What are random interesting facts about yourself?

What are random interesting facts about yourself?

Well kwa watu smart. Hili swali lako litawafanya watu wengi wa spill details zao binafsi bila wao kujua.
Details hizi zinaweza kuchukuliwa na watu au mtu .. ana akatengeneza character yako kupitia uliyo yasema.

Pia inaweza kutumika kumsoma muhusika na id yake.

So to me no thanks man. Ningeweza but it too risky kuweka character yangu on public.
Tanzania kuna watu milioni 60 almost, sidhani kama itakuwa rahisi kiasi hicho cha kumjua kila mtu kati ya watu 60m.
 
1.Mzee wa kutabasamu na matani mengi
2.Ni "simba" kwani nyama ndio chakula kikuu.
3.Sio mpenzi wa soka
4. Art collector
5. Mpaka leo duduwasha akipita sehemu napata goosebumps
 
Kwanza mi ni mtu ambaye siipendi shule na kwa bahati nzuri au mbaya hata crew yangu huko shuleni tulikia tuna altitude sawa

Nilikua nagombana sana na dingi kwenye swala la shule ilifika mpaka hatua nimepelekwa polisi kupigwa kwa usumbufu wangu

Katika umri wa miaka kama 8 niling'atwa na mbwa kichaa. Nililazwa hospitalini na kupachikwa dripu nane na kwa bahati mbaya dawa ya mbwa kichaa haikuwepo pale hospitali.

Hivyo ikabidi itumwe ambulance mpaka hosptali nyingine ambayo iko kilometa 30 kutoka hapo.

Nilidumu hospitali kwa muda wa wiki 4 na nusu nikatoka nikiwa niko fresh
 
Ngoja na mimi niandike.
Tangu darasa la 3 hadi la 5 nilikuwa "monitor".
Darasa la sita na la saba nilikuwa " Dada mkuu".

Form 1 na form 2 nilikuwa "Monitress" .
Form 3 nikawa kiongozi wa michezo na Monitress.
Form 4 nikawa kiongozi wa chakula na Monitress.

Five na six nilikuwa mweka hazina wa kikundi chetu cha dini.

Chuo nilikuwa CR miaka yote na Mbunge mwaka wa pili.

Kazini Mimi ni mwalimu wa nidhamu.


Mara nyingi walimu wa nidhamu huwa wanakuwa wanoko Sana, wewe kwako ikoje mkuu?
 
Sina rafiki wa kusema huyu ni rafiki yangu, am mostly quite, sipendi makelele, sidumu katika mahusiano ya kimapenzi na muda mwingine huwa nayaona ni kero. Am good Hearted Man, nisiyejuta wala kulaumu kwa chochote nitakachoamua kukifanya. Sipendi kuwa Threatened au Threatening anyone, sipendi mikusanyiko.

Am Introvert.
Umezaliwa tarehe ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
To be honest sindano naziogopa sana mazee


Bora niandikiwe ndoo 2 za lita 20@ za vidonge Kuliko sindano 1, vile inaingia, wanapause Kwanza, afu wanasukuma dawa, halafu wanachomoa...aaggggggrrrrrr
 
Nikiendaga ugenini sitamani tena kurudi nyumbani napenda kuishi nyumba yenye watu wengi sana nadhani nimeathiriwa na kuzaliwa mwenyewe na kuishi na mama tu.
 
Tanzania kuna watu milioni 60 almost, sidhani kama itakuwa rahisi kiasi hicho cha kumjua kila mtu kati ya watu 60m.
Kuna methods za kumfaham tu . America wana 300+ plus ,mpaka leo NSA wana read emails na sms za watu ku detect wenye nia mbaya. And wanaweza mpin point na kumpata.
It all possible.. unahotija ni methods na resources.
 
Back
Top Bottom