Natamani ningeandika kwa ID nyingine.
Sijipendi, sioni sababu yakuishi. Sifurahii maisha na sijui ni kwa nini. Sina maisha mazuri ila ninakula na kulala kwangu na siombi cha mtu.
Ukiniona huwezijua kama moyo wangu umepondeka kwasababu ninadress smart, ninacheka inapobidi (sio sana), ninachangamka nikiamua.
Sina hofu ya aina yoyote kwenye maisha yangu.
Sijisikii tena kuchase ndoto zangu.
Tangu nipo shule ya msingi nimekua nikijaribu kujiua ila nashindwa. Sijui kama ngao ya maji ilikua haiui ila nikiwa darasa la sita nilikunywa ngao na sikufa wala sikuumwa tumbo. Vingine siwezi kuandika. Jaribio lamwisho la kujiua nililifanya nikiwa form six. Halikufanikiwa
Mwaka jana nilipata kazi serikalini, msimamizi mkuu wa ngazi ya wilaya akanitishia kunifuta kazi kwa sababu zisizo za msingi, nikamwambia me nimeshaifuta hiyo kazi kichwani, kazi kwako.
Mwaka huu mkurugenzi wa mamlaka niliyopo kwa muda alikuja kiukaguzi akaongea maneno machafu sana, akatusimangia watu chai ya ofisi nikamwambia mkuu ni chai ya rangi na chapati mbili kama unaona tunafaidi sana sema tukuagizie kuliko kuitolea macho ukudhani ni chai zenu za makao makuu.
Sijui kama mtoa mada alitaka haya au mengine, nowadays nina mashaka hata na uelewa wangu.