Whatsssssss!!!!!!!!!????

Whatsssssss!!!!!!!!!????

1479553368263.jpg
 
MKE: Vipi leo mbona leo umerudi mapema na mpole hivyo?
MUME: Ofisi yetu imeungua moto na watu wote wamekufa.
MKEWE: Sasa ilikuwaje wewe ukapona?
MUME: Nilikuwa chooni, nje kidogo na ofisi.
MKE: Loh maskini familia zao zitakuwaje?
MUME: Watalipwa milioni 200 kila mfiwa.
MKE: umenikosesha mihela yote hivi hivi!! Hebu rudi huko ukaungue na wewe ufe kabla moto haujazimika! [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya.

MUME: Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama hajisikii vizuri. Tunaweza kwenda kumnunulia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kumtembelea?

Tafadhali andika orodha ya mahitaji kisha tuondoke.

MKE: Orodha ya vitu hivyo sio muhimu, tutanunua tu kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia.

MUME: Vitatosha kweli?
MKE: Ndiyo mpenzi, hakuna haja ya kupoteza pesa, vitatosha.

Walielekea mjini na kununua kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia. Wakati wakinunua mume alimuuliza mkewe tena kama vitu hivyo vingetosha.

Mke alisisitiza zaidi kuwa hawatakiwi kutumia pesa nyingi kwenye ziara ya kushtukiza.

Walianza safari kuelekea kijijini, na walipofika kwenye eneo la njia panda yenye barabara zinazoelekea vijiji mbalimbali, mume alikata kona kuelekea kwao na mke.

MKE🙁Kwa mshituko) tunaelekea wapi mpenzi? Nilidhani tunaenda kumtembelea mama yako.

MUME: Ndiyo, ndiko tunapoelekea, ni mama yako(mama yetu) ndiye anayeumwa.

MKE: (kwa mshituko na kilio), lakini mahitaji haya hayatoshi. Turudi tuongeze vitu vingine.

MUME:Hapana! Nilikuuliza tena na tena kama mahitaji hayo yanatosha, ukaniambia “NDIYO”. Hakuna kurudi

FUNZO:Wafanyie wenzako kile unachotaka ufanyiwe!!

Mume hapendangi ubaguzi[emoji12][emoji13][emoji13]
 
KUMBUKUMBU
1.Hata uwe mtaalamu wa internet kiasi gani huwezi kudownload msosi.
2.Hata kama Mwl. Nyerere ni babuyako kamwe huwezi kuwa mjukuu waTaifa.
3.Hata isomwe kwa mbwembwe na bashasha tele ila fahamu kwamba historia yamarehemu haipigiwi makofi.
4. Hata uwe busy kiasi gani huwezi kumuagiza mtu akuendee chooni.
5. Calculator ina batons lakini huwezi kuchati nayo.
6. Hata uwe na haraka kiasi gani huwezi kufunga supu kwenye gazeti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
MWALIM: utafanya nini endapo mama yako amepigwa na butwaa na bumbuazi?.'
MWANAFUNZI: Kitu cha kwanza mimi nitaenda kwa kina butwaa, nampiga ngumi butwa lakini simuuwi, sababu yeye ndio atanipeleka kwa bumbuazi nimuulize kwanini walimpiga mama yangu. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
MGONJWA : doctor nikikojoa nakojoa mkojo wa njano
DOCTOR: mara ya mwisho kufanya mapenzi ni lini?
Shikoh : tangu mwaka jana
DOCTOR: hio ni KUTU inatoka [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
JOB VACANCY[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
Je unatafuta ajira nzuri inayolipa?
1) Mshahara Tsh 900,000/= kwa mwezi.
2) Mda wa kazi kuingia kwanzia saa 8:30 hadi saa 4:00 jion
3) Allowance 300,000/= kwa mwezi
4) siku za kazi jumatatu hadi ijumaa
5) Usafiri na nyumba ya kuishi ipo
REQUIEREMENT
1) Cheti cha form four & form six (CSE&ACSEE)
2) Elimu ya chuo{Diploma au Bachelor degree}
3) Hakuna uzoefu unaohitajika
4) Umri kwanzia 18-45. Kama unahitaji hiyo kazi basi usijali . Njoo ungana na mimi tuanze kuitafuta maana hata mimi ninaitafuta kazi kama hiyo.
 
Tafiti kwa tafiti
1.Cuba......Doctors
2.America...... Technology
3.Brazil......Football
4.China......Architecture
5.Japan......Electronics
6.Germany...... Mechanics
7.Britain......administration
8.Italy......Shoe/Clothing
9.Jamaica...... Reggae
10.Israel...... Scientist
11.Netherlands. ..Engineers
12. Tanzania .?????[emoji12][emoji13][emoji23][emoji23]
 
Jamaa alikosea kutuma m-pesa sh 500,000/= ikaenda namba nyingine, kuona hivyo akaumiza akili akatuma meseji ifuatayo kwenye namba hiyo." UMETEULIWA KUINGIA CHAMA CHA FREEMASON NA UMETUMIWA PESA, BAADA YA DAKIKA 15 ATAKUFA MWANAO UMPENDAE. HARAKA KAA NJIA PANDA GARI YETU NYEUSI ITAKUFUATA UJE UNYWE DAMU YAKE.! KAMA UMESHINDWA MASHARTI RUDISHA PESA HARAKA KABLA YA MAAFA" baada ya dakika 1 tu jamaa akaona salio limerudi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
JAMAA: Hello Salome! Uko wapi?
Nimekumiss
DEMU: Hny niko Samaki Samaki hapa napata Lunch, then namsubiria driver wangu aje kunichukua anipeleke Chuo, wewe uko wapi?
JAMAA: Nipo siti ya nyuma ndani ya hii daladala ya Mbagala Uliyopanda, nilitaka kukwambia nimeishakulipia nauli. Usilipe[emoji12][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mpenzi akikupigia usipopokea atakutext.
MZUNGU: ''Honey what's wrong!, are you alright? I hope you are safe, call me back love you!!
MPENZI WA KIBONGO: ''Wewe mshenzi umalaya utakuua mbwa wewe na mwaka huu ukimwi utakumaliza.'' [emoji12][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtoto kaibiwa, jambazi akampigia simu baba yake mtoto,
JAMBAZI: kama unataka mtoto wako lete milioni 20 ndio utampata mtoto wako,
BABA: kwanza nataka kujua mtoto wangu mnampa chakula?
JAMBAZI: tunampa
BABA: mnampa maji ya kunywa?
JAMBAZI: tunampa
BABA: mnampa pakulala?
JAMBAZI: ndio
BABA: kama ni hivyo, basi njoo uwachukuwe na ndugu zake.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee mmoja wa baraza alikuwa anasinzia wakati wa Kesi moja ya shambulio..
HAKIMU..Mlalamikaji ieleze mahakama ulichoambiwa na mshtakiwa
MLALAMIKAJI..Mh hakimu siwezi litamka neno aliloniambia maana ni tusi labda niliandike ktk karatasi mlisome
Basi akaandika alichoambiwa kuwa (NATAKA
TWENDE TUKA ZINI) kisha akampa hakimu asome.
Hakimu akasoma kisha akampa mzee wa kwanza wa baraza naye alipokisoma akampa
mzee wa baraza anayefatia ambaye alikuwa mwanamke baada ya kukisoma akampa mzee
wa mwisho ambaye alikuwa usingizini, akamshtua na kumpa kikaratasi, mzee akiwa hajui kinachoendelea akakisoma kisha akamuuliza yule mama... SASA HIVI AU MAHAKAMA IKIMALIZA MUDA WAKE? [emoji12][emoji13][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
ukiona mrembo wako hajibu meseji zako, we wala usijali, mtumie msg hii.
"Baby umepata hiyo hela?"
Asipojibu hiyo nambie nijitoe JF[emoji12][emoji13][emoji13][emoji13]
 
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi... njoo ndani uone mwenyewe.
wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla,
MZEE: 'Nyie mnafanya nini hapa?'
DALALI: Tunangoja treni' [emoji12][emoji13][emoji13]
 
Yani hapa kuna kamuchezo nakacheza ni katamu kweli hebu jaribu uone utamu wake. WEKA VIBRATION SIMU YAKO ALAFU IDUMBUKIZE NDANI YA PIPA AU NDOO YA MAJI ALAFU UONE INAVYODUNDADUNDA. Hasa kama simu yako ni BLACKBERY AU SAMSUNG GALAX au NOKIA ASHA WEKA kwa wenye simu za mchina si saana. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom