What are random interesting facts about yourself?

Mie huwa namshukuru sana Mola kwa kunijalia kipawa cha kuichambua hesabu katika ngazi ya elimu kuanzia msingi hadi chuo kikuu na sasa kazini.

Ila sasa, ni hesabu ndogo sana ambayo imenipiga chenga kabisa kuielewa hata nijitahidi vipi itanitoa tu na si nyingine, bali ni kuhesabu mzunguko wa siku za mwanamke. Sijui ni kwa vile nakua busy kiasi kwamba sina focus na hizo mambo za dates zao.
 
karama ya uongozi
 
Mimi katika vitu ambavyo watu nawashangaa na mpaka muda huu sijapata sababu yenye kunishawishi ni nyie watu ambao mnaogopa vidonge halafu sindano hamuogopi

Kuna dawa moja inaitwa "palamalanget" (sijui kama nimepatia) hiyo dawa ni kali kinoma lakini nilikua napita nayo kwenye glass kama juice ya miwa vile. Hii miarobaini arobaini ndio hata stimu ya ukali sijawahi kuiona naona ka ipo overrated tu

Mwaka jana ndiyo ilikua mara yangu ya tatu kuchoma sindano baada ya kukanyaga msumari wenye kitu. Ikanibidi nikachome tetenus lakini kabla ya yote nilimuuliza dokta hakuna option ya vidonge akasema hakuna

Nikaona anaongopa nikapiga simu kwa daktari ambaye ni rafiki yangu naye akaniambia hivyo hivyo, nikaona wote wazugaji nikaingia hadi google nikakutana na jibu lilelile. Ikanibidi nichome tu japo kiugumu sana

Mkuu sindano naziogopa sana
 
mkuu kabla ya kuwa mboga ni mnyama yule
Mimi nyoka naziogopa sana, yani kama nyoka kaingia ndani na hajauliwa halafu hakuna aliyemuona akitoka basi humo silali.

Huu uoga niliupata kipindi mdogo ambacho nilimkanyaga kifutu bila kumuona ila bro alikua nyuma alivyoona aka-shout nikaruka kwa hofu nilikua nimemkanyaga katikati kwenye kiwili wili.

Kama hiyo haitoshi nilishawahi kumshika nyoka juu ya mti nikadhani ni tawi la mti kutokana na rangi ya yule nyoka kua yakijani. Mwili wote ulisisimka hapo ndio nikaamini kua mtu aliyekoswa na nyoka hata jani likimgusa hukimbia

Wengi wasioogopa nyoka mara nyingi hawajawahi kukitana na visanga vyake, wengine wamekulia ushuani nyoka kumuona sio rahisi wengi nyoka wamewajulia kwenye sinema au mabanda ya maonyesho ya wanyama.
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒ dahh pole sana. .. narudia tena mkuu mimi na vitu vichungu tuko tofauti.. muarabaini ndio kabisa siuwezi
 
πŸ˜„πŸ˜„ mimi nyoka simuogopi kabisaa.. ila huwa nina tension kubwa sana dhid yake ukitokea nikiwa na tembea katika majani huwa nawaza labda naweza kumkanyaga so nakuwa,natembea kwa uangalifu,mkubwa,mnoo cause nalijua balaa. lake
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒ dahh pole sana. .. narudia tena mkuu mimi na vitu vichungu tuko tofauti.. muarabaini ndio kabisa siuwezi
Niliumwa washkaji wakaniambia kapime tukafika kwenye ki-dispensary dokta akaniambia lete kidole tukuchukue vipimo.

Nikamuuliza hicho kipimo unakichukua kwa mtindo upi akasema nataka damu yako niifanyie vipimo ili tujue kwa hakika ugonjwa unaoumwa.

Nikamuambia nina jeraha bichi nililoumia leo unaonaje nikamue damu nikupe ufanyie vipimo kuliko kuniongeza kidonda kingine. Dokta akawa anacheka mi nikamjibu niko serious ka vipi we nipatie mseto tu swala la kutoboana naona dusko tu
 
πŸ˜„πŸ˜„ mimi nyoka simuogopi kabisaa.. ila huwa nina tension kubwa sana dhid yake ukitokea nikiwa na tembea katika majani huwa nawaza labda naweza kumkanyaga so nakuwa,natembea kwa uangalifu,mkubwa,mnoo cause nalijua balaa. lake
Kuna nyoka mmoja anaitwa swila yule nyoka hanaga limitation kwenye ukuaji. Nilimkuta mtoni tulikua wawili kipindi hicho watoto hapo tuko kuwinda.

Aisee yule nyoka alikua mrefu kishenzi ilikua kila asubuhi unamkuta kajianika anaotea jua. Kuna siku nilikua niko alone nikapita sikumkuta lile eneo anapopendelea kukaa. Nilipofika mbele nikastaajabu kuona nyoka anapita alikua ametokea upande wa majani sasa katikati kuna njia ambayo ukiivuka hapo unakutana na majani mengine yani njia iko katikati ya kimsitu. Ile njia ilikua inaupana wa futi kama 5 hivi

Lakini yule nyoka alivyopita pale sikuweza kujua wapi kichwa wapi mkia
 
daaah hakukufanya kitu? huyo sindiye koboko black mamba. . ni nyoka hatari sana
 
daaah hakukufanya kitu? huyo sindiye koboko black mamba. . ni nyoka hatari sana
Ndugu yangu acha tu yule nyoka hakuwahi kuuliwa nadhani alisepa mwenyewe na kama alikufa huko alikoenda labda kwa ugonjwa maana huo muonekano wake hata mbwa zilikosa ushirikiano siku ile
 
Ndugu yangu acha tu yule nyoka hakuwahi kuuliwa nadhani alisepa mwenyewe na kama alikufa huko alikoenda labda kwa ugonjwa maana huo muonekano wake hata mbwa zilikosa ushirikiano siku ile
aahhh koboko unamuuaje sasa? labda mumtegee sumu.. wataalamu wa mambo wanasema anauwezo wa kuua watu 100 ndani ya dakika kadhaa tu. labda kama alikufa kwa mafuriko.. mshukurusana. hakuwaanzishia songombingo
 
LIKES

*Tangu mdogo napenda sana RADI, both Thunder & Lightning...nikiwa mdogo mvua ikinyesha nimekuwa nikifungua dirisha na kusikiliza mngurumo wa radi na kuangalia miale yake hata usiku, hadi wadogo zangu walinishangaa

*Pia napenda sana kuangalia anga, Galaxy at large nikiona nyota, mwezi natamani nizifuate nikashike

DONLIKES :

- Mlenda, sili na siwezi kaa karibu na MTU akiwa anakula

- I have trypophobia, nikiona vipelepele au vinundu vingi mahali pamoja nachefukwa kbs.
 
Sijawai kua kiongozi katika level zote za shuleni hadi kazin hii naisi ni sababu sikutaka kuoneka mbaya ile kumshurutisha mtu afanye kitu.
Nilisema nitakua tu kiongozi wa familia yangu Allah akijalia siku moja.
Napenda kukaa peke yangu lakn naenjoy watu wakiwa around tunapiga story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…