Kwanza, vipande ambavyo mpaka sasa vimethibitishwa kuwa ni vya kutoka kwenye ndege hiyo ni vitatu [3].
Vilithibitishwa kwa kutumia “unique identifiers” za hiyo jetliner.
Kipande cha kwanza kilipatikana huko Pemba. Ni kipande cha ubawa wa ndege.
Cha pili kilipatikana Mauritius. Nacho ni kijisehemu cha ubawa wa ndege.
Cha tatu ni kinachoitwa flaperon. Kilipatikana kwenye visiwa vya Reunion.
Hivyo ndivyo ambavyo wachunguzi wa mambo ya ajali za ndege wakishirikiana na shirika la Boeing pamoja na Malaysian Airlines na parts makers waliweza kuthibitisha kwa uhakika kwa kutumia ‘unique identifiers’ na ‘parts identifiers’.
Vitu vingine vilivyopatikana vinahisiwa na kusadikika tu kuwa huenda ni vya hiyo ndege au vya abiria waliokuwemo kwenye hiyo ndege lakini hakuna uthibitisho.
MH370: Here's what's been found from missing jetliner
Wiki iliyopita, tarehe 8 Machi, imetimia miaka 6 tokea ndege hiyo ipotee na bado hakuna ajuaye kwa uhakika nini kiliikumba hiyo ndege na wapi ilipo.
Vipande vilivyopatikana havitoi majibu kamili ya nini kilitokea, wapi kilipotokea, kwa nini kilitokea, na muhimu zaidi, ndege yenyewe iko wapi au sehemu kubwa ya hiyo ndege iko wapi.
Ndugu wa abiria waliokuwemo kwenye ndege bado hawana majibu ya kilichoitokea hiyo ndege.
Malaysia Airlines Flight 370 remains mystery six years on as families appeal for new search