Who am I / Mimi ni nani?

Who am I / Mimi ni nani?

Tahadhari! Mwandishi wa Uzi huu amejikuta anajiuliza yeye Ni Nani baada ya subconscious mind kuleta kumbukumbu kadhaa katika Maisha yake, kwahiyo anawaza Kwa sauti kubwa!!!

Nikiwa shule ya msingi nadhan Darasa la tano au la sita, wanafunzi wenzangu waliniambia huwa wanamuona Baba yangu kwa binti mmoja hivi, ingawa mpaka sasa hivi ninavyoandika ni mama yangu mdogo kwa maana aliolewa mke wa pili na Baba. Kwa umri ule ingetarajiwa ningeenda straight kumwambia mama au mtu mwingine yoyote Yule lakini sikufanya hivyo kabisa na hii Siri ndio naitoa Leo

Najikuta najiuliza WHO AM I

Kuna kipindi miaka ya 2003/4 nilienda na girlfriend wangu club, akaniaga anaenda washroom, akachukua Mda kidogo kurudi nikasema ngoja nitembee kidogo pale ukumbini,dah nikamuona ameshikwa makalio na mwamba kama wanakiss hivi. Nikapita kimya hakuniona, sikumuuliza chochote na tuliendelea Kula gudtime, nilikuja kumwambia siku nyingine kabisa, akabaki anajikanyaga Tu.

Najiuliza WHO AM I

Kuna kipindi nilikuwa na kirukuu / suzuk carry, nikampa jamaa mmoja aniletee hesabu,kumbe nae anatoa deiwaka bwana, aliyepewa deiwaka akapata ajali na alikuwa hajui gari vizur, nikaingia gharama na hasara Kwa matengenezo, huwezi amini jamaa hakuwahi kuomba msamaha hata kidogo, hakuonyesha kusikitika hata Kwa kinafiki, ni jamaa kutoka ilikodondoka Ile ndege hivi majuzi, nikajua huenda ni hulka zao, sikusema chochote wala kulalamika Kwa yeye kutoomba msamaha.

Najiuliza WHO AM I

Unaweza kunitukana au kunitamkia maneno ya hovyo hovyo nikakuangalia Tu na kujifanya kama hakuna kitu kilichotokea, na siweki kinyongo Rohoni

Najiuliza WHO AM I

Nahisi hata kama siku ikija kutokea Nikamfumania mama watoto wangu ingawa sipendi wala kufikiria kuja kutokea, sitarusha ngumi au kuleta fujo kwa yeyote yule isipokuwa kumpa talaka Tu Kwa roho Safi.

Najiuliza WHO AM I

Natambua kuna baadhi ya watu baada ya kusoma Uzi huu watakuja na comment za kejeli na matusi na Maneno ya ovyo ovyo lakini sitawajibu chochote kile na wala sitakwazika.

Najiuliza WHO AM I

Kutoka kwangu ETUGRUL BEY

Ni hayo Tu!
Hongera sana
Natamani nipate uwezo kama huo maana ikitokea tafrani yoyote aisee nakuwa mbogo mpaka badae najishangaa kama ni mimi
 
Unaishi maisha mazuri sana.Ambayo napenda kuyaishi.
ni kutokuwa na matarajio makubwa kuelekea wengine. hii inasaidia hata return inapokuwa tofauti kutokujali.

Ukiishi hivi unakuwa na amani sana.
Kweli mkuu

Na huwa mara nyingi nakuwa na Amani kwasababu nayapokea mambo kama yalivyo huwa sijiulizi sana KWANINI IMEKEKUWA HIVI, WHY ME NA MAMBO KAMA HAYO
 
Unatafuta huruma kwa wananchi
 
Kweli mkuu

Na huwa mara nyingi nakuwa na Amani kwasababu nayapokea mambo kama yalivyo huwa sijiulizi sana KWANINI IMEKEKUWA HIVI, WHY ME NA MAMBO KAMA HAYO
Ukiwa hivi inakuwa ngumu sana kuumizwa.
Unaenjoy life.
Ingawa mimi huwa siumii bt ikishakuwa tofuti huwa namuepuka tu mtu. Japo sibaki na kisasi au manung'uniko.
 
Hongera sana
Natamani nipate uwezo kama huo maana ikitokea tafrani yoyote aisee nakuwa mbogo mpaka badae najishangaa kama ni mimi
Asante mkuu

Inawezekana mbona mkuu,kwangu Mimi ingawa ni nature lkn imeongezeka zaidi kwasababu huwa napenda Sana vitabu vya saikoloji na Maisha kwahiyo imeongeza mambo Kwa kiasi Kikubwa.

So unaweza Anza Leo kupitia pitia mambo then baada ya Mda utaweza kujicontrol
 
Ukiwa hivi inakuwa ngumu sana kuumizwa.
Unaenjoy life.
Ingawa mimi huwa siumii bt ikishakuwa tofuti huwa namuepuka tu mtu. Japo sibaki na kisasi au manung'uniko.
Swadakta hiyo ni njia nzuri ya kukwepa nguvu hasi, ni kujiweka mbali Tu na Maisha yanakuwa mazuri tu
 
Mkuu hapo kwenye kufumania ungesubiri kwanza tukio litokee ndio ujekutuambia kilitokea nini. [emoji3]
Usimtukane mamba kabla hujavuka mto.
 
Maoni yako Yana ukweli kiasi Fulani wala siyapingi.
Nakubali nitaumia lkn siwezi fanya mambo ya ajabu kama kudhuru mtu na mambo kama hayo
 
Mwenyewe unajiona umepitia changamoto,mie nikiweka zangu hapa utafuta uzi wako,maana hizi zako ni trela tu
Sawa mkuu nimepokea maoni yako,
Natamani ije siku ufungue code ili nifute huu Uzi hahaha
 
Back
Top Bottom