Wenzetu mmewezaje kuvunja 'cycle' ya umasikini wa ukoo/familia?

Wenzetu mmewezaje kuvunja 'cycle' ya umasikini wa ukoo/familia?

Ni jambo zito sana ila linahitaji mkakati mkubwa kwa familia katika kulitokomeza

Mama na baba wapya wajue wanapambania nini kwa ajili ya kizazi chao na si bora kuzaa kwa nia ya kuijaza dunia bila ya kupanga namna gani huyo mtoto mnataka awe, hivyo basi mkifeli ktk hilo la kujua na kumuandaa mtoto au watoto mtakao waleta wawe katika viwango vipi vya maisha basi ni wazi itakuwa ngumu kwa watoto kufikia hatua ya kuukwepa ufukara

Kikwazo ni hizo ndoa au mahusiano ya baba na mama ya kuweza kulea kwa pamoja huku mkijenga hiyo misingi kwa watoto wenu ndoa hazipo na kama zipo nyingi zinakuwa mfu au za mitikisiko mikubwa ikipelekea kila mzazi kuvutia kwake.

Kupambana na ufukara ni vita kuubwa inayohitaji imani kuu kwa muumba wako, ari kuu, nidhamu, mikakati, maelewano na uvumilivu usio kifani
 
Jua kwamba matatizo mengi ya kifamilia ni ya kijenetic mengine ni ya kimazingira na mengine ni ya kimalezi na mengine ni ya kiroho. Yote haya yaweza kutengeneza mzunguko usio na mwisho (vicious cycle) ambapo ni ngumu kutoka.

Chunguza vizuri kujua nini chanzo cha kushindwa kwa familia au ukoo wenu, halafu chukua hatua stahiki.
Nakubaliana na wewe 100%
Mkuu mimi na kupinga umasikini ni man made haunauhusiano wowote na uumbaji au kiroho, hayo yote nivisingizio vya wale walio shinda kupambanua udhaifu wao na kuishia kumsingizia Mungu.......wa kuristo wa kimißsionary ndo walio anzisha hiyo theory ya kusema umasikini unatoka kwa Mungu, na masikini amebarikiwa kwake ataenda binguni, hizo kauli zilitumiwa na hao watu ili exploit mali za waafrica na kutengeneza utii kwa wafasi wao masikini, we can fight and eradicate poverty.
Mkuu sijui kama unaamini kwenye maswala ya kiroho ila alichokiandika mkuu kina uhalisia kwa kiwango kikubwa sana, nadhani tutoke kwenye ishu ya umasikini, twende kwenye changamoto ya baadhi ya familia mabinti kutokuolewa(sio kwamba wanazalia nyumbani). Kwenye hili utagundua kua kuna namna kuna kitu hakipo sawa, nini kifanyike? Ni muhimu kujua chanzo ili kuweza kuishinda changamoto hiyo.
 
d4b62842-ab7e-442f-b7b3-81c928bec3f9.jpg
 
Mkuu mimi na kupinga umasikini ni man made haunauhusiano wowote na uumbaji au kiroho, hayo yote nivisingizio vya wale walio shinda kupambanua udhaifu wao na kuishia kumsingizia Mungu.......wa kuristo wa kimißsionary ndo walio anzisha hiyo theory ya kusema umasikini unatoka kwa Mungu, na masikini amebarikiwa kwake ataenda binguni, hizo kauli zilitumiwa na hao watu ili exploit mali za waafrica na kutengeneza utii kwa wafasi wao masikini, we can fight and eradicate poverty.
Mkuu kama mtoto anaweza kurithi kipaji cha mzazi inashindikanaje kurithi umaskini? Haishangazi mtoto wa footballer kuwa footballer, mtoto wa Rais kuwa Rais, mtoto wa mfanyabiashara kuwa mfanyabiashara nk. Hata mtoto wa maskini kuwa maskini inawezekana sana kama hatua za makusudi zisipochukuliwa kwa sababu hata mtoto wa Rais kuwa Rais huwa lazima jitihada ziwepo pia. Kipaji tu hakisaidii.
 
Jinsi ya kuutokomeza umaskini ni kuhakikisha wanafamilia wameenda shule na kupata elimu ya kutosha. Watu wakiwa na elimu wanaweza pambana angalau wakaweza kujimudu hata kama sio kuwa matajiri. Mzazi ahakikishe kwa namna yoyote ile mtoto apende shule. Binafsi nimesoma shule za serikali mwanzo mwisho. Mzee wangu alikuwa ananijaza sana matumaini.. yaani alikuwa ananijaza upepo nikienda shule hata bila pocket money najiona niko sawa na kuamini baba atatuma. Ile spirit niliyojazwa na mzee wangu ikanifanya niwashike wadogo mkono kwenye ishu za shule. Kwa sasa familia nzima imefika chuo kikuu na angalau kila mtu anajishughulisha.

Mbinu yangu ya elimu inaweza isifanye kazi pia kama wanafamilia hawana nidhamu. Familia iliyokosa maadili hata wawe na akili za darasani wanaweza bado wakaendelea kuwa maskini. Wanafamilia wanatakiwa kuheshimiana na kuishi kama timu. Sio mmoja ajione bora zaidi.
Hii ya kuishi kama timu ni bonge la point sema hatokesakana anaejiona yeye mbora zaidi na pia kama familia haina upendo wa kweli basi watamaind mwenzao akitoboa
 
Mkuu huwezi kuanzisha ukoo peke yako lazima ndgu ni muhimu, japo wengi hawana msaada, kuunganisha undugu ni kazi ngumu katika familia za kiafrica.
Unaweza, tatizo liko wapi ukiweka focus yako kwa mke na watoto wako, hao wajomba na mabinamu kama wanataka tuwe pamoja lazima waende na program la sivyo ni kufunga vioo tuu, sio ndugu tuu hata uchaguzi wa marafiki unaweza kuamua future yako, watu wa roho mbaya, negativity za kupeana stress, majungu, wachawi , wavivu etc kaa nao mbali sana la sivyo hutoboi
 
Jua kwamba matatizo mengi ya kifamilia ni ya kijenetic mengine ni ya kimazingira na mengine ni ya kimalezi na mengine ni ya kiroho. Yote haya yaweza kutengeneza mzunguko usio na mwisho (vicious cycle) ambapo ni ngumu kutoka.

Chunguza vizuri kujua nini chanzo cha kushindwa kwa familia au ukoo wenu, halafu chukua hatua stahiki.
Umeongea machache lakini mazito. Ikikupendeza elezea kwa undani zaidi.
 
Kuwepo kwa masikini na matajiri ndio kuna ifanya Dunia kua hivi ilivyo,ndio maana Mungu anasisitiza kua unapobarikiwa kipato usisahau kuwasaidia masikini coz alijua masikini watakuwepo,hatuwezi kua wote matajiri au wote masikini,

Kuutokomeza umasikini ni mwenye nacho kumsaidia asiye nacho kama Mungu alivyo sisitiza,ukiwa na uwezo na ukakutana na masikini,toa hicho kidogo ulichonacho umsaidie nae apate mahitaji japo kidogo,kila mtu akiwa na moyo wa kusaidia basi tutapunguza sana hili tatizo la kua na watu ambao hawamudu hata kununua chakula,

Utajiri ni mtihani na umasikini ni mtihani pia,maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya juu sana,Binadamu wote ni ndugu na hii Dunia tunapita tu,ukibarikiwa usisahau kuwasaidia wenye uhitaji,maisha ni fumbo.
 
Mkuu kama mtoto anaweza kurithi kipaji cha mzazi inashindikanaje kurithi umaskini? Haishangazi mtoto wa footballer kuwa footballer, mtoto wa rais kuwa rais, mtoto wa mfanyabiashara kuwa mfanyabiashara nk. Hata mtoto wa maskini kuwa maskini inawezekana sana kama hatua za makusudi zisipochukuliwa kwa sababu hata mtoto wa Rais kuwa rais huwa lazima jitihada ziwepo pia. Kipaji tu hakisaidii.
Mkuu umasikini sio kipaji ni hali. Hali hairithishwi, ila kazi na mali zina rithishwa, ndo maana ni rahisi mtoto wa raisi kua Raisi au mtoto wamkulima kua mkulima pia. Ila hayo yote yana changiwa na Elimu na juhudi binafsi ya mtu uhusika, hata kama baba ni Raisi lakini mtoto hana elimu sio rahisi yeye kua rahisi
 
Alisema usaidie muhitaji (anayehitji ila hana uwezo wa kukipata kwa namna yoyote,) hapa tutamhusisha mlemavu, mtoto, mgonjwa na wenye uhalisia wa kweli kiwa wanahitaji ila hakuna uwezekano kabisa wa kupata na hata wakikosa ni tatizo kubwa wanaweza kuwa kwenye hali mbaya au hatari kubwa na sio
mwenye nacho kumsaidia asiye nacho kama Mungu alivyo sisitiza,
Asiyekuwa nacho. Hii inafanya asiyekuwa nacho akae asubiri mwenye nacho ampe badala ya kupambania
 
Unaweza, tatizo liko wapi ukiweka focus yako kwa mke na watoto wako, hao wajomba na mabinamu kama wanataka tuwe pamoja lazima waende na program la sivyo ni kufunga vioo tuu, sio ndugu tuu hata uchaguzi wa marafiki unaweza kuamua future yako, watu wa roho mbaya, negativity za kupeana stress, majungu, wachawi , wavivu etc kaa nao mbali sana la sivyo hutoboi
Mtu mnae share nae vinasaba sio rahisi kumtenga litakusumbua uko mbeleni tu au watoto wako, bora uweke juhudi ya kuunganisha wakatae wenyewe.
 
Back
Top Bottom