Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Ukiomba mleta mada alete ushahidi, unaonekana mnaa!!!
 
Hii habari haitashughulikiwa kwasababu wewe mleta habari hujajitambulisha ni nani, isitoshe wahusika katika kashfa hiyo wamo watu wazito (wana CCM)----kama ilivyo ada wana CCM ni mahodari sana kulindana katika maovu.

Njia bora ni kuing'oa madarakani CCM tu.
 
Hivi mjinga huwa anjijua?
 
..na TANROADS kuhusika ktk ununuzi wa mitano ya kiwanda imekuwaje?

..kuna dokoment inayohusu manunuzi ya mitambo ya sukari ililetwa JF ina saini za wakubwa wa Tanroads.
Taasisi zinaruhusiwa kukaimisha manunuzi kwa taasisi nyingine
 
Mzalendo umetisha sana hongera na Mungu akubariki
Kweli katisha ila Mungu ni Mungu hakuna wa kufanana nae, Sasa ona mfugale kakwapua hela za wastaafu kabla hajazila kastaafishwa maisha ma Mungu.
Majaliwa hizo 4.6 bil zitamtokea puani maana wazee wastaafu machozi yao hayaendi bure.
 
Ko huyu Majaliwa pia mpigaji ...ukute mtoa post pia kapigia kura CCM
 
Ukiomba mleta mada alete ushahidi, unaonekana mnaa!!!
Mwandishi wa hii habari hana uzoefu au taarifa sahihi za miradi ya sukari. Kujenga kiwanda cha sukari 2500TCD si chini ya miaka mitatu na ndo maana Bahresa alianza pamoja na NSSSF na mpaka leo kiwanda chake hakijakamilika wakati kiwanda chake ni 1500TCD tu. Pia hakuna faida ya dollar 200m kwenye sukari,TPC Limited wanaozalisha tani laki moja za sukari na wako vizuri sana kwenye management yake wanapata si zaidi ya 60bilions
 
Kwani wewe umeona hizo mashine za hicho kiwanda? Au wewe ni mmoja wao?
Nenda Dakawa utaziona na inasemekana kiwanda kitaanza kazi Augost 2022 na shamba zaidi ya 2800ha limeshalimwa na kupandwa miwa.
 
Kweli katisha ila Mungu ni Mungu hakuna wa kufanana nae, Sasa ona mfugale kakwapua hela za wastaafu kabla hajazila kastaafishwa maisha ma Mungu.
Majaliwa hizo 4.6 bil zitamtokea puani maana wazee wastaafu machozi yao hayaendi bure.
Sidhani kama kuna ukweli katika hili
 
Hitler hakuwa mlafi kama CCM, yeye alipigania maslahi ya taifa lake, alitamani taifa lake liwe giant kwenye uso wa Dunia, CCM wanachota kupitiliza , imagine mtu mmoja anachota billions hela walizokamua wavuja jasho bila huruma
 
Mifumo mibaya huwabadili wema kuwa wabaya, where is the greatest African author who wrote " The beautiful ones are not yet born!" ?
 
kwa hiyo watu wakae watunge uwongo halafu serikali utumie gharama ambazo zingesaidia Miradi ya maendeleo Ndiyo aziamishe kwenye mambo yakutunga! Atoe ushahidi usiotiliwa mashaka!
Hivi, unataka ushahidi wa aina Gani Kama mleta hoja kawataja wahusika Kwa majina Yao yote, majina ya makampuni, miradi husika, kiasi Cha fedha kilicholipwa na eneo la mradi husika! Au unataka ushahidi wa mavazi na hoteli walikosainia mikataba?
Itoshe kuelewa kuwa rais ambaye ameelekezwa kuchukua hatua Hana haha ya kuhamisha fedha za miradi mingine kutekeleza uchunguzi Bali ana mfuko wa rais ambayo ni mahsusi Kwa task force!
Halafu mwamba unatanua mno mishipa ya shingo kupingana na mpuliza kipenga kana kwamba wewe unao ushahidi wa kuwa tuhuma hizo ni za kutunga, mwache aliyeekekezwa aamue mwenyewe kufanyia kazi au kuzina macho wahusika waendelee kula!
 
Hebu tuambie ni kwa nini upigaji wote unafanywa na wana CCM? kila siku,kila mwezi kila mwaka ni CCM tu why?
 
Hukuandikiwa wewe, ameandikiwa Rais SSH. Rais ana vyombo vyake vya uchunguzi. Watachunguza ili kupata huo ushahidi. Usitake kuleta ushuzi wako hapa
 
Kazi sana, tukiweka sheria ya kunyongwa/kupigwa risasi kwa ukweli ukibainika juu ya mtenda makosa, basi ndani ya miaka mitatu Taifa litaanza kuigwa na kufuata maadili na sio kuimba na kuhubiri amani
Hii ndiyo ilifanya wachina wakaendelea hapa tutakuwa tunapiga dana dana tu. Tanzania tuna shida kubwa kwa kweli. Sijui hatima ya hii nchi yetu nzuri.
 
Mkuu, ili kuboresha mjadala naomba urejee post yangu ya kwanza ya uzi huu ambayo hasa ndiyo ilisababisha nimjibu mwanaJF kwa bandiko langu ulilo nukuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…