Whatsssssss!!!!!!!!!????

konda anamwambia dereva "NIULIZIE HUYO MZUNGU KAMA ANASHUKA POSTA" dereva kajibu 'waambie abiria wakusaidie mm jino linaniuma' [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Padri alitangaza kila mtu atoe mchango kulingana na uzuri wa MUME wake. Basi watu wakaanza kutoa 15,000, 300,000 na
2,000,000.
Kuna mama akatoa 500. Padri akamuita na kumuuliza,
PADRI: Ina maana mumeo
sio mzuri?
MAMA: ukimuona
utanirudishia na chenji! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DOGO: Eti baba mtu stupid yuko je?
DADDY: Hilo ni swali zuri sana, a very good kweshen kwa kweli I am praud of you, you see mwanangu,
mtu stupid ni yule ambaye akiulizwa just a simpo kweshen, yaani swali dogo sana basi huanza kulinyumbulisha na kuongeza mofimu na fonimu katika hilo swali,
kuanza kutafuta, tena infact bila mantiki yoyote basis ya swali,na baada ya hapo kufanya mchanganuo na hati mae kukam up na solushenz ambazo in prinsipo hazikuweko katika swali husika kiasi cha kwamba aliyeuliza swali anakuwa haelewi hata kitu, umeelewa??
DOGO: Hapana [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa karuhusiwa kutoka hospitali ya vichaa, akapandishwa kwenye ambulance hadi karibu na kwake, akaulizwa unapakumbuka kwako? akajibu ndio nyumba yangu ileee, wakatoka watoto wawili wamevaa unifom akasema wanangu walee wanaenda shule, akatoka mwanamke akasema mke wangu yule, ghafla akatoka mwanaume akasema na mimi ni yule naenda kazini. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dogo mmoja umri 12, awaacha watu midomo wazi ni baada ya kuingia club na kuagiza bia ya "kilimanjaro" kama vyupa 11.
Kimbembe ni pale waiter alipokuja na kuhitaji malipo.
Mara Dogo" kazama mfukoni na kuchomoa bango la Kilimanjaro ambalo chini limeandikwa kwa maandishi makubwa:
"ONYO, HAIUZWI KWA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18" [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Gari imeondoka KARIAKOO kufika MANZESE konda akauliza kuna mtu anashuka?
ABIRIA: Tumeziacha nyumbani tuna mitandio tu." kufika mbele..
abiria mwenye nyodo akawa anashuka UBUNGO MAZIWA. Akasema;
"Konda nashuka maziwa."
KONDA: "Itabidi urudi mjini ukanunue Sidiria." [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ustazi mmoja aliletewa zawadi za pensi tatu kutoka Oman,
Alipendelea sana kuivaa na kanzu wakati wa swala,
Siku moja alichelewa swala ya Ijumaa, na ilimbidi avae kanzu na kusahau kuvaa pensi kwa haraka zake,
Wakati anatia udhu miguuni alipandisha kanzu juu kabisa kiunoni na makalio yakawa wazi bila kujua, waumini wakamuuliza kwa mshangao baada ya kumuona Ustazi makalio wazi.
Heh! Vp Ustazi!? ustazi akajibu kwa mbwembwe...!
"MAMBO YA OMAN HAYO..! ninazo nyengine 2 nyumbani" [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwenye kituo cha bus manzese jamaa kanyewa na kunguru kichwani.
Jamaa akaangalia juu alivyogundua amenyewa akamuona kunguru usawa wake, jamaa akaangua kicheko sana yaani.
Watu wakamuuliza: “sasa unacheka nini ndugu yangu wakati umenyewa?”
Jamaa akajibu: “We acha tu, afadhali bata hawapai angani kama kunguru” [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
DOKTA: dah Mungu mkubwa mama.
MAMA: kwa nini dokta?
DOKTA: umezaa Jembe
MAMA: (kazimia)[emoji13]
kumbe dokta alimaanisha kajifungua mtoto wa kiume[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mama mmoja alimtuma mwanawe wa miaka sita (6) aende dukani akanunue unga robo na maharagwe. Wakati mwanae anatoka akamwambia
MAMA: Angalia magari barabarani siku hizi ajali nyingi
MTOTO 1: Haya mama
Baada ya saa moja kupita mama akaona huyu mtoto atakuwa amepotea ama anacheza akamtuma mtoto mwingine akamuangalie na amwambie arudi haraka. Wakati anatoka huyu mtoto mama akamkumbusha
MAMA: angalia magari huko kuna ajali
MTOTO 2: Haya
Mtoto huyu nae akaenda.
Baada ya saa jingine kuisha mama akatoka kwa hasira na kuwafata huko dukani. Alipofika barabarani kabla hajavuka kwenda dukani akawaona watoto wake wamekaa katika matofali wanaangalia magari
MAMA: (kwa hasira) mnafanya nini hapa?
MTOTO 1: Tunaangalia magari
MAMA: mitoto mijinga kweli, ndo nilichokutuma hicho?
MTOTO 2: ndo nasubiri ajali nirudi [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
BABA: Sikiliza Dogo akija mtu kunitafuta mwambie nimesafiri
DOGO: Sawa baba.
MGENI: Dogo baba yako yupo?
DOGO: Baba kasafiri
MGENI: Kaenda wapi?
DOGO: Ngoja nikamuulize.
DOGO: Mgeni anauliza umesafiri umeenda wapi?
BABA:Mwambie nimeenda Songea.
DOGO: Baba kasema ameenda Songea.
MGENI: Basi akirudi mwambie anitaarifu [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Una sura ngumu mpaka nikikupiga picha inajisave kwenye tools.
Anhaa TWENDE TWENDE
--Wewe ni mweusi hadi ukibeba mtoto anasinzia anajua giza limeingia!
--Kwenu mpo wengi mpaka mtoto wa mwisho anaitwa etc.
--Dingi ako kazoea kuendesha baiskeli hata akipanda gari anakunja suruali.
--Kwenu muko wengi mpaka babako akiingia anasema hamjambo wananchi.
--Una macho mekundu, ukiangalia maindi yanaiva.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Baba, mama na mtoto wao wamelala, ghafla usiku
MTOTO: mamaa nataka nikakojoe
MAMA:chukua tochi
mtoto akanyoosha mkono anatafuta tochi kumbe baba kalala uchi mtoto akashika naniihino ya baba yake akidhani tochi.
BABA(kwa kuzuga):we acha hiyo haina betri. [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna jamaa moja alienda kuiba kuku alipoona anafuatwa akakimbilia mtoni.
Halafu jamaa kufika mtoni akamtoa kuku manyoya kisha akamrusha kwenye maji.. Watu walipofika wakamuuliza: kuku yuko wapi!?.
Mwizi: kaenda kuogelea yule kule amenipa nguo zake nimshikie akawaonesha manyoya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mume mvivu aambiwa na mke wake :mume wangu si unisaidie kazi za bustani
MUME: kwani mi ni houseboy?
MKE: basi nisaidie kutengeza mlango
MUME: kwani mi ni carpenter?
MKE: basi nisaidie kutupa taka taka,
MUME: kwani mi ni manispaa?
(mume aliporudi jioni)mke wangu nani amesafisha bustani,akatengeza mlango na kutupa taka?
MKE: ni jirani yetu swaleh lakini alinipa options mbili nimpe wali ama nilale nae,
MUME:hahaha,najua ulimpa wali,
MKE: Kwani mi ni hoteli? nililala nae kwa taarifa yako [emoji12][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Kuna makonde mmoja alienda kwa muuza chipsi
MTEJA: nikaangie chahani moja
MUUZAJI: tomato unataka?
MTEJA: tomato chili
MUUZAJI: akamuekea kila kitu.
MTEJA: akasusa kwa kusema..Nchakwambia tomato chili chacha wewe umeweka chacha chitaki..! [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Idea ngumu sana hii,
Ameeein.
 
We jamaa kibookkoo,
Umemshikia kuku nguo zake.
 
Yalaaaaahh ..!!
Hatari sana hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…