Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Whistleblower: Kashfa nzito suala la sukari, wamo vigogo wazito

Tatizo njia mnayotumia siyo sahihi. Mama ndiye rais na ndiye mpeperusha bendera wetu wa 2025, ila nyie mnafanya kila mbinu kuhakikisha mnamfitinisha na wapiga kura. Mnatunga uongo mwingi wa ufisadi ili awamu ya 5 ionekane ilikuwa fisadi ili mje kusema Mama alikuwa sehemu ya ufisadi hafai. Kikubwa tumewastukia lazima Mama na Dkt Magufuli tuwatetee kwa nguvu zetu zote. Awamu ya 5 ilikuwa ni serikali ya kizalendo sana
wahuni ndio wanamfitinisha huko ccm sisi yetu kushangilia tu.
 
Ukishakuwa mpigaji unakosa guts za kuwatia hatiani wengine, sababu utahofia nawe madhambi yako yatawekwa hadharani...

CCM kuna madudu sana mkuu...
Ndio maana hawawezi kurekebisha matatizo. Kila mtu ana yake.
 
wahuni ndio wanamfitinisha huko ccm sisi yetu kushangilia tu.
Huku kwetu CCM tupo makini na wahuni. Wanajitahidi sana, maana mpaka sasa Mama alikuwa hajastuka, ila kaanza kuusoma mchezo. Kikubwa Mama ni mtu muadilifu sana tena sana hata Mzee JK ni waadilifu tatizo ni ushikaji tu. Dkt Magufuli hakuwa na urafiki linapokuja mambo ya kitaifa.
 
Huyu jamaa katunga uongo na ni mnafiki kabisa. Mh. Majaliwa ni muadilifu sana na Mama Samia ni muadilifu sana. Mleta habari lengo lake ni kuichafua serikali ya Mama Samia. Akikubali tu watabadili gia, mtoto akikunyea mkononu unajisafisha hukati mkono, ila watasema Mama nayeye alikuwa sehemu ya uovu hivyo hafai na yeye ni mwizi. Yaani Mama ajue genge analohusika nalo la Msoga ni hatari sana tena sana. Arejee Salim Ahmad Salim walivyomtungia mpaka kitabu na wakamuita mhizbu na walienda zenj kuzindua kitabu cha kumdhalilisha. Mama achana na akina Makamba na Nape ni wahuni. Mipango yao ni noma, juzi kati hapa wamemnyamazisha msukuma kwa kumpatia PhD fake, sasa msukuma hawezi kujipambanua tena maana kila akiropoka watasema PhD fake. Hahahah
Halafu ameandika:
Magufuli akafirki dunia. Haraka haraka Mfugale akatuma hela iliyobakia kwenda Malaysia, yani bilioni 169. Hayo malipo yalipata baraka za Waziri Mkuu Majaliwa na yeye alipewa shilingi bilioni 4.6.
Yeye anadhani malipo ya bilioni 169 ni kama kwenda kulipia soda kwenye duka la Mangi! Process ni ndefu na Mama Samia angeweza kuisimamisha kama alivyoomba uchunguzi wa Benki Kuu!
Haache kumchafua Mama na wengine!
 
Wewe jamaa ni liongo na linafiki. Yaani ktk kujiita mnyetishaji ni muongo kabisa. Huo mradi kwanza ulikwama kwa sababu kuna watu walileta feasibility study ya kubumba na ya kifisadi serikali ikaamua kufumua na kufanya upya. Na hiyo ndiyo sababu ya prof kuondolewa kwa sababu alitoa kazi ya kuandaa plan kishikaji na hao ma prof wa udsm walijifungia ndani na kuandika andiko. So ujue serikali ya Dkt Magufuli ilikuwa makini sana. Acha kupotosha. Huu ujinga wako ni wakitoto sana, kila ulichoandika ni cha kutunga na ni uongo. Nimepuka tu hint kidogo ya kilichoanza mi najua mpaka mwisho wewe muhuni muhuni usipotoshe. Mnataka Mama kumjaza uongo ili afanye kama kwenye mkataba wa meli, wahuni nyie.
Wewe ndio muongo na mpotoshaji..ulikua wapi kusema haya mwanzoni..baada ya kuona wizi wenu uaanikwa ndio unakuja na utetezi wa kipumbafu..haya mambo peleka huko fbk sio Jf huku watu wanajielewa na wanajua kuhoji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Halafu ameandika:

Yeye anadhani malipo ya bilioni 169 ni kama kwenda kulipia soda kwenye duka la Mangi! Process ni ndefu na Mama Samia angeweza kuisimamisha kama alivyoomba uchunguzi wa Benki Kuu!!
Hapo hajazungumzia process za malipo. Amesema malipo yalifanyika.
 
Tatizo Samia naye ni sehemu na zao la ufisadi, yuko mikononi mwa mafisadi na ananufaika nao. Dawa pekee ingekuwa ni katiba ya wananchi lakini mafisadi wanajua katiba hiyo itawaumiza, hawako tayari kuona inapatikana. CCM tulishambiwa kuwa ni ukoo wa panya
 
Nanukuu: "Hao mabwana wakamuhakikishia Magufuli kupata chake, naye akaingia tamaa"😁😁😁

Alieandika hii barua ni punguani kwa sababu hadi yeye ambae ni kapuku anapata taarifa hizi maana yake ni kwamba Rais wa nchi ambae ana intelijensia ya hali ya juu tayari ana taarifa hizi.

Rais anayajua yote haya ila anakula kimya kwa manufaa yake.Either na yeye anapata chake cha juu au anakaa kimya kulinda urais wake ambao hauna kibali cha wananchi.

Mwandika barua ungekuwa na akili badala ya kumwandikia Rais barua hii ulipaswa utuandikie sisi wananchi hii barua ambao ndiyo wenye nchi kisha utushauri kuwa tuiondoe CCM madarakani kwa nguvu kwa kuwa CCM ni mafisadi.Ungefanya haya ungekuwa na akili.
 
Kama wanaamini siku ya mwisho na iwe hivyo
Ila kama wote wamo katika ufisadi huu tutajua mbele

Umewataja mpaka waliotangulia (wafu) sasa je unafikiri Mama hajui haya?

Hapo kuna Seif, Mama na PM wote waislam na Ramadhan imebaki miezi kadhaa
Tutaona kama hii sukari itashuka au ndio wataendeleza kutengeneza hela za HARAM huku wakiwa wamefunga mwezi mtukufu

Subhanaa Allah eee Mwenyezi Mungu tupe Imani Thabit
Tamaa mbele mauti nyuma mlikumbuke hili kuwa hela ni mapambo tu

Kama tuhuma ni za kweli basi mbele ya Mungu hata mama haponi
Dini Ni mwamvuli wa kuwatia Moyo masikini
 
Dini Ni mwamvuli wa kuwatia Moyo masikini

Kama huamini ni wewe ila bila dini naona tungekuwa kama wanyama kabisa

Dini ni imani ila wengi wanaikimbia na kufuata mengine
Ni maamuzi yako kufanya mema au mabaya
Umasikini hauhusiani na unachoamini

Umasikini sio wa kuomba bali kuukemea na pia tunasema eeh Mungu tuepushe na umasikini
 
Back
Top Bottom