Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Hujamuelewa mleta uzi. Ni kuwa yeye mleta uzi katumwa na genge la wezi na mafisadi. Prof. Mkenda alifafanua vizuri sana. Nyie mafisadi hamuwezi kutudanganya hata iweje. Dkt Magufuli alikuwa mzalendo alifanya vitu vyenye tija na faida kwa taifa. Acheni uhuni wa kutunga. Maana unaposema eti wanaamua wazalishe kiasi gani wakati waziri aliwahi kusema na inajulikana capacity ya viwanda vyetu ni ndogo. Halafu mnavyotaka vibali vitolewe ili mlete na sukari oliyo isha muda ili watanzania wafe??? Kipindi cha JK watu walikula bidhaa za ovyo ovyo cheki watu wanavyokufa na cancer. Kwa ufupi huo mlango wa ufisadi hautafunguliwa!
Nonsense! Kwa sauti ya SSH.
 
Hukuandikiwa wewe, ameandikiwa Rais SSH. Rais ana vyombo vyake vya uchunguzi. Watachunguza ili kupata huo ushahidi. Usitake kuleta ushuzi wako hapa
Rais ni wa kwetu wote. Sote tunataka Rais afanye kazi kwa wepesi tena yeye anafanya kazi muhimu tu kwa taifa.

Kama una nia njema na nchi hii huna budi kumsaidia Rais kwa kuhakikisha ni kazi tu halisi na zenye manufaa zinamfikia Rais tena zikiwa kwenye package nzuri.

Ninachokifanya ni kujitahidi na kuhakikisha anapelekewa kazi muhimu kwa taifa zikiwa Zimekamilika (kwa case hii zikiwa na ushahidi) na ziko kwenye Package nzuri(kwa case hii zikiwa na maneno yasiyo a kashfa na fitina).

Nakushauri uniunge mkono tumrahisishie kazi Rais wetu Mpendwa, Mama Samia.

Karibu.
 
Huyu jamaa ni moja ya wahuni. Kaandika majungu. Yaani ungejua tangu mwanzo wa mradi na serikali ilivyokuwa makini kuhakikisha haiibiwi.
Kitumbua cha legacy kimeingia mchanga. Mtajua hamjui.
 
Mafisadi wa sukari mnatumia nguvu sana kufanya biashara ya sukari iwe holela.Sukari ni usalama wa taifa brother huwezi kuwaachia wahuni...huko nyuma wafanyabiashara walipokuwa na ruhusa ya kuingiza sukari bei ilikuwa haipandi?mbinu mnazotumia kuhakikisha bei inapanda iii serikali irejeshe mfumo wa zamani mpige hela.Bakhresa anamalizia kujenga kiwanda cha sukari baada ya kupewa kiwanja bure na serikali haya tuone mapambano yenu mtafikia wapi.
 
Nenda Dakawa utaziona na inasemekana kiwanda kitaanza kazi Augost 2022 na shamba zaidi ya 2800ha limeshalimwa na kupandwa miwa.
Hivi Kuna mtu kweli anaweza kukomaa kuandika uongo mwingi hivi? Basi Kuna shida mahali vichwani. Unaanzaje kuandika tuhuma kubwa hivi za uongo na ukaacha kufanya kazi kama kweli unalipenda taifa letu?
 
Heeeh! Nakumbuka kuja Jamaa nilikuwa nasoma nae advance, alisema alisema magufuli ni moja ya matajiri wa kutupwa hapa nchi. Ana miradi ya kufa mtu huko Kanda ya kwao. Lakini kwa kuwa sisi ni sikio la kufa wahalaaaa hatusikiii
 
Hojazake zimejichanganya changanya ukimsoma vizuri utaona amejikita kumchafua Marehemu tu.

Kama akiliyako imechangamka kidogo huwezi hata kumaliza kusoma uziwakemrefu kabla hujajua lengolake.
Ameunganisha unganisha uovuwa watuwengine ilikupata mtaji wa kustabilize malengoyake.
Shida ni kuna watu wanapenda kusikia kile wanachopenda. So hapo usitegemee mtu atulize kichwa
 
..nafahamu.

..MAJIZI huwa yamejipanga kwenye taasisi inayokaimishwa kufanya manunuzi.
Ni sahihi lakini tumeona nyaraka ya mkataba kwenye twitter ya Zito,mkataba umesainiwa mwishoni mwa 2019,gharama nzima ya ujenzi wa kiwanda mpaka kukabidhi bila kuhusisha mashamba si zaidi ya 130billions lakini mwandishi anadanganya kuwa zaidi ya 500bilions zimetumika. Taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizotumika mpaka June 2021 hazizidi 85billions,hizo 500bilions anazosema zimeibwa zinatoka wapi???
 
Wakati mwingine nitakuandikia kuhusu Mbowe, ndege, mafuta ya kula, dizeli, petroli, mafuta ya taa, bwawa la Mwalimu Nyerere, na kadhalika. Nakuombea kheri nyingi uweze kuitoa nchi yetu katika makucha haya.
Hakika nitakusoma nitakapopata nafasi ya kukusoma; lakini nimeuona huu mstari mwisho wa bandiko lako, nikajuwa umekwishafeli mkuu!

Sasa sijui kama utanielewa nina maanisha nini!

Hata hivyo, najuwa huu siyo mwandiko wa mkuu 'Missile', naona leo kaamua kukodisha jina.
 
Dah umechambua vizuri ingawa umeeleza mambo yote katika pumzi moja. Uko vizuri, hususani ulipotaja uhusika wa Majaliwa kwenye huo utapeli. Ishu ni kwa bi mkubwa, anao uwezo wa kupeleka kamera eneo la tukio ili aruke nao live??
 
Atakayepata nafasi apitie pia bandarini ajionee ni makontena mangapi ya mitambo ya kiwanda imeshafika mpaka sasa kwa jina la Mkulazi Holding Company Limited au aende Dakawa akajionee ujenzi unavyoendelea kwa kasi
 
Ni sahihi lakini tumeona nyaraka ya mkataba kwenye twitter ya Zito,mkataba umesainiwa mwishoni mwa 2019,gharama nzima ya ujenzi wa kiwanda mpaka kukabidhi bila kuhusisha mashamba si zaidi ya 130billions lakini mwandishi anadanganya kuwa zaidi ya 500bilions zimetumika. Taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizotumika mpaka June 2021 hazizidi 85billions,hizo 500bilions anazosema zimeibwa zinatoka wapi???

..labda ungeweka vielelezo / dokoment kuthibitisha gharama unazozisema.

..halafu ukamdai mtoa tuhuma naye aweke ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

..Je, nikisema wewe uko ktk kundi lilitofichuliwa na whistleblower nitakuwa nimekosea?
 
Fuatilieni hotuba ya Prof. Mkenda. Kilichopo ni capacity ya viwanda ni ndogo.
Miaka na miaka kuna ugumu gani wa kuongeza uwezo wa uzalishaji? Badala yake wamebaki kuzalisha kidogo na kuagiza kingi. Ndiyo cartel anayoongela mleta mada. Huku wakulima wadogo wakidodewa na miwa yao. Kisa? Uwezo mdogo wa kiwanda. Shenzi.
 
..labda ungeweka vielelezo / dokoment kuthibitisha gharama unazozisema.

..halafu ukamdai mtoa tuhuma naye aweke ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

..Je, nikisema wewe uko ktk kundi lilitofichuliwa na whistleblower nitakuwa nimekosea?
Mimi ni raia huru,taarifa ziko wazi,tafuta ziara ya Waziri Mkuu Mradi wa Sukari Mkulazi Augost 2021 utapata picha halisi ya mradi
 
Sijawahi wala sitakaa nimfikirie Majaliwa kama mtu mwema kwa hili Taifa na watu wake. Mungu anisamehe ila namuona Majaliwa kama mtu mwenye roho mbaya, mnafiki, mzandiki na mwenye tamaa. Hajawahi kuwa mkweli kwa Taifa. Hata sasa namuona ndie masta mind wa anguko la Mama. Ana jionyesha kwake kama mtu mwema lakini hafai. Muda utaongea. Nani alijua yeye na Jenister ndio wako nyuma ya sakata la sukari? Bado ikija ya mafuta ya kula na mafuta ya gari utamkuta Majaliwa.
Tulimpigia Mama kelele aanze na safu yake akaona watu wana mfundisha kazi. Akabeba uchafu wa mwenda kuzimu. Sasa wazimu una mkuta. Amebaki kusema hato kubali wakati amesha kubali. Hata madudu yaliyopo bandarini ukifuatilia mkono wa Majaliwa upo. Makesi ya hovyo mahakamani Majaliwa yupo.. Say all evils lazima yupo..
EeeenHeeeee! Umemchambua toka utosini hadi kwenye unyayo.

Kiongozi mwenye uthubutu wa kusema "Rais yupo ofisini anachapa kazi", huku akijuwa kiongozi huyo tayari ni maiti, mtu wa aina hiyo siyo wa kawaida hata kidogo.
 
..na TANROADS kuhusika ktk ununuzi wa mitano ya kiwanda imekuwaje?

..kuna dokoment inayohusu manunuzi ya mitambo ya sukari ililetwa JF ina saini za wakubwa wa Tanroads.
Leta kwanza ushahidi wa hiyo documents; I don’t subscribe to hearsay.
 
Back
Top Bottom