Paula Paul
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,649
- 13,607
- Thread starter
- #241
Hii ya Finland nimeielewa vyema asante nitapata cha kusimulia.Hiyo ya Finland wanadai kuwa Finland haipo ila Russia na Japan ndio wametengeneza uongo huo(kuwa kuna nchi inaitwa Finland) ili wawe wanavua samaki katika maeneo hayo bila kuingiliwa. Na wanadai hata kujengwa kwa Trans Siberian Railway ilikuwa ni kwa lengo la kusafirisha samaki hao kwenda Japan na samaki hao wanasafirishwa kwenda Japan kwa kificho kwa kuziziba kwa bidhaa za Nokia ili ionekane kama ni bidhaa za Nokia ndio zinasafirishwa.
Na kulithibitisha hilo wanasema ndio maana Japan ndie importer mkubwa zaidi wa Nokia products duniani licha ya kuwa ni watu wachache tu ndio wanaomiliki simu za Nokia Japan. Wanadai pia hata jina la Finland linaanza na "fin" kwa sababu samaki wana "fins". Kuongezea zaidi wanadai wanaodaiwa kuwa ndio raia wa Finland, kiuhalisia ni raia wanaoishi aidha Sweden, Estonia au Russia. Na hata Helsinki, ambao ndio mji mkuu wa Finland,wanadai unapatikana mashariki mwa Sweden. Wanadai picha zote za anga zinazoionesha Finland ni feki na marubani wote wanaoruka juu ya anga ya hiyo nchi inayodaiwa haipo wanapewa hongo ili waseme kuwa kuna nchi inaitwa Finland.
Na kuhusu hiyo ya Ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea March 2014 kuwa ndio ndege ya Malaysia MH17 iliyodunguliwa Ukraine July 2014, wanadai Malaysia MH370 haikupotea bali ilifichwa tu na baadae ikawa reintroduced kama Malaysia MH17 na kudunguliwa July 2014 kwa sababu za kisiasa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ya ndege kama ilifichwa na kuwa reintroduced vipi abiria waliokuwamo ndani?.