi. Nguvu za giza hupenyeza kupitia madhaifu ya watu kama ulevi, uvivu, wivu, woga, ugonjwa, ujinga, n.k. na kuyafanya matatizo hayo kuwa makubwa na complicated zaidi.
Laana nazo zipo kama zilivyo baraka. Kuna kulogwa na kutumikishwa katika ulimwengu wa kiroho katika ngazi mbalimbali za usukule. Kila mtu aweza kutumikishwa kwa viwango tofauti lakini kufikia ngazi ya usukule ni kiwango kikubwa cha utumishi katika ulimwengu wa giza. Laana za ukoo zaweza kuvunjwa kwa kuacha mazoea mabaya na pia kwa kubadilisha fikra na maneno wanayokiri wanafamilia kila siku. Matambiko yanafunga watu katika maagano kwa vizazi na vizazi. Kuvunja laana za ukoo sio kazi ndogo inahitaji mabadiliko makubwa ya kiroho na imani kubwa katika nguvu iliyo kubwa kuliko ile ya mizimu ya kwenu. Nguvu hiyo ni ya Mungu Muumba na wala siyo ya viumbe vyake. Nguvu na mamlaka hayo yamejidhihirisha kati Yesu Kristo ambaye tunajua mizimu na shetani mwenyewe humwogopa. Jufungamanishe na Yesu kwa kila namna uepuke utumwa wa mizimu, majini na shetani.