Wewe na simu yako ni nani anayemiliki mwenzake?

Wewe na simu yako ni nani anayemiliki mwenzake?

Usipofanya deep analysis unaweza fikiria ni uraibu (addiction) lakini ukweli simu inatumika sana kwasababu ya mabadiliko ya teknolojia. Simu ndo kila kitu kwa sasa, huwezi kaa mbali na simu. Mfano mdogo majuzi kupitia simu nimetafuta,nime bargain, nimenunua, nimesafirisha mzigo kutoka sehemu tatu tofauti kwa wakati mmoja. Simu tu hiyo. Mimi nikiwa nimetulia zangu ofisini. Meanwhile mambo mengine nikiendelea nayo ndani ya simu hiyo hiyo. So matumizi ya simu yamekuwa makubwa kutokana na technology transformation na simu hazifumiliki bali upepo wa teknolojia ndo tunavuma nao. Mobile phone is everything.
I strongly agree with you kwamba simu ina faida kubwa sana, Lakini pia ikumbukwe kuna watu wengi ambao wamekua addicted na simu in a way ambayo haiwaingizii kipato au kuwasaidia kwa namna yoyote.

Kuna watu hushinda mitandaoni tu mda wote (social networks) just for Likes and so
 
Strongly Agree with you✅
Naaam hakuna namna unakwepa kwa sasa

Mails utazipata humu,

Taarifa iwe ya kazini, msiba, sherehe yoyote WhatsApp utaona,,

Mawasiliano ndo usiseme,, mfano WhatsApp tuu Kuna calls, na video kitu ambacho huhitaji kumwona mtu wakati video umeongea nae,

Yaani simu kwa sasa ni Kila kitu plus going with updates basi
 
Tuseme ukweli bila kupepesa macho
  • Unalala nayo kitandani
  • Ukiamka kitu cha kwanza ni kuiangalia
  • Ukiisahau nyumbani, siku yote unakuwa kama umetupwa kisiwa cha peke yako
  • Battery ikishuka chini ya 20% moyo unaanza kukudunda kama una deni.
  • Bundle likiisha kwa baadhi ya watu bora asinunue chakula anunue bundle.
Sasa swali ni moja tu: Wewe ndio unamiliki simu, au simu ndio inakumiliki wewe?

Na unapokosa muda wa kuishika, unahisi kama vile kuna mtu amekuondoa kwenye “group la maisha”😂😂
 
Back
Top Bottom