Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Kwa andiko hili heshima ya JF inarudi kabisa. Hongera Sana Mkuu. Well researched.
 
Halafu kuna wapiga jaramba eti watajwa wawili hapo eti ni presidential material.
 
Huwa najiuliza tu kama kwa 1B mtu mzima wa umri wa miaka 40 tu anaweza kula maisha ya kawaida tu kula kulala mpaka akafa na still pengine akaiacha chenchi ya hio pesa kwa watoto.

Je, inakuwaje mtumishi anadokoa labda billion 20 na still bado ana tamaa tena ya mahela zaidi? Huyo mtu ikumbukwe analipiwa almost kila kitu na ofisi anapofanyia kazi!

Hayo mahela unaiba sijui billion 100 kesho tena unadokoa billion 50 hivi mahela yote huwa wanafanyia kitu gani? Au ndio wanajengea mahoteli labda!

Imagine umedokoa billion 100 tu inaweza kuwalisha familia yako na ukoo mzima mpaka mkapukutika kama hamuifuji! Na still pesa mtaiacha! Yani imagine kila mtoto aingiziwe 10B tu anaweza ikamsomesha mpaka akaoa na kulea familia na still pesa anayo tu.

Mi najiuliza kwa haya maisha dah unaiba trilion nzima na bado huriziki wakati expectancy ni miaka 60 tu kibongo bongo😂
 
BARUA KWA RAIS SAMIA SULUHU KUHUSU UFISADI KWENYE SUKARI

11 December 2021


Mheshimiwa Rais nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ningependa badala ya kusema Kazi Iendelee basi uitikie haki, ustawi wa watu na uhuru wa kweli.
Mheshimiwa Rais nina mengi ya kukueleza kuhusu nchi yetu lakini leo ningependa kukueleza moja ambalo ni maombi yangu kwamba utalifanyia kazi ili kuitoa nchi yetu katika uchafu huu mkubwa. Jambo hili ni ulanguzi katika bei ya sukari na ufisadi mkubwa uliopo katika eneo la bidhaa muhimu (nipatapo wasaa nitakuandikia barua zaidi kuhusu bidhaa nyingine kama mafuta ya kula). Nakiri kwamba bei ya bidhaa hizi inachangiwa na mwenendo wa bei ya soko la dunia lakini pia inachangiwa na ufisadi uliopo katika soko la ndani.
Kwenye sukari tuna kundi dogo la wazalishaji nchini na hawa wana kikundi chao ambacho kisheria si sahihi (cartel). Kikundi hiki kiko chini ya Seif Ally Seif ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Superdoll (wamiliki wa Mtibwa na Kagera Sugar). Bei za sukari zinaweza kupandishwa kwa namna mbili, kwanza kwa kuamua kiasi gani cha sukari viwanda vya ndani vizalishe, maana yake hapa unaamua kiasi gani cha sukari kiwe kwenye maghala. Ukishaamua kiasi basi bei itapanda kuendana na kiasi. Maana yake ukiamua sukari uzalishe kidogo basi bei itapaa sababu bidhaa inakuwa chache na wahitaji ni wengi. Namna ya pili ni kushirikiana na watendaji walio serikalini kuhakikisha kwamba unapobana uzalishaji soko la ndani ili kuwe na uhaba na bei iwe juu basi serikali haitoi vibali kwa watu kuingiza sukari nchini sababu kwa kufanya hivyo uhaba hautakuwepo na bei unayotaka wewe itavurugika. Huo ndio mchezo unaochezwa Tanzania.
Ilikuwaje?
Mheshimiwa Rais zamani ilikuwa vibali kuagiza sukari nchini vinatolewa kwa kampuni yoyote inayofanya biashara ya vyakula na kukidhi vigezo lakini alipoingia madarakani Rais Magufuli kikundi hicho hapo juu kilimpotosha kwamba vibali vinauzwa kwa madalali (lengo likiwa wao wapewe nguvu hiyo ili waweze kuendelea kupangia wananchi wanyonge bei ya sukari). Bahati mbaya Rais Magufuli akakubaliana nao, akapitisha sheria kwamba atakayepewa kibali kuagiza sukari sharti awe mzalishaji wa sukari. Hapa Mheshimiwa Rais tukawa rasmi tumewapa kikundi hicho haramu nguvu zote mbili, ya kuamua kiasi gani wazalishe kwenye viwanda vya ndani na kiasi gani kiingie kutoka nje. Tukawa tumekamilisha lengo lao la kuamua bei ya sukari kwa wananchi badala ya soko kuamua. Kama si kundi hili haramu kuna uwezakano mkubwa sukari nchini isingezidi shilingi elfu mbili kwa kilo tofauti na ilivyo sasa.
Mchezo huu umechezwa kuanzia wakati wa Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli (yeye kaurasimisha kabisa) na sasa wanasubiri kuona kama na wewe utaucheza.
Nani wahusika? Wahusika kwa sasa wa mchezo huu ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda, Waziri Jenista Mhagama na nduguye kwa jina la Alex Mhagama.
Hapa chini Majaliwa anaongea uongo huku akijua fika nini kinaendelea.

Mheshimiwa Rais huu mchezo hauumizi wananchi tu kwenye bei ya sukari lakini umeleta madhila makubwa kwa wakulima wadogo wadogo wa miwa na wengi wamerudi kwenye umaskini mkubwa. Unapokuwa na kundi linakaa na kuamua bei ya sukari maana yake linaamua kiwango cha uzalishaji, kiwango cha miwa na hata bei ya miwa. Imefikia mahali Mheshimiwa Rais huyo Seif anawaambia wananchi hamna la kufanya zaidi ya kuuza miwa kwa nusu bei. Yako maelfu ya ajira yanapotea katika mchezo huu haramu.
Mheshimiwa Rais, wakati Kikwete anaondoka madarakani alijaribu kutaka kuinasua serikali toka kwa mdomo huo wa mamba wa kilanguzi. Ukaandikwa mpango wa kuwa na shamba na miwa na kiwanda cha sukari cha serikali chini ya NSSF kule Mkulanzi (shamba) na Mbigiri (kiwanda). Magufuli akaingia madarakani akataka kuuendeleza mpango huo mzuri ila akatekwa na genge hilo hapo juu la wauza sukari chini ya Seif (Seif alimtumia Mkapa kumweka sawa Magufuli, naamini unazo taarifa kwamba Mkapa alikuwa mmoja ya wamiliki wa Kagera Sugar). Pale Kyaka nako Magufuli na Seif wana hekta zaidi ya elfu 60 wametumia pesa za serikali kusafisha shamba, njia na mitambo walitaka kujenga shamba lao la miwa na kiwanda cha sukari. Baada ya Magufuli kufariki sijui mpango ukoje. Hii habari ni ya siku nyingine, turudi kwenye hili la sasa.
Hao mabwana wakamuhakikishia Magufuli kupata chake, naye akaingia tamaa. Kwa kuanzia Magufuli akamtoa Profesa Godius Kahyarara pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaama akamuweka NSSF akijua Kahyarara angekuwa mtu wa YES tu ili kuhakikisha hicho kiwanda cha sukari cha NSSF hakisimami. Bahati mbaya au nzuri Kahyarara alikuwa mtu makini, akausoma mchezo huo wa ufisadi wa kimafia kwa nchi kupitia sukari na akakusudia kuhakikisha kiwanda cha NSSF kinakamilika.
Kahyarara akatangaza tenda pale NSSF kwamba anataka mitambo ya kuzalisha sukari kwa ajili ya kiwanda cha sukari Mbigiri. Kikundi kile cha mafia wa sukari kikaona kitumbua chao kitaingia mchanga. Ile tenda ilishindaniwa na kampuni mbili moja toka India (Isgec Heavy Engineering Ltd) na nyingine toka Ethiopia. Kampuni ya Ethipoia ilipenyezwa na hao mafia wa sukari na sababu walikuwa tayari wako karibu na Magufuli wakashinda tenda ila Magufuli akaifuta mwishoni. Hakuishia tu kuifuta tenda lakini pia akamuondoa Kahyarara kwa aibu NSSF akamrudisha UDSM na badala yake pale NSSF akamuweka mtoto wa shemeji yake Mkapa, bwana William Erio (rudi nyuma unganisha kwamba Mkapa ni mmoja ya wamiliki wa Kagera Sugar, mnufaika wa ulanguzi wa sukari na godfather wa Magufuli).
Wakati wa sarakasi zote hizo za kutaka kujikwamua kwa kuwa na kiwanda cha sukari cha nchi yetu pesa bado inaingia shambani kule Mbigiri na wakulima wadogo wadogo wanaendelea kulima wakijua mashine zitakuja, miwa watauza na maisha yataboreka. Wastaafu nao wanajua pensheni zao ziko salama na shirika linazifanyia uwekezaji mzuri. Kumbe nyuma ya pazia hayo ndiyo yanaendelea. Sijamaliza Mheshimiwa Rais, naomba kuendelea. Zaidi ya shilingi bilioni 500 zimeingia kwenye kuandaa shamba Mkulazi, kulima na miundombinu shambani na kiwandani na hakujazalisha hata kilo moja ya sukari. Mheshimiwa hizi ni pesa za wastaafu. Leo hii kila ofisi ya NSSF malipo ni shida nadhani sasa wananchi wataanza kujua nini kinaendelea kwenye huo mfuko.
Baada ya Magufuli kufuta tenda ile akawaagiza TANROADS kuichukua tenda na kununua mashine zile za kiwanda cha sukari kwa niaba ya NSSF. TANROADS chini ya swahiba wake Magufuli, marehemu Mfugale wakachukua dola milioni 5 toka NSSF karibu bilioni 11 (ikabaki bilioni 169) wakaipa kampuni moja toka Malaysia inaitwa Kay Bouvet Engineering Ltd na hadi ninapokuandikia barua hii ndefu hakuna mashine iliyofika Tanzania. Narudia tena hizi ni pesa za wastaafu mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais hao Kay Bouvet wana wakala wao raia wa Sudan ambaye hapa chini naye ana wakala wake anaitwa Alex Mhagama (ndugu yake Waziri Jenista Mhagama).
Wakati mpango unaendelea wa kuchelewesha mashine na kuchezea hela za NSSF kama hivyo, Magufuli akafirki dunia. Haraka haraka Mfugale akatuma hela iliyobakia kwenda Malaysia, yani bilioni 169. Hayo malipo yalipata baraka za Waziri Mkuu Majaliwa na yeye alipewa shilingi bilioni 4.6.
Ulipoingia madarakani ninafahamu uliuliza mashine za kiwanda cha sukari cha NSSF Mbigiri kwa miwa ya shamba la Mkulanzi iko wapi na Majaliwa akasema ziko bandarini. Uongo mtupu Mheshimiwa na vyombo vyetu ya ulinzi na usalama vinajua naamini vitakupa mkeka wote.
Katika hizi sarakasi zote Mheshimiwa najua unajiuliza kina nani wanafaidika kwa kiasi kikubwa kwa maumivu ya bei kubwa ya sukari kwa wananchi? Katika ile bilioni 180 kuna watu wana pasenti zao ndani ya fedha hizo. Hapa Mheshimiwa ndipo nakuletea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri Jenista Mhagama, Profesa Adolf Mkenda (huyu aliona yaliyomtokea Kiharara akaona bora asalimu amri na yeye akinge bakuli) na Alex Mhagama (ndugu yake Jenista).
Mheshimiwa ulanguzi huu kwa wananchi ili kuneemesha kikundi kidogo ni dhambi kubwa. Ukichelewa watakuzunguka na kusema wewe ndiye unataka kutoa vibali huku wakificha ukweli kwamba vibali wanapeana wao kwa mkakati huku wakihodhi uzalishaji wa ndani na kuhakikisha bei ya sukari kwa mlaji wa mwisho inabaki kama wanavyotaka wao. Hii ni dhulma na dhambi kubwa sana. Bei ya sukari Tanzania inawapa faida zaidi ya asilimia mia moja, huu ni moto Mheshimiwa Rais mbele ya Allah kama ukiamua kulea mfumo huo.
Huko kote sijagusa kodi ambazo hicho kikundi cha mafia kinapewa nafuu na misamaha kwa kuwaweka hao watendaji mifukoni hadi bodi ya sukari. Tukiweza kusimamia vizuri sekta hii hapa nchini Mheshimiwa Rais utapata thawabu kubwa kwa mwenyezi Mungu lakini utaziba mianya ya dhulma na kupotea kwa kodi. Tanzania sekta ya sukari ingeweza kuleta faida ya zaidi ya dola milioni 200 kwa mwaka, yani tungeweza kujenga barabara hizi za lami Dar hadi Dodoma kila mwaka kwa pesa za ndani au kujaza madawa na wataalamu katika hospitali zetu bila shida yoyote. Ila kwa sasa wanakula wachache kwa machungu ya mamilioni ya watu kama hivyo.
Wakati mwingine nitakuandikia kuhusu Mbowe, ndege, mafuta ya kula, dizeli, petroli, mafuta ya taa, bwawa la Mwalimu Nyerere, na kadhalika. Nakuombea kheri nyingi uweze kuitoa nchi yetu katika makucha haya.

Mchambuzi zaidi ya habari
www.umeandika kirefu Sana kuonesha uyaandikayo unayafahamu. Tunaomba utuwekee ushahidi usioacha shaka yeyote ili twende sawa
 
mateso mnayoyapata wastaafu yanasababishwa na hawa viongozi vibaka, poleni wastaafu wa NSSF na watanzania kwa ujumla
 
Bagamoyo sugar nadhani Magufuli ana share kubwa sana.
 
sijajua Majaliwa anapata wapi guts za kuwaita watu wezi na kuwafukuza kazi.Mungu anakuona Majaliwa
 
Mama umefika wakati kumtimua Majaliwa ukweli unaosasa kama tiss alikuambia hukuamini sasa umesikia source ingine.....Kazi kwako achana na udini huyo kitu get muweke Makamba PM na Waziri Nishati hapo hapo....IGP amechoka na Mabeyo umri unaenda sasa 65 imetosha
 
Hujamuelewa mleta uzi. Ni kuwa yeye mleta uzi katumwa na genge la wezi na mafisadi. Prof. Mkenda alifafanua vizuri sana. Nyie mafisadi hamuwezi kutudanganya hata iweje. Dkt Magufuli alikuwa mzalendo alifanya vitu vyenye tija na faida kwa taifa. Acheni uhuni wa kutunga. Maana unaposema eti wanaamua wazalishe kiasi gani wakati waziri aliwahi kusema na inajulikana capacity ya viwanda vyetu ni ndogo. Halafu mnavyotaka vibali vitolewe ili mlete na sukari oliyo isha muda ili watanzania wafe??? Kipindi cha JK watu walikula bidhaa za ovyo ovyo cheki watu wanavyokufa na cancer. Kwa ufupi huo mlango wa ufisadi hautafunguliwa!
we ngdere bdio haueleweki au umetumwa na hao mafisadi au unahusika. Uzi uko very clear
 
Sisi wananchi tuliichagua CCM ili ituongoze kumbe kuna mambo machafu sana yanayotendwa na Watendaji wake. Hapa Mwanza bei ya sukari ni Tshs.3,000. Mungu isaidie nchi hii inaelekea pabaya.
 


Ziara ya NSSF na Magereza kwenda kujifunza kwa Bakhresa ni ubia wa watu wawili hiko kiwanda; tofauti na porojo tunazotaka kulishwa.

Binafsi naamini serikalini kuna wazalendo wengi sana wenye nia njema ya kulisaidia taifa. Wanachohitaji ni kiongozi mwenye maono kama yao vinginevyo ukiingia kichwa mwenyewe utapotea kihasara hasara bure tu; kilichobaki unaangalia misimamo ya raisi ukiona yupo kama mama na wewe iba yaishe kuliko kiherehere.

Ata huyo Magufuli alikuwa na ushamba fulani kama kuwasaidia wazalendo serikalini ni kwa asilimia ambazo azifiki za juu kabisa. Walau he did something na alikuwa anasoma mafaili waliyokuwa wanampelekea na kushaurika maeneo kadhaa.

Hii nchi imejaa mijizi japo siungi mkono NSSF kuingia kwenye sukari (simply they don’t have the know to run such a business) lakini Magufuli hana mkono ni kihehere chao. Na NSSF awapo kwenye sukari kipindi hiko hiko cha Magufuli waliingia kwenye ubia wa kuzalisha mafuta ya kupikia (god knows what other production industry they’re involved in) na kwenye sukari wanaenda jenga kwa ubia na Magereza awapo pekee yao.

Mtu anakuja anaandika ujinga mtupu what would you call that, other than nonsense.


..na TANROADS kuhusika ktk ununuzi wa mitano ya kiwanda imekuwaje?

..kuna dokoment inayohusu manunuzi ya mitambo ya sukari ililetwa JF ina saini za wakubwa wa Tanroads.
 
Mwambie huyo mchambuzi alete ushahidi wa maelezo yake. Mbona Hutaki Unaacha alikuwa anatupa hata na account namba za benki pesa zilipopita, siku hata saa na nani alipokea hizo fedha!? Watu watoe tuhuma kwa ushahidi usiotiliwa shaka. Vinginevyo, huku ni kuchafuana kwa maslahi binafsi.
Katafute na wewe ushahidi wako utuwekee humu acha kusumbua watu..
Mwenye macho haambiwi soma
Nani asiyejua nchi inavyoibiwa miaka nenda rudi cha kukushangaza hapa ni nini eti weka ushahidi?
 
..na TANROADS kuhusika ktk ununuzi wa mitano ya kiwanda imekuwaje?

..kuna dokoment inayohusu manunuzi ya mitambo ya sukari ililetwa JF ina saini za wakubwa wa Tanroads.
1639335449289.png

1639335481150.png
 
Ukisoma andiko hili kisha ukaenda site kuona yanayoendelea kuna vitu utagundua haviko sawa. Kwa tuliobahatika kufika Dakawa,tumeshuhudia ujenzi wa kiwanda ukiendelea. Gharama zote za mradi inasemekana hazizidi 250billions. Hizo billion 500 zinazotajwa na mwandishi zinatoka wapi??
 
Katafute na wewe ushahidi wako utuwekee humu acha kusumbua watu..
Mwenye macho haambiwi soma
Nani asiyejua nchi inavyoibiwa miaka nenda rudi cha kukushangaza hapa ni nini eti weka ushahidi?
Pole, Mkuu.
 
Back
Top Bottom