Mnamo September 6 niliandika Uzi uliohusu Hali ya biashara yangu kukosa wateja, nilipokea maoni mbalimbali kwenye Uzi na PM pia (Nawashukuruni nyote kwa maoni yenu na ushauri )
Miongoni mwa PM nilizopokea ni za huyu dada (sitopenda kumtaja) dada huyu yupo Kigamboni
Alinifuata PM akanambia kama sitojari niende Kigamboni siku ya weekend tuweze kuonana huenda nitaongeza kitu chanya kwenye biashara yangu
Kiukweli nafsi ilinisuta nikasema usije kuwa mtego pia mtu mwenyewe licha ya kuonekana ni mcheshi kwenye comment na nyuzi zake hapa jf ila pia anaonekana ni mtu ambae masihala ni mengi na anapenda sana ushari hasa pale mtu akimkwaza
Kwanza sikujua kama ni ID ya kike licha ya kunambia yeye ni Ke ila sikujiridhisha kabisa 100%
Ila niliamua kumcheki jamaa yangu na kumwambia anisindikize kwa ajili ya usalama wangu.
Jamaa alikubali na akanisindikiza mpaka Kigamboni nilivofika nikamcheki PM akawa yupo offline maana hakutaka kunipa no ya simu basi nikavuta subra hatimaye akawa amenijibu na kunambia atafika hapo feri muda si mrefu hivo anikute NMB ATM ya feri.
Baada ya dakika kama 20 nikaona Toyata Rush ikipaki nje ya ATM mwanaume akashusha kioo cha gari huku akiwa anatuangalia sisi maana tulionekana kuzubaa akamwambia mwenzake ambaye ni huyu dada "bila shaka ni hawa"
Dada mzuri mrefu mweupeee alikuwa amevaa miwani na ushungi akashuka kwenye gari na kuniita Alparsalan maana nilikuwa nimemkazia macho kweli nikaitika akasema ni wewe nkamwambia ndio akasema upo na huyo akimnyooseha kidole jamaa alonisindikiza nkamwambia ndio akasema kama hamtojali ingieni kwenye gari tuondoke.
Nilisita kidogo ila jamaa yangu akasema twende tu tukaingia kwenye gari
Nitaendelea kuhadithia baadae nisiwachoshe