Sasa kwa nini hayo mataalamu yasirudi Afrika kusaidia kuleta maendeleo?
Ni kweli hakuna ajuaye kila kitu lakini usiniambie katika mijitu millioni 40 hatuna watu wanaojua mambo ya kilimo.
Duhhh, umeshindwa kunifahamu kabisa, kwanza wataalamu ninaoongelea mimi ni wale ambao wanaishi Tanzania na kutakiwa kutowa ushauri wao nje ya hapa, si tu kuwa huko wanakokwenda hakuna wataalam, no, wapo lakini kupeana ushauri ni wajibu wa ubinadam.
Siwezi kukwambia kuwa "katika mijitu millioni 40 hatuna watu wanaojuwa mambo ya kilimo" bali ntakukumbusha:
1) mashamba ya mbarali, yalipoanzishwa na wachina yalikuwa yalizalisha vizuri sana mpunga, walipoondoka yamekufa kuzalisha na wataalamu wetu wa kilimo walikuwa wapi?
2) Mashamba ya ngano ya katesh, hali hiyo hiyo, haya yalianzishwa na wa-canada.
3) Mashamba ya mkonge, haya tuliyataifisha kutoka kwa watu mbali mbali wengi wao wakiwa wagiriki na yapo zaidi Morogoro na Tanga, yalikufa kabisa, baada ya kupewa wawekezaji, tunaona yanafufuka. Kulikoni na waTaalam wetu?
Kwa hayo inabidi tupate ushauri, kwa nini tushindwe? labda there is something very wrong with us? what is it? tungoje washauri wanasemaje, tukifata tusifate ni shauri letu. Kwa hili la kutaka ushauri unaweza kunipa ubaya wake? wakati wenyewe tunafanya madudu?