Jambazi "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu", wote wakalala chini
HII INAITWA DHANA
YAUSHAWISHI - kubadilisha
njia ya kawaida ya kufikiria
••••••••••••••••••••••
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini kimitego, Jambazi
akamwambia, "dada hebu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio laujambazi na sio la ubakaji.”
HUU UNAITWA WELEDI -
zingatia ulichofundishwa
kufanya
•••••••••••••••••••••••
Walipotoka kwenye wizi
jambazi mdogo ambaye
anashahada ya uzamili ya
biashara akamwambia
mwenzake, "tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina haja
ya kuhesabu saa mbili
watatutangazia kwenye
taarifa ya habari tumeiba
kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI - Siku
hizi ujuzi ndio bora kuliko
vyeti
•••••••••••••••••••••••
Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, "ujumlishie na zile milioni 80
tulizo iba sisi.”
HUKU KUNAITWA KUOGELEA
NA MKONDO WA MAJI -
kushabihiana na mazingira
magumu kwa faida binafsi.
•••••••••••••••••••••••
Mhasibu akafurahi na
kusema, "dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.”
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi
•••••••••••••••••••••••
Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza. HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama
ni hatari kiasi gani.
•••••••••••••••••••••••
usiku wake taarifa ya habari
ikatangaza kuwa wizi
mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki.
Majambazi kuskia hivyo
wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah!yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli? Bora umeneja kuliko ujambazi. HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana elimu
ina nguvu kuliko dhahabu[emoji120]