Genta hujawahi kuwa Chawa na naamini hautawahi kuwa Chawa wa Mtu yeyote.
Lakini Kwa hili la Kramo, aidha Kwa makusudi au Kwa kutokujua umejikuta unatumika kuficha madhaifu ya viongozi waliofanya usajili. Kramo ni injury prone na maneno ya Ahmed Ally juzi kwamba alitoka Asec akiwa na jeraha la goti ni sahihi na yanathibitisha watu wasivyo makini kwenye usajili. Viongozi wanasajili mchezaji Kwanza halafu ndo wanampeleka kwenye vipimo wakati malipo yake ya awali na manunuzi kwenye timu yake mama yalishafanyika. Hili limefanyika pia Kwa mchezaji mmoja (Kipenzi chako) ambaye Kwa Sasa ili kuficha udhaifu huo anachezeshwa dakika 25 Hadi 35 per match Hadi ukaanza kupiga kelele kwamba anabaniwa. Lakini ukweli ni kwamba tunampunguzia Muda wa kutumika na tunahakikisha anaingia Muda àmbao timu zimeshachoka na ameshauriwa asicheze Kwa kukamia hiyo kazi amuachie "Kiungo Punda". Yeye ni kupokea na kutoa, na pass za mbaaali.