Who created God? Who made him? Where did he come from?

Who created God? Who made him? Where did he come from?

Bila google.hawawez kujenga hoja alaf wanakuja hapa.wanaishia ku~attack personality,mungu dhaifu anatengeneza viumbe dhaifu,huyu jamaa ni empty headd

Ni Dhaifu sana huyo Ishmael kwanza anapanic mapema na kuanza kupayuka hovyo.Amekosa mwelekeo sasa anataka kujua jinsia za watu.Sijawahi ona udhaifu kama huu.

Hawa jamaa ni vichekesho,wanashindwa kumthibitisha mungu wao wanabaki kuandika taarabu humu.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nataka nifahamishe waamin kuwa jehanam haipo huko.mnapopajua nyiny,jehanam ilikuwa ni eneo nje ya jerusalem ambapo takataka zlikuwa znachomwa moto hapo,kutokana na hilo.palikuwa na joto sana,na ndipo manabii na mitume walipoanza kuwatisha watu kuwa ukfanya dhambi unaenda jehanam,huu.ni uthibitisho kuwa dini ni uoga...karibu eiyer

Japo sikubaliani na wewe kuhusu kutokuwepo Mungu, ila nakubaliana na wewe juu ya neno Jehanam. Kwa kweli neno hili asili yake ni kiyunani na linatokana na neno, "Gehanoni" likimaanisha jalala au dampo ambalo huchomwa moto uchafu na mizoga kule nje ya jiji la Yerusalem. Na mle palichomwa hata mizoga ya watu waliouawa kwa kutenda makosa mbalimbali ili kuwatisha watu wengine wasitende kinyume na amri za watawala. Jina hili lilichomekwa kwa waamini wa dini kiujanjaujanja lakini hakuna mahali ambapo lina asili zaidi ya hapo.
 
Nithibitishei Hapa KUWA WEWE SIO Mwanamke? Wewe unatupapatikia ndio maana kila kukicha unafuta thread zetu.

Thibitisha kwanza kama wewe sio wale wa vidole juu ama one of kanga moko members sababu umejaa vijembe na maneno ya ki-ke.Kitendo cha kumwambia mtu akuthibitishie jinsia yake mahala pasipo husu ni tabia za upande wa pili.Kuwa makini kijna utawapoteza hata wale wanaokuaminia humu kwa maswali yako ya kukopy na kupaste
 
Your DEITY IS DEAD, ndio maana unatokwa POVU CHAFU. By the way, you can't even PROVE TO ME THAT YOU ARE NOT A WOMAN. So continue to keep your fiendish opinions to yourself and husband.

Ona Ulichoandika sasa,kumbe ndo mana watu wana kuweka kwenye ignore list.Kumbe Kiranga alikuwa sahihi, kama ndo ukipanic unakuwa hivo.
 
Last edited by a moderator:
Japo sikubaliani na wewe kuhusu kutokuwepo Mungu, ila nakubaliana na wewe juu ya neno Jehanam. Kwa kweli neno hili asili yake ni kiyunani na linatokana na neno, "Gehanoni" likimaanisha jalala au dampo ambalo huchomwa moto uchafu na mizoga kule nje ya jiji la Yerusalem. Na mle palichomwa hata mizoga ya watu waliouawa kwa kutenda makosa mbalimbali ili kuwatisha watu wengine wasitende kinyume na amri za watawala. Jina hili lilichomekwa kwa waamini wa dini kiujanjaujanja lakini hakuna mahali ambapo lina asili zaidi ya hapo.

Honest,umeandika vyema,sasa kuna watu humu wanaujua ukweli hawataki kuusikia, hakuna jehanam ya.kidini,na bado kuna mengi nitaendelea kuyaweka wazi
 
Honest,umeandika vyema,sasa kuna watu humu wanaujua ukweli hawataki kuusikia, hakuna jehanam ya.kidini,na bado kuna mengi nitaendelea kuyaweka wazi

Hawa wengi wao wamekaririshwa bila kutafakari hata kile walichokariri.

Mungu gani atuumbe kisha atuahidi kutuchoma moto?.Ili iweje na kwa faida gani?.Huyo mungu gani anayepoteza muda kuhesabu dhambi n mungu kwel!.Dunia dhaifu kama hii bado mtu anasema kuna mungu?.Kaz yake nn sasa.
 
Huku Mtaani kuna hoteli inaitwa Nile

Ikipita miaka 2000 halafu mtu akaja na kusema kuwa hakukuwahi kuwa na mto unaoitwa Nile bali kulikuwa na hoteli iliyokuwa inaitwa Nile na ile hoteli ilikuwa na mambomba makubwa ambayo watu waliyafananisha mambomba hayo na mto na hicho ndicho kilichotokea mambomba yale kuitwa mto nile na hakujawahi kuwepo mto halisi ulioitwa hivyo,[halafu wakati huo kuwe hakuna ushahidi wa kuwahi kuwepo mto Nile ila upo wa kuwepo hoteli]

Je,huyo jamaa atakuwa yupo sahihi kwasababu tu hakuna ushahidi wa kisayansi wa uwepo wa mto Nile?

CC: Mkuu wa chuo Ishmael 2013 TanzaniaLaw Mutabaruka .......!!
Umemjibu sawa sawa na concept yake alivyoijenga, hapo ni yeye kuelewa concept aliyoitumia haina mantiki...
 
Honest,umeandika vyema,sasa kuna watu humu wanaujua ukweli hawataki kuusikia, hakuna jehanam ya.kidini,na bado kuna mengi nitaendelea kuyaweka wazi

Mimi ninayo dini, na nina imani nzuri tu (wastani) na dini yangu. Sasa ninachojiuliza mara nyingi ni baadhi ya maswali ambaye nitayaweka hapa mimi yananitatiza labda tuyajadili kwa pamoja kwa upendo lakini:
1.Kama Mungu katuumba ili tuishi, kuna haja gani ya yeye kutuandalia moto?
2.Kama Mungu anajua hatima yetu tangu tunazaliwa hadi kufa kwetu kuwa tutakuwa ni waja wa aina fulani na tutaishia aidha Jehanam au Penye uzima wa milele kuna haja gani ya kumuacha (yule asiyemtakae) aendelee kufanya ibada kutwa kucha huku akijua wazi kuwa huyu kiumbe ataishia wapi!?
3.Kwa nini Mungu ampe nguvu shetani ya kutusumbua sisi hadi tufike mahali tumuasi Mungu kwa kwenda kwa waganga?
4.Mungu alituumba wa nini endapo anataka kututesa si angekaa tu peke yake?
Hebu tuanze na hayo machache mnipe elimu kidogo ntakuja na mengine baadae.
 
Hiyo dini yako inaonekana imeshindwa kukusaidia kujibu maswali hayo

Ni dini gani hiyo?

Halafu,kwani kwa ufahamu wako wewe Mungu ni kitu gani/nani?
 
Hiyo dini yako inaonekana imeshindwa kukusaidia kujibu maswali hayo

Ni dini gani hiyo?

Halafu,kwani kwa ufahamu wako wewe Mungu ni kitu gani/nani?

Mkuu hujanisaidia bado, unapojibu swali unaanza na Intro, unakuja na Definition, kisha unazama kwenye jibu, na mwisho unatoa conclusion ya jibu lako. Sasa mkuu wewe umeniatack kama ugomvi! Sijakuelewa hasaa!
 
Pamoja na hayo amekuuliza swalik utokana na swali kama kawaida yake akikosa majibu
 
Mkuu hujanisaidia bado, unapojibu swali unaanza na Intro, unakuja na Definition, kisha unazama kwenye jibu, na mwisho unatoa conclusion ya jibu lako. Sasa mkuu wewe umeniatack kama ugomvi! Sijakuelewa hasaa!

Kuna kanuni mbili za kujibu swali

1;Swali linajibiwa na jibu
2;Swali linajibiwa na swali

Lakini kuna maswali mengine hayafuati utaratibu huu,lakini haimaanishi kuwa uko sahihi na hiyo formula yako

Hiyo formula yako ni ya wapi?
Lakini pia pamoja na hayo,kitendo chako cha kuona nimeku atack ni kwasababu hujaelewa kile ambacho nimekuuliza na faida zake na hiyo ni kwasababu umekariri namna swali ambavyo linaweza kujibiwa

Yaani mtu akija na namna nyingine tu unaona hajakujibu kwakuwa ulikariri hivyo

Nilichosema ni kweli kuwa dini yako imeshindwa kukupa majibu ya maswali yako,lakini masawali yako hayo yanajibiwa kirahisi sana na mtu ambae anajua Mungu ni nani/nini,hilo hujaliona kwasababu ya kukariri aina ya kujibiwa ambayo imekufanya ukawa kipofu wakutokuona dunia nyingine!
 
Kuna uthibitisho hapa kuwa hakuna jehanam.ya kidini,yaani hakuna mahali ambako soul inachomwa moto,sasa naona watu wanajifanya hawaoni,kama.hakuna jehanam basi watupe sababu kwanini wamemtengeneza mungu dhaifu
Jehanam lilikuwa jina ambalo Yesu alilitumia kwa mahali pa adhabu ya mwisho kwa watu waovu.

Ni tafsiri ya kiyunani kutoka neno la kiebrania la bonde la Hinomu. Bonde la Hinomu lilikuwa mahali nje ya ukuta wa Yerusalem, kipindi wakati wa ibada ya sanamu Waisrael waliteketeza watoto wao kama sadaka kwa mungu Moleki

Yeremia 7:31 Nao wamepajenga mahali palipoinuka pa Tofethi, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kuwateketeza wana wao na binti zao motoni; jambo ambalo mimi sikuliagiza, wala halikuingia moyoni mwangu.

Mahali palipo fanyika mambo haya Mungu aliwaadhibu kwa mauaji makali sana Yeremia 7:32-34
32. Basi angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo halitaitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu bali litaitwa, Bonde la Machinjo; maana watazika watu katika Tofethi, hata hapatakuwapo mahali pa kuzika tena.

33.Na mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani, na cha wanyama wa nchi; wala hapana mtu atakayewafukuza.

34. Ndipo katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, nitaikomesha sauti ya kicheko na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi; kwa maana nchi hiyo itakuwa ukiwa.

Baadae mahali hapo palikuwa sehemu ya kutupia takataka yote ya mji moto uliwaka huko bila kuzimika Yeremia 19:1-13

1. Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;

2. ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,

3. ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.

4. Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;

5. nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;

6. basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.

7. Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.

8. Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake.

9 Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha.

10 Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,

11 na kuwaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.

12. Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema Bwana, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;

13. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.

Kwanini basi jehanamu lilitumika na Yesu? kwasababu ya kuunganisha mambo yale na hukumu na kuteketeza jehanamu lilikuwa neno lililofaa kudokeza mahali au hali ya adhabu ya milele

Mathayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Mathayo 18:9 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.

Mathayo 23:33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

Yakobo 3:6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

sasa hilo jina sahihi katika kutumika kwa mfano we ulitaka Yesu atumie jina gani? Kufuatana na Agano jipya, adhabu ya Ziwa la Moto(Jehanamu) ni mahali pa mateso Inafananishwa na kuteketea milele bila ya kukoma

Mathayo 13:42 na kuwatupa katika tanuru ya moto, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

Panafananishwa na giza la milele

Mathayo 8:12 bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Mathayo 22:13 Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Na kutengwa kwa milele na Mungu na baraka zake

2 Wathesalonike 1:9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
 
Japo sikubaliani na wewe kuhusu kutokuwepo Mungu, ila nakubaliana na wewe juu ya neno Jehanam. Kwa kweli neno hili asili yake ni kiyunani na linatokana na neno, "Gehanoni" likimaanisha jalala au dampo ambalo huchomwa moto uchafu na mizoga kule nje ya jiji la Yerusalem. Na mle palichomwa hata mizoga ya watu waliouawa kwa kutenda makosa mbalimbali ili kuwatisha watu wengine wasitende kinyume na amri za watawala. Jina hili lilichomekwa kwa waamini wa dini kiujanjaujanja lakini hakuna mahali ambapo lina asili zaidi ya hapo.
hapo nilipoweka red unaweza ukapitia maelezo yangu kuhusiana na Jehanamu nime m quote mtu nikimpa jibu... hapo juu
 
hapo nilipoweka red unaweza ukapitia maelezo yangu kuhusiana na Jehanamu nime m quote mtu nikimpa jibu... hapo juu

Sasa mkuu si keshasema limechomekwa kiujanja ujanja?
Hayo maandiko si atakuambia ndio yaliyochemekwa kiujanja?
 
Sasa mkuu si keshasema limechomekwa kiujanja ujanja?
Hayo maandiko si atakuambia ndio yaliyochemekwa kiujanja?
nadhani mtu wa namna hiyo hayupo kuelewa... ukimuomba ushahidi kama limechomekwa kiujanja ujanja bado atakosa jibu! hawa watu ni watu wa ajabu sana, yaani mtu yupo radhi kuamini kwamba mambo fulani fulani yamechomekwa kiujanja ujanja kana kwamba alikuwepo enzi hizo... ila ukimwambia hivi anabisha
 
Maana iko hivi kama ukiweza kujibu swali alilokuuliza inamaana inaua hoja yako...

Hawa watu bana sijui wakoje tu

Na sijui ni shue gani wamesomea
Sisi wengine elimu yetu ni STD 7 lakini tulisoma siku nyingi kidogo na waalimu walitufundisha namna ya kujibu maswali

Mtu akikuuliza swali unaweza kumpa jibu au swali ambalo kama atalijibu atakuwa amepata jibu la swali lake

Mfano;mtu akikuuliza kuwa "Kama Yesu ni Mungu,wakati yupo Israeli nani alikuwa akifanya kazi zake nyingine maeneo mengine"?

Huyu unaweza kumuuliza swali badala ya kumpa jibu,unaweza kumuuliza "kwani Mungu ana uwezo gani"?

Jibu la swali hili lina jibu la swali lake,yaani kama Mungu anaweza kila kitu na yupo kila mahali hiyo inakuwa imempa jibu kuwa anaweza kuwa yupo Israeli kama Yesu lakini wakati huo huo akiwa eneo lingine kwasababu anaweza kila kitu na yupo kila mahali

Hiyo kanuni ndogo tu ambayo sisi tulifundishwa darasa la tano imewashinda,au shule za siku hizi zimekuwa za ajabu hivi?
 
Back
Top Bottom