Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Sema Majaliwa ni mkurupukaji sana.sijui ni kwa sababu gani.yaani naweza kuamini kwamba hizi tuhuma zinamhusu.maana toka ameanza kuunda tume hakuna iliyowahi kuleta mrejesho.Ananyamazishaga watu kwa kuwambia anaunda tume ichunguze
Kifupi hakuna jambo lolote tangible alishawahi fanikisha kama waziri mkuu. Yupo yupo tu as long as mambo yake yanamwendea.
 
Utakapoandika hayo mengine ukumbuke pia kuwa unayemwandikia ni Mwana CCM...anayajua nje ndani ila sijasema anaweza kuwa pia sehemu yake
Hata sielewi mwandishi anapata wapi ufahamu na uhakika wa kujuwa kwamba anayemwandikia ni tofauti na hao anaoandika juu yao!

Mwandishi anajuaje kwamba anayemwandikia siyo sehemu ya mpango mzima anaounanga?

Kama Magufuli, na hasa Mkapa kawahusisha kwenye mipango hiyo, ni kipi hasa kinachomtofautisha Samia kiasi kwamba mwandishi aamini kuwa yeye yupo tofauti?

Majaliwa, Jenister, na wengine wafanye anayoyasema mwandishi, huyo anayemwandikia asiwe hata na chembe ya taarifa yoyote juu yao?

Wakati sukari ya Uganda imekataliwa Kenya mara kadhaa kwa kujuwa kwamba ni sukari inayotoka nje ya nchi hiyo, Samia yeye bila shaka yoyote kaikubali..., na hana shaka nayo na wala hana haja ya kusisitiza uzalishaji wa ndani ya nchi! Hapo kuna matumaini kweli?
 
Leta bandiko lako la ukweli tulione.
 
Umeandika kwa urefu ila umeharibu tu pale ulipomtaja :MAGUFULI' hapo umedhihirisha uongo wako ma conspiracy theory zako.Hakuna asiyefahamu kwamba Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli asiyeyumbishwa na mafisadi.Haya bhn kwa hiyo hizo Trilion alizopiga alipeleka wapi? Mbona maisha yake ya kawaida tu
 
Kesi ya Ngedere anapelekewa nyani, Ila sijui kwa nini namuamini sana mama kweli yeye ni mnyenyekevu Ila kazungukwa na majenerali wa ufisadi na Hivi vitu ndivyo vya kujadiliwa

Je inawezekana ile " NONSENSE" aliyoitoa mama kwa waziri wa Kilimo ilikuwa baada ya kupata taarifa hizi?
 

Haya makundi mawili ya ccm yanagombania ulaji na hapo kazi ya Mama Samia ndio itakapokuwa ngumu kwani genge zote mbili anazikumbatia!!!
Ukweli ni kwamba Majaliwa na Jenista Mhagama sio wasaidizi wa kuwategemea na hilo JIWE alikwisha liona na ndio maana alimwambia Majaliwa kuwa asidhani angekuwa waziri mkuu kwa miaka kumi!!! Samia alikuwepo kwenye huo mkutano JIWE alipomuwashia Majaliwa taa nyekundu!!!
 
Haya makundi mawili ya ccm yanagombania ulaji na hapo kazi ya Mama Samia ndio itakapokuwa ngumu kwani genge zote mvili anazikumbatia!!!
Bora aangalia less evil, maana wamsogo hawafai bora kukumbatia waadilifu
 
Hata kama kuna 'gaps' katika stori hii, lakini 'core' ya stori ni sahihi. Kama ningekuwa rais at least ningepata 'second source' na siyo kuiacha tu kisa kuna majina makubwa yaliyotajwa.
 
Bora aangalia less evil, maana wamsogo hawafai bora kukumbatia waadilifu

Sasa hao unaosema hawafai ndio washauri wake wakuu nje na ndani ya serikali!!! Salama yake ni kufuata ushauri kutoka busara zilizobaki chamani MZEE MANGULLA.
 
Hahhahahahah
Ndio mkataba unavyosema mkandarasi afanye design na kujenga kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha tonne 250 za sukari kwa siku (na kiwanda kidogo as far as sugar plants are concerned) lakini hakuna sehemu ya ununuzi wa mashine.

Ni ujenzi wa Kiwanda cha sukari; sasa TANROADS anaweza kapewa kazi ya usimamizi tu.
 
Hii ndiyo ile wanasema nyama hatari akishaonja damu ndiyo basi tena, ataua sababu anaweza lakini mizoga ataiacha hamalizi.
 
Umetumwa. Sema mzee wa deal kakuvutia ngapi
 
Sijasoma lugha lakini kiwanda kina mkusanyiko wa mashine mbalimbali zitakazochakata malighafi ili kupata zao/product inayotakiwa
 
Hata kama kuna 'gaps' katika stori hii, lakini 'core' ya stori ni sahihi. Kama ningekuwa rais at least ningepata 'second source' na siyo kuiacha tu kisa kuna majina makubwa yaliyotajwa.
Ni sahihi usemacho,shida katika uagizaji wa sukari ipo lakini tunachobishania ni gharama na uwepo wa ujenzi wa kiwanda
 
Inasemekana tatizo la kuhujumu uanzishaji wa viwanda vya sukari nchini ndo ulipelekea taasisi nunuzi kukaimisha ununuzi wa kiwanda kwa tanroad na ni kundi dogo sana la watu walijua hii kitu vinginevyo hakuna kiwanda ambacho kingejengwa
 
Sijasoma lugha lakini kiwanda kina mkusanyiko wa mashine mbalimbali zitakazochakata malighafi ili kupata zao/product inayotakiwa
Nimepitia tena posts number 1 naona mwandishi anachanganya mambo.

Kwanza serikalini consultant na Civil engineer awezi kuwa mtu mmoja; so inaonekana Tanroads kapewa tender ya kusimamia huo ujenzi wa kiwanda cha NSSF na yeye katafuta contractor wakufanya hiyo kazi; it is all part of Tanzania Gov requirement on infrastructure projects.

Lakini hakuna mahala huo mkataba unasema TANROADS wanunue machine, if anything contractor ndio anaweza propose mashine gani itafaa based on his design ya kiwanda na capacity waliyopewa.

Mbona kila kitu kiko wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…