Mimi bwana naweza kuwa sielewi natoa wapi confidence , mimi kosa lako kunipa muda nionngee hapo kaa ujue sitakuogopa hata uwe nani .
Nilifumaniwa na wanakijiji na mke wa mwanakijiji , nikatimuliwa ili nipigwe nikaingia kwenye ofisi za kijiji , huku nawaza nachomokaje , kosa ni pale mtendaji aliposema nijitetee niliongea kama lisaa wanakijiji wakaanza kutawanyika mmoja baada ya mwingine .
Hapo nataja vifungu vya sheria kuwa wakiniuwa basi wanalo wataacha familia zao , mara utajiri wao utakoma mpaka namaliza nilikuwa na watu wanne tu , demu niliyefumwa naye , mmewe na wazazi wa binti wakaitwa ndani tukayajenga ikanitoka mia hamsini maisha yakaendelea .
Hivyo mimi nikianza kuongea hata uwe nani sikuogopi tena .